KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
Na Chama cha wachaga siku kikipata mfadhili kama Rostam unafikiri hawatmkumbatia!na wachaga wanavyo penda pesa!!
NA USIONE KILA ALIYESIMAMA NYUMA YA BENDERA YA TANZANI NI MTANZANI yakhe !
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Chama cha wachaga siku kikipata mfadhili kama Rostam unafikiri hawatmkumbatia!na wachaga wanavyo penda pesa!!
Na Chama cha wachaga siku kikipata mfadhili kama Rostam unafikiri hawatmkumbatia!na wachaga wanavyo penda pesa!!
Kuwanunua watanzania haikugharimu pesa nyingi. Njaa ndiyo inayowamaliza watanzania walio wengi. Mimi nimeshuhudia watu wakinunuliwa chai na vitumbua ili wamchague mtu fulani (aah, Manju Msambya) wakati nikiwa mdogo na alifanikiwa kupita. Kwa hizo pesa wanazoiba watatumaliza kwani bado wapo wengi wasiofahamu athari za kuuza utu wao.Kama memba toka jimboni kwake anaweza kuwa na jibu zuri kuhusu huyu mbunge....
Kuwanunua watanzania haikugharimu pesa nyingi. Njaa ndiyo inayowamaliza watanzania walio wengi. Mimi nimeshuhudia watu wakinunuliwa chai na vitumbua ili wamchague mtu fulani (aah, Manju Msambya) wakati nikiwa mdogo na alifanikiwa kupita. Kwa hizo pesa wanazoiba watatumaliza kwani bado wapo wengi wasiofahamu athari za kuuza utu wao.
Rostam ni mwizi kama wezi wengine, na anachogawa si chake bali ni makapi ya mali alizoiba za watanzania.
Mwanakijiji said:Kati ya wabunge ambao inadaiwa wana ushawishi sana kwenye serikali na nje ya serikali ni Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz (CCM) Siyo tu Bungeni lakini pia jina lake limekuwa likitajwa katika mambo mbalimbali na hivyo kumfanya kuwa ni miongoni mwa wabunge wenye "ushawishi" wa aina fulani na wenye nguvu ya aina fulani. Kuna watu wanaomini kuwa yeye ndiyo "King Maker" wa Tanzania. Je ushahidi ukoje. Ufuatao ni wasifu wa Mhe. Aziz ambao licha ya kutojibu maswali, unazua maswali mengi zaidi na kubwa zaidi ambalo binafsi ningependa kusaidiwa majibu yake ni "Mchango mkubwa wa Bw. Rostam kwa taifa letu ni nini"?
Je, ni ajira, kuanzisha vyombo vya habari n.k Je yawezekana kuwa kule Bungeni kwa miaka miwili Bw. Aziz hajawahahi kusema kitu chochote? Na kama amewahi imekuwaje kuwa tovuti ya Bunge haionyeshi mchango wake hata mmoja? Kwanini miaka miwili baadaye hata wasifu wake wameshindwa kuumalizia? Mbunge huyu mwenye utata, kweli anazo nguvu anazodaiwa kuwa nazo au ni uonevu wa wapinzani wake wa kisiasa?. Binafsi sina jibu. wewe unalo?
8. Ikiwa RA tushamweka wazi juu ya UFISADI why tena kuangalia mchango wake? Tunahitaji kumsamehe au kumsafisha???Tell me akija Spika au Mtendaji wa Bunge akaleta michango ya RA...JF tufanyaje??
Mwaka alozaliwa anaogopa kutaja.
Shule alosoma na kupata BA anaogopa kuitaja.
MWaka alohitimu anaogopa kuutaja.
Umaarufu wa ROSTAMU AZIZI ni kugawa Pochi kama hana akili nzuri.
Ni OPEC ya Bongo.
Sisi watanzania tunaamini kwamba watu wote wenye ngozi light kuliko yetu wanafedha.
Kabla ya uchaguzi mwaka 2003 nilisikia kwamba wazazi wa Rostamu wanafaidika na neema ya Mafuta huko Iran kwahiyo wamemfadhiri mtoto wao akisaidie chama chake.
Hadithi hiyo ilinoga na kuonekana ya kweli mpaka kagoda ilipo ibuliwa.
Duniani hakuna cha bure.
Ukiona jirani yako anajipitisha kwako kwa maneno ya huruma na kujifanya anakuonea huruma ujue moja, ana lake jambo.
Nipe nikupe ndo mahusiano ya kawaida.
Fedha itoke Iran kuwasaidia SISIEMU, wao SISIEMU watawapa nini?
Hata sasa usione tunapeleka majeshi Commoro kuzima uasi. hayo ni malipo ya namna fulani.
Unakumbuka Rais wa visiwa vya Commoro alisha funga safari kuja Dar mara kadhaa enzi za Mkapa?
Tukae tusubiri jibu litaibuka lenyewe.
Hakuna shirika wala jumuia yeyote inayogawa Fedha duniani.
Unaarufu wa Rostamu ni kibwagizo kilichoanzishwa na viongozi wa SISIEMU ili kulipa fadhira za kupewa migao ya fedha zilizo ibiwa serikalini na kubandikwa sifa kwamba zimetoka Iran.
Pengine usione Viongozi wengine wanamsifia, pengine washa fanya naye mambo kibao ya aibu na ya kujidharirisha utu wao.
Kuna viongozi wengine wana jinsia moja hadharani lakini mafichoni wanayo jinsia nyingine.
Elewa wakiisema mvuto wana maana gani, hayo mambo hayako Marekani tu.
Wewe umesema.
Kumbe ni kweli mvuto wake ni kugawia pochi viongozi wa SISIEMU?
Wachaga wanajua BOT ndiko kwenye Pochi kuliko kwingine kokote, Mbona kwenye ile LIST OF SHAME kuna mchagga mmoja tu?
Wakati huo huo, Mchungaji Mtikila ametaka Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, akamatwe mara moja kwa kuwa anaishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria.
(Tanzania Daima)
Mchungaji Mtikila alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini, na kusena kuwa Rostam ni kama hana uraia na Tanzania.
Alisema Rostam ni raia wa Iran na aliinngia nchini miaka ya hivi karibuni akiwa mfanyabiashara wa ngozi baadaye kuingizwa kwenye siasa na viongozