Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Na Chama cha wachaga siku kikipata mfadhili kama Rostam unafikiri hawatmkumbatia!na wachaga wanavyo penda pesa!!

Wewe umesema.

Kumbe ni kweli mvuto wake ni kugawia pochi viongozi wa SISIEMU?

Wachaga wanajua BOT ndiko kwenye Pochi kuliko kwingine kokote, Mbona kwenye ile LIST OF SHAME kuna mchagga mmoja tu?
 
Kama memba toka jimboni kwake anaweza kuwa na jibu zuri kuhusu huyu mbunge....
 
Kama memba toka jimboni kwake anaweza kuwa na jibu zuri kuhusu huyu mbunge....
Kuwanunua watanzania haikugharimu pesa nyingi. Njaa ndiyo inayowamaliza watanzania walio wengi. Mimi nimeshuhudia watu wakinunuliwa chai na vitumbua ili wamchague mtu fulani (aah, Manju Msambya) wakati nikiwa mdogo na alifanikiwa kupita. Kwa hizo pesa wanazoiba watatumaliza kwani bado wapo wengi wasiofahamu athari za kuuza utu wao.
Rostam ni mwizi kama wezi wengine, na anachogawa si chake bali ni makapi ya mali alizoiba za watanzania.
 
paspo kujali rangi,sura,chama,kabila,dini,jinsia,itikadi......WATU KAMA HAWA.......(richmond&billcanas)
hata kama wana michango ni ya kutunyonya sisi watanzania.....UTAJIRI ISIWE KIPIMO CHA WAO KUGOMBEA.....NI MAFISADI HAWA........
DOWN..DOWN.....ROSTAM...!
DOWN..DOWN...MBOWE...!
DOWN..DOWN..BUZWAGI...!
DOWN..DOWN...BULYANHULU....!
DOWN..DOWN...LOLIONDO....!
DOWN..DOWN...NYARI(alitolewa lupango kwa mashinikizo ya walanchi)
DOWN..DOWN..MAFISADI HATA KAMA NI MA-MEMBER HUMU JF!
 
Inashangaza sana kuona Mbunge hajakamilisha kujaza forms ambazo zinapaswa kuwa public, na hii ni dalili kuwa anaweza akawa hajakamilisha kujaza forms za kutangaza mali na madeni yake. Au anaweza akawa amejaza lakini figures zisiwe sahihi.

Niliwahi kuuliza pale Maadili kuwa inakuwaje kuhusu mwenendo wa umma anayeenda kinyume na maadili? wakanijibu ni budi pawepo na malalamiko rasmi yapelekwe kwao kwani ndivyo sheri inavyowabana, hus Muungwana akaona hiyo haitoshi na anataka wawe na meno ila naongezea wapewe meno ya kumng'ata yeyote kisheria..... Pasiwepo na yeyote above the Law of the Land
 

Ukitaka kumjua Rostam ni nani kwenye serikali ya JK basi fika pale Movenpick utajionea mwenyewe.Kuna mtu aliwahi kuandika hapa hilo nami nikaamua kufuatilia ni aibu kwamba mawaziri hufika kwa King wao na kupanga mstari kumuona akiwa anakunywa chai na hata wao huondoka na chochote pale .Kama huwezi basi ulizia pale Movenpick utajua mengi ya huyu jamaa .
 


Hii ni ishara moja kubwa sana inayoonyesha kuoza kwa system yetu, Inawezekana vipi kuingia bungeni kwa kadiri ya kipindi cha miaka mitatu na bado unao wawakilisha hawafahamu ukweli wa maisha yao. Absolutely ridiculous.
 
Hivi amewahi kusema nini Bungeni, kuuliza nini, kupinga nini, kuunga mkono hoja gani, kwanini vyote vilivyosemwa havionekani na hajapewa credit? Ina maana hata wapiga taipu wa Bunge wako mfukoni? anaogopwa, anaogopesha?.
 
Kuna siku itafika pale bongo patawaka moto. Haya mambo ya kuona kila kitu ni sawa tu yataisha na wengi wataishia Ukonga na Keko.
 
Nadhani Rostam anaushawishi mkubwa katika ku-lobby kwa siri-kali makampuni ya kitapeli kama Richmond, etc. Ametajwa huko, lakini pia inawezekana anaushawishi kwenye vyombo vya habari ili asitajwe kiasi cha kutosha kwenye kashfa kadhaa. Dua la kuku halimpati mwewe? Rostam ni mwewe....wananchi ni kuku!! Rostam si mfano wa kuigwa.
 
