Rostam Aziz: Historia ya Dkt. Slaa haimpi uhalali wa kujifanya anajali maslahi ya Mtanzania. Kampuni zangu hazihusiki na uwekezaji wa DP World

Mbunge Mstaafu wa Igunga bilionea Rostam Aziz amesema yeye anafanya kazi na sekta Binafsi hafanyi Kazi na Serikali sasa atakuwaje Fisadi?

Rostam amesema hajawahi kuomba ku-supply hata Sindano serikalini sasa atakuwaje Fisadi!!

Sina skendo yoyote katika Biashara Zangu na sifanyi Biashara ya Bandari ila Ikitokea fursa sitaiacha , amesisitiza Aziz

Source: Jambo TV
 
🤣🤣🤣Nilifika Igunga mwaka jana, aiseeh ni aibu tupu, 🤔 huwezi dhania rostam alishakuwa mbunge pale,pamechoka,mji hauna stend,soko,haueleweki senta iko wapi,yaani vululu vululu.
 
Yaani wameongea Wanasiasa wote mashuhuri Mbowe, Prof Lipumba, Dr Slaa, mzee Wassira, mzee Warioba, Jenerali Ulimwengu nk lakini aliyemtoa pangoni Mfalme wa Siasa za Tanzania alhaj Rostam Aziz ni Dr Slaa

Aisee Dr Slaa bado ana Nguvu na Ushawishi mkubwa

Ujue hapo alipo hana Chama ananyemelewa tu na Umoja Party lakini moto anaowapelekea Mafisadi Tundu Lisu anasubiri mbali kabisa yaani Mbagala huko

Mungu mbariki Dr Slaa
Ccm Kahama lini mara ya mwisho alikuwa balozi
 
Ila ni kweli, huyu mzee alichowafanyia CDM hakiwezi kusahaulika kamwe.
 
Binafsi siwezi msikiliza Dr Mihogo na Njaa zake badala yake nitamsikoliza na kumpa attention Rostam Kwa sababu kwanza ni mlipa Kodi na Mwajiri ila huyo mwingine ni njaa zinamsumbua ni WA kupuuzwa ,ameshazeeka hana jipya Kwa umri wake..

---

“Huyu ndugu yangu Dkt. Slaa sijui nimjibu nini maana historia yake haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania, siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.” – Mfanyabiashara Rostam Aziz

Dr Mihogo siku hizi haeleweki anasimamia nini
 
Atuambie kama yake yeye Rostam ina uthubutu wa kuongea!
Dowans ilikuwaje!

umiliki wa vodacom aliupataje!
Waandishi wa habari alikuwa anawanunua kwa sababu zipi!
Bora angekaa kimya kuficha uovu wake!
 
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

---

Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.

Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.

Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.

Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.

Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.

Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.

Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.

Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.

Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.

Huyu Bwana Dkt. Slaa anaangalia maslahi yake binafsi, hakuwa mwanachama wa CHADEMA bali alipoona jina lake limekatwa (alipogombea kupitia CCM) ndio akahamia CHADEMA

Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu

Historia ya Dkt . Slaa inatosha kabisa kueleza kuwa yuko tayari kupandikiza chuki na uhasama kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa Kiswahili kifupi huyu jamaa (Dkt. Slaa) ni 'kizabizabina' ni fitina, mbinafsi. Na ni mtu wa kusema chochote na lolote na wakati wowote kwa maslahi yake binafsi"

Dkt. Slaa ananiita mimi fisadi, sasa mimi (Rostam) nafanya kazi na sekta binafsi wala sifanyi kazi na serikali nakuwaje fisadi, kwa hiyo nawafisadi sekta binafsi wenzangu, je watakubali nao? Sijawahi kupata skendo ya serikali na wala sijawahi kuomba ku-supply hata sindano serikalini

---

My Take

CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani

Nchi imejaaa rushwa nyingi nyingi na kubwa kubwa ,mpaka wafanyabiashara wezi wanajuhamin na kuanza kutukana na kukejeli wazawa.Huyu Rostam ni mhuni mhuni tu.Mjinga mjinga tu.Mwizi mwizi tu.Anajihamin kabisa kuwa yete ndiye bosi wa nchi hii.
 
Kumbe Dr alinunuliwa,akapata nauli akaenda zake Canada,alambishwa asali akatulia.Baada ya ubalozi karudi kusumbua.Kumbe ukilambishwa asali unatulia
 
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

---

Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.

Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.

Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.

Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.

Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.

Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.

Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.

Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.

Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.

Huyu Bwana Dkt. Slaa anaangalia maslahi yake binafsi, hakuwa mwanachama wa CHADEMA bali alipoona jina lake limekatwa (alipogombea kupitia CCM) ndio akahamia CHADEMA

Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu

Historia ya Dkt . Slaa inatosha kabisa kueleza kuwa yuko tayari kupandikiza chuki na uhasama kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa Kiswahili kifupi huyu jamaa (Dkt. Slaa) ni 'kizabizabina' ni fitina, mbinafsi. Na ni mtu wa kusema chochote na lolote na wakati wowote kwa maslahi yake binafsi"

Dkt. Slaa ananiita mimi fisadi, sasa mimi (Rostam) nafanya kazi na sekta binafsi wala sifanyi kazi na serikali nakuwaje fisadi, kwa hiyo nawafisadi sekta binafsi wenzangu, je watakubali nao? Sijawahi kupata skendo ya serikali na wala sijawahi kuomba ku-supply hata sindano serikalini

---

My Take

CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Toka 2015, ndy leo yazungumzwe hayo!
Tunategemea Hoja!
 
Ni kama anatutukana watanzania wote with His body language and attitude 🚮🚮
 
Back
Top Bottom