Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Katika suala la kupambana na UFISADI kuna waliofikiria wakati MAFISADI wanajibu mapigo, wataonekana kirahisi. Lakini mpaka sasa lazima watu wajue mafisadi ni watu hatari sana wanaweza kutokea usipotegemea.

Mafisadi wanajua loop hole zilipo na kwa Chadema naona waliijua mapema, hata kabla Chadema hawajajua.

Sasa hizi tuhuma za aliyekuwa Makamu mwenyekiti kuiba sijui nini hii tumefika mbali!!.
 

CHADEMA imekuwa ikishughulikia mambo yake ndani. Mambo mengi tu ya mazito na ya siri. Bila hayo kutoka nje.

Lakini katika hili la Chacha naona mambo mawili:

1. Chacha mwenyewe ameamua kuwamwaga hadharani kupitia Mtanzania na Rai kabla na kupotosha mijadala ya vikao; hivyo Mbowe na Tundu Lissu ilibidi wajitokeze kumwaga hadharani ukweli kwa niaba ya chama.

2. Hapa huyu mtu anayeitwa Paparazi Muwazi ndiye aliyemwaga haya ya Chacha na UDSM na Chacha na Mkewe. Na huyu si mwanaCHADEMA. Sasa kama mambo yamemwaga hapa, sisi kama wanaCHADEMA tunakosa gani kuuliza kama ni ukweli au uwongo ili tupate maoni ya watu wengine ikiwemo viongozi wetu wa CHADEMA wanaopita hapa? Wasipojibu hapa nitawauliza vikaoni

Asha
 

Si unaweza ukampigia simu ukamuuliza chacha mwenyewe, au waogopa?

Hivi wakati mwanachama wenu anapojaza form za kuomba uongozi, hakuna swali la kuuliza criminal hitory yake. Kama lipo Chacha alilijaza vipi? kama aliandika hakuwa na criminal history yeyote, je alidanganya? na mwanachama anapodanganya sheria za chama chenu zinasemaje?
 


Nitawafikishia ujumbe wako.

Kwani uliambiwa wanaopiga kura ni wanachama tu? CCM yenyewe ina wanachama milioni 4 tu. We uliambiwa watakaompigia kura Obama ni wanachama wa Democrat tu? Suala la kuangalia ni jinsi gani CHADEMA itawatumia wanacham wake milioni moja kupata kura milioni 10. Kila mwanachama akitafuta kura kumi tu, tayari CHADEMA inachukua dola.

Asha
 

Nimempigia jana, ameniuliza kwani wewe ni nani na kwanini unataka kujua hayo? Amesema nimpigie akiwa na nafasi. Labda jaribu na wewe kumpigia au Mwanakijiji ampigie amhoji hayo. Maana naona wanapatana

Asha
 

Suala la wanachama ni muhimu, kama CCM wana wanachama 4000 tu, kwa nini nyie msiwe na wanachama 5000 au 6000. Hii itawasaidia kupata wabunge wengi pia. Independents wengi si wapiga kura! jengeni chama, bla bla zimeshatosha sasa na Mbowe asigombee tena urais 2010, ameshachuja kama alivyochuja Lipumba na maalim Seif.
 

Vita ya panzi, furaha ya kunguru. Chadema waache porojo zao kwenye media, wakae chini na kutatua matatizo yao ndani. Hii inatuletea wasiwasi sisi ambao tumekiamini chama na tunaona kwamba ni mtetezi wa wanyonge. Sasa leo wanaanza kutupiana matusi. Je tutafika kweli?
 

Nimerudia tena kuusoma huu uchambuzi. Haya ni maneno mazito

Asha
 
Asha
Suala la kuangalia ni jinsi gani CHADEMA itawatumia wanacham wake milioni moja kupata kura milioni 10. Kila mwanachama akitafuta kura kumi tu, tayari CHADEMA inachukua dola.