Binafsi napinga mafisadi wa kila namna si wa kuchagua kama baadhi yetu....kuanzia UZINIFU wa KUKUBALIANA hadi BOT,EPA, BUZWAGI,TRA na MENGINEYO

Ni kweli RA anatuhumiwa kwa mengi, lkn mtoa mada na wachangiaji washaanza kubwabwaja bila facts alizouliza Muanzisha Mada. Sifikiri hili ndilo tunalohitaji hapa JF, unless the everything zitajaa FIKRA moja.

MKJJ its good idea kuja na hio analysis zako, lkn umekuwa so specific juu ya RA tu!!! sikatai upo huru, lkn ningependa kuweka ktk broad mind ya analysis zako.

1.Kwanza website ya Bunge ina mapungufu mengi sana hasa kuhusu updates za yanayoendelea Bungeni on day to day basis...mtakumbuka CV ya Wassir hadi sasa haioneshi kuwa kasomea Masters...somebody from JF kaleta data nyingi kuwa Wassira ana elimu so n so...lkn website ya Bunge bado haijawa updated!!!

2. Je wabunge wengine out of RA nao wamechangia nini?....nafikiri kwa nature ya bunge letu lilivyo wengi hukaa kimya huko Bungeni...

3. Vipi wale wanaolala na kupigwa picha LIVE...nao wanachangia nini au wametumwa kulala Bungeni?

4.Huko Nyuma tuliwahi kujiuliza hivi Bungeni wabunge wa Upinzani ni Zitto na Slaa wengine wapo wapi?...niliwahi kusikiliza Vipindi vya CUF vya kampeni thru redio wakasema yapo mengi tu ambayo wabunge wa upinzani wanachangia lkn si wenye kujulishwa Wananchi...in this case kuna uwezekano wa Maoni mengi ya baadhi ya wabunge kutoandikwa!!!

5. Hivi Mbunge kama huna cha kuzungumza yapasa uwe unapayuka tu?ili mradi uwe unajiongeza credits(kupata umaarufu)?

6. Ikiwa Spika ndie kinara wa Bunge assume yeye ni Mwalim Darasani na mwanafunzi maarufu darasani haulizi maswali wala hashiriki group works, Je nani anahitajika kumweka sawa mwanafunzi? kwa Mtaji huu ni vema pia spika akaeleza Ummah kwanini Mbunge so n so hashiriki ipasavyo Bungeni? au yeye spika kazi yake kuombwa Ruhusa na wabunge wanazamia msituni.??..kama vile wanafunzi wa shule ya Msingi wanavyoingia mitini...

7. Ni vema kujua kila mtu talents zake...na ndio maana Vyama vyetu vingi tu vimewaweka watu makada, Kampeni managers + vyombo vya sanaa kupoteza muda kwa wananchi...wale wabunge wenyewe wanakuja kuongea dk 5. In this case kuwapata wabunge ambao si wazungumzaji Bungeni ni wengi.na Wabunge wanaofanya Kampeni zao wenyewe wachache sana...its possible ikawa RA ni miongoni mwao....lkn Hii isiwe kigezo au Kipimo cha kupima mchango au utendaji wake ktk Jamii yetu...Nashauri tuangalie vigezo vingine vya Kupima Utendaji wa Mbunge...

8. Ikiwa RA tushamweka wazi juu ya UFISADI why tena kuangalia mchango wake? Tunahitaji kumsamehe au kumsafisha???Tell me akija Spika au Mtendaji wa Bunge akaleta michango ya RA...JF tufanyaje??
 

8. Ikiwa RA tushamweka wazi juu ya UFISADI why tena kuangalia mchango wake? Tunahitaji kumsamehe au kumsafisha???Tell me akija Spika au Mtendaji wa Bunge akaleta michango ya RA...JF tufanyaje??

Mkuu Chuma,
Nimeshindwa kuelewa hii conclussion yako, kuwa ilikuwa kumtetea RA au ilikuwa kuchambua hoja. Hebu fafanua hii sentesi yako.
 
Chuma, umesoma zaidi ya kile nilichouliza. Sijauliza kuhusu wabunge wengine kwa sababu sijawasikia wakitajwa kuwa na nguvu anayotajwa kuwa nayo RA; Hakuna mbunge mwingine ambaye anahusishwa na mambo yachanganyayo kama Rostam. Ni ni kwa sababu hiyo sikuwaangalia wabunge wengine wote 320, kwa sababu huo muda binafsi sina!

Nimemchagua Rostam kutokana na jina lake kutangaa katika masuala mbalimbali na nimeuliza kwa sababu licha ya mapungufu mengi ya tovuti ya Bunge, kushindwa hata kuweka mwaka aliozaliwa ni upungufu unaopakana na uzembe! Ni bora kuweka taarifa kiasi unavyozijua kuliko miaka miwili baadaye kushindwa kuweka taarifa za uhakika za mmoja wa wabunge maarufu nchini! Hakuna excuse, none whatsoever.

Na ndio maana katika kuchambua siyo suala la Bungeni tu, binafsi ningependa kujua Bw. Aziz amefanya nini kuchangia kwenye TAifa letu ? Hayo ya wabunge wengine nitawaacha wengine waulize, na hayo mambo ya "broad analysis" nitawaacha wengine, la kwangu ni kuhusu Rostam.

Huku mbeleni nikiwa interested na kujua ya kiongozi mwingine, believe me sisiti kuuliza. So, kama unajibu naomba unisaidie, kwa ufahamu wako kuhusu Bw. Aziz (na mimi sijamtaja kama fisadi wala kumuweka kwenye orodha ya mafisadi ni wewe umemhusisha na ufisadi) amefanya nini katika kuchangia kwenye Taifa ambacho kingepaswa japo kidogo kuwekwa kwenye tovuti ya Bunge?
 

BWANA MWANAKIJIJI SI BUSARA KUANZISHA THREAD NA KUOMBA WATU WACHANGIE HUKU UKIJA WEWE MWENYEWE NA JINA HILI LA MADELA KUJIJIBU.

SEMA KAMA UNA NIA YA KUMCHAFUA ROSTAM INGIA MOJA KWA MOJA HUO NI UTOTO. ROSTAM ANA ELIMU YA KUTOSHA HUWEZI KUMFANANISHA NA BOSI WAKO (MBOWE) ALIYEKIMBIA SHULE -HULL, ROSTAM KASOMA OXFORD WEKA REKODI ZAKO.

LAKINI LAZIMA UJUE KUWA KWELI ROSTAM ANA POCHI KAMA UNA SHIDA UTAPEWA NA WATU KAMA WEWE ULIYENUNULIWA NA MBOWE KWA KUFUNGULIWA WEBSITE TU NDIO UNAPATIKANA KIJINGA KABISA.

ROSTAM KAANZA UBUNGE MIAKA MINGI SIO 2005 NA HUKO IGUNGA USIFIKIRI CHADEMA INAWEZA KUPATA HATA DIWANI KWA MUDA ATAKAOKUWA ROSTAM KAMA MBUNGE.

SWALI UNGEWAULIZA WATU WA IGUNGA KABLA YA KUTULETEA SISI JF.

KAMA KWELI CHADEMA CHAMA MBONA HATUJASIKIA MKAENDA IGUNGA KUONGEA NA WANA IGUNGA AMBAO SIO MEMBERS HAPA JF ILI KUWAFAHAMISHA HABARI YA ROSTAM?

NADHANI KAMA KUNA KITU AMBACHO NINGEKUONA MWAMBA NI KWENDA IGUNGA AU KUMBWAMBIA BOSI WAKO APELEKE MKUTANO UONE KAMA WATU KUMI WATAKUJA KUKUSIKILIZA.

NA UNAJUA KUWA TABORA NDIKO KWENYE CHIMBUKO LA VYAMA VINGI 1962 MZEE KASANGA TUMBO NDIYE ALIYEACHA UBALOZI-LONDON NA KWENDA KUANZISHA UPINZANI. 1990s KUNA MAPALALA NA CHIFU FUNDIKIRA KAMA VINARA WA MAGEUZI NA KUNA PROFESSOR LIPUMBA KAMA CHACHU YA UPINZANI HADI BOSI WAKO MBOWE ALIKUWA AKIPELEKA KURA YAKE URAIS HUKO.

PAMOJA NA KUWA NA HISTORIA KUBWA YA UPINZANI HALISI(TABORA) LAKINNI IGUNGA-TABORA BWANA ROSTAM ANA PENDWA KULIKO WEWE AU KITILA ANAVYOMPENDA MBOWE, MAANA WEWE UNAPENDA MTU SI CHAMA.
 
Wewe umesema.

Kumbe ni kweli mvuto wake ni kugawia pochi viongozi wa SISIEMU?

Wachaga wanajua BOT ndiko kwenye Pochi kuliko kwingine kokote, Mbona kwenye ile LIST OF SHAME kuna mchagga mmoja tu?

MBONA HUULIZI RIPOTI YA EPA KWANINI INACHELEWA? NI WACHAGA AKIONGOZA MAMA ANNA MKAPA MWENYEWE.KUNA MRAMBA NDANI.