Duh!! Chadema ina wanachama 1m!!!! Hawa si kama wale clayanti wa Voda???



Nawe!??! nani kakwambia milioni nne inaandikwa 4000!!!!
 
Duh!! Chadema ina wanachama 1m!!!! Hawa si kama wale clayanti wa Voda???




Nawe!??! nani kakwambia milioni nne inaandikwa 4000!!!!

Nilikuwa nawaza kipesa pesa, hebu zidisha mara elfu moja hapo chap chap!
 
Umemaliza Kila Kitu.
 
Tukubali kusaidiwa na Idara zinazoheshimika kama TISS kwenye SCREENING ya viongozi wetu hasa wa KITAIFA. Naamini hili lingefanyika tusingekuwa na watu kama LOWASSA, KARAMAGI, WANGWE,... Kwani MWALIMU alikuwa anafanyaje enzi za Urais wake?

Wilcard,
TISS haiheshimiki tena. Kumejaa watetezi wa ufisadi kule.
 
Moderators

Mpaka sasa kuna thread zaidi ya tano zote zinamzungumzia Chacha Wangwe na CHADEMA. Naona zinajaza uwingi hapa. Nashauri zote ziunganishwe chini ya thread moja ili mjadala uweze kufuatiliwa kwa urahisi

Asha
 


hakuna kumsubiri atoroke mi naona tuandamane ili akamatwe achukuliwe hatua za kisheria (nimesema tuandamane ili kushinikiza maana tukisubiri hawatamkamata si tunajua uswaiba wake na kikwete) hawezekani kwenye soo zote kama richmond na EPA tukose ushahidi wa kumtia hatiani huyu.
 
PM

Kila nikiangalia bungeni simuoni Chacha. Yuko wapi? Anawawakilishi vipi wananchi wa Tarime kama haendi bungeni?

Sasa mbona kiongozi wa upinzani Hamad Rashid wa CUF aliposema Chacha ni mtoro Chacha alikanusha?

Asha
 
PM

Kila nikiangalia bungeni simuoni Chacha. Yuko wapi? Anawawakilishi vipi wananchi wa Tarime kama haendi bungeni?

Sasa mbona kiongozi wa upinzani Hamad Rashid wa CUF aliposema Chacha ni mtoro Chacha alikanusha?

Asha

Jamani PM uko wapi? Hebu endelea kutumwagia mambo

Asha
 

Lile shinikizo la Sitta nililowaeleza limefanya kazi na wote mmeshuhudia jinsi KKKT walivyomkana Rostam. Kutokana na KKKT kumwahi Rostam kabla ya yeye kufanya tukio na waislamu sasa amesitisha mpango huo, badala yake amejizatiti kupingana na tamko la KKKT kiufundi. Amejiandaa kufanya propaganda kupitia Majira na Tanzania Daima kwamba tamko la KKKT limetokana na inda ya bwana Sitta na Mwambalaswa. Bila kuwashambulia moja kwa moja ataeleza wazi michango ambayo ameitoa kwa KKKT siku za nyuma na kueleza wazi kuwa wao ndio waliomualika wakati huo. Timu yake ya mkakati imechukua uamuzi huo baada ya ukweli kwamba baada ya KKKT kutoa tamko hata waislamu anawatumia nao wamesita sita. Wakati huo huo,timu ya mkakati ya Bwana Rostam inaendelea kutafakari jinsi ya kumwingiza Bwana Mengi kama mmoja wa watu waliofanya shinikizo zaidi ya Sitta kwa KKKT kutoa hilo tamko. Bwana Mengi ni mmoja wa waumini wa KKKT. Napo katika KKKT bado moto unafukuta Kinondoni, huku baadhi ya watu ikiwemo mchungaji wakipinga hatua za kinadhamu zilizochukuliwa. Na Bwana Rostam amekuwa katika mawasiliano nao wakati wote.

Wakati huo huo, kile kikao cha Bwana Chacha Wangwe cha Dar es salaam kimefanyika, kwa kiasi kikubwa mjadala uliofanyika hapa ambao bwana Balille alipeleka nakala umeathiri mipango yao. Bwana Rostam ameanza kumwona Chacha Wangwe kama mzigo. Ule mpango wa kuwaibua mashujaa wengine unaendelea ingewaje uzito wa viongozi hao umeonekana mdogo sana. Mkakati unafanyika wa kujaribu kumweka upande wa Chacha kiongozi mmoja mwandamizi wa CHADEMA(jina nalihifadhi kwa sasa). Wakati hayo yakiendelea imekubaliwa kwamba Bwana Dr Paul Kyara, Mwenyekiti wa SAU, mchagga ambaye alinyimwa nafasi ya uongozi CHADEMA kuepusha ukabila na hatimaye akaamua kujitoa chama hicho na kuanzisha chama chake; amuunge mkono Chacha Wangwe katika kuishambulia CHADEMA. Tayari bwana Kyara amepewa fedha na Rostam kuzunguka kuunga mkono madai ya Chacha Wangwe kuwa CHADEMA kuna ukabila, wachagga wanapendelewa na kwamba yeye amewahi kuwa makao makuu ya CHADEMA na anajua kwamba ruzuku zinatumika vibaya. Bado Bwana Rostam amemtaka Chacha Wangwe kuendelelea kubaki Dar es salaam wakati wanaendelea kutafuta 'mashujaa' wengine wa kumuunga mkono. Katika kukaa kwake Dar es salaam, ilikubaliwa kwamba Chacha Wangwe aitishe maandamano ya wanaCHADEMA Dar es salaam ya kumuunga mkono kutoka Temeke Mwembe Yanga mpaka Kinondoni Ndugumbi ya kuunga mkono hoja yake kwamba ruzuku ya CHADEMA haipelekwi wilayani. Chacha Wangwe aliwasiliana na viongozi wa Temeke kuandaa maandamano hayo. Hata hivyo viongozi wa CHADEMA Temeke walichukizwa na uamuzi wa wanaojiita wanachama wa Dar es salaam 20 wanaomsaidia Chacha Wangwe ambao wamesambaza waraka kwamba Chama hakipo Dar es salaam kokote kwa kuwa watatu kati yao walisimamishwa kuwa viongozi wa CHADEMA Dar es salaam, na kwamba suala hilo limeua uhai wa chama Dar es alaam kiasi kwamba hata mikutano ya hadhara haifanyiki. Suala hili liliwaudhi watu wa Temeke badala ya kuandaa maandamano wakaandaa mkutano na waandishi wa Habari na kutangaza wazi kuwa Chacha na watu wake ni waongo, Mkoa wa Dar es salaam ulishavunjwa na kwa mujibu wa mabadiliko ya Katiba ya 2006 Dar es saalam ni Kanda, Mikoa yake ikiwa wilaya za sasa za kiserikakali na kwamba wao Mkoa wa Temeke wanapokea ruzuku ya chama kila mwezi, wanaofisi ambayo si ya kukodi inamilikiwa na CHADEMA yenyewe pamoja na kiwanja, na pia wana utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara kila weekend; hivyo madai ya Chacha na wanachama hao wa Dar es salaam yamelenga kugawa makundi katika chama. Mzee Kikoti Mwenyekiti wa Temeke akatoa mwito kwa chama kumvua uanachama Wangwe. Matokeo ya Tamko hilo ni Chacha kumpigia simu mratibu bwana Semkwai pamoja na Kikoti na kuwatukana matusi ya nguoni pamoja na kuwatisha. Kutokana na hali hiyo, Chacha amesimamisha maandamano hayo kutokana na kukosa mahali pa kuanzaia na anafikiria kufanya utaratibu mwingine.

Kikao kingine kati ya Chacha na Ballile bila ya Rostam kitafanyika tena Dar es salaam, nitawajulisha yatakayojitokeza

PM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…