MAMA MKAPA ANA KAMPUNI 13 AKIKAMATWA JEETUL-PATEL BASI NA MAMA MKAPA NDANI.KIGUGUMIZI KALETA MAMA MKAPA NA MKAPA HAISHI KULIA KWA JK(CHONDE CHONDE NIHIFADHI KIJANA WANGU) NDIO MAANA MKAPA ALIKUWA ANAMTAKA SUMAYE ILI AJIHIFADHI.

SASA KAMA NYINYI WAPIZANI MNA NIA YA KWELI FANYENI KAMA KWA CHILUBA.MWAKYEMBE KASEMA HOSEA HAFAI NA MAKATIBU MBONA HAMJAANDAMANA KUSHIKIZA WAONDOKE? CHADEMA MNAGANGA NJAA TUU.
 
Wakati huo huo, Mchungaji Mtikila ametaka Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, akamatwe mara moja kwa kuwa anaishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria.

(Tanzania Daima)

Mchungaji Mtikila alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini, na kusena kuwa Rostam ni kama hana uraia na Tanzania.

Alisema Rostam ni raia wa Iran na aliinngia nchini miaka ya hivi karibuni akiwa mfanyabiashara wa ngozi baadaye kuingizwa kwenye siasa na viongozi wa serikali.

Alidai ana ushahidi wa kutosha hadi hospitali aliyozaliwa mbunge huyo na kwamba hadi sasa wazazi wake wanaishi nchini Iran.

“Rostam ni rafiki yangu mkuu, lakini siwezi kumtetea kuliko nchi yangu. Hata maandiko matakatifu yanaonya kuwa ‘msimtawaze mgeni kuwa kiongozi wenu ila atoke kati yenu’. Ushahidi upo kuwa bado ni raia wa Iran na hajawahi kuomba uraia mwingine popote,” alisema Mtikila.

Ameapa kwamba kama Rostam hatakamatwa atashirikiana na wananchi kumkamata na kumfikisha mahakamani pamoja na wale waliomfanyia mpango akapata nafasi ya kuwa mbunge.

Mtikila alisema kuwa katiba ya Tanzania inatamka kuwa mgeni yeyote ambaye wazazi wake si raia wa Tanzania, hata kama amezaliwa nchini, akitaka kuwa raia sharti kwanza akane uraia wa wazazi wake, kisha aombe uraia wa Tanzania kwa kutangaza kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi, ili kama wananchi wana pingamizi waweke.

Alisema Rostam alipoingia nchini akiwa mfanyabiashara wa ngozi, akakutana na baadhi ya viongozi walioingia nao urafiki kwa ahadi kuwa atawasaidia kwenye uchaguzi mkuu, kisha akanunua kiwanda kimoja cha ngozi mkoani Morogoro kwa msaada wa nchi ya Iran.

Mtikila alisema wakati Rostam akiwa nchini, aliyekuwa mbunge wa Igunga wakati huo, Charles Kabeho, alifariki ndipo viongozi waliokuwa wakimbeba wakampatia jimbo hilo, ambalo amedai kuwa anaamini lipo wazi hadi uchaguzi utakapoitishwa na kumpata mbunge mzawa.

“Iwapo hatakamatwa kwa kudanganya uraia, wananchi tutamkamata, kwani ushahidi upo hata hospitali aliyozaliwa jina tunalo,” alisisitiza.

Aidha, Mchungaji Mtikila alisema wana-CCM wanakwenda kufanya mkutano Butiama ili kuungama madhambi waliyotenda kutokana na kutofuata maagizo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Alihoji uhalali wa mkuatano wa CCM unataotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kufanyikia Butiama, wakati walimdhihaki Mwalimu Nyerere kwa kuuza nchi.

Aliwashauri viongozi wa chama hicho wanaotarajiwa kwenda katika mkutano huo utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu, kujiuzulu nyadhifa zao na kutubu makosa kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere.

“Wanapelekana alikozikwa Mwalimu Nyerere waliyemuumiza moyo akafa kabla ya siku zake, kwa kupora nchi na kuiuza...ni vema kama wote wanakwenda kuungama na kujiuzulu, lakini kama wanakwenda ‘kuusanifu’ mzimu wa Mwalimu Nyerere, utawamaliza.

My Take:

Je hili laweza kuelezea kwanini Bunge wanashindwa kusema Rostam alisoma shule gani ya msingi na sekondari, au hata chuo kikuu? Maana hawawezi kusema alisoma shule ya Msingi ya Igunga mwaka fulani wakati waliosoma wapo watamuumbua? Rostam alizaliwa wapi, na wazazi wake wako wapi?
 


Kwa mujibu wa Mtikila, Mkapa naye si raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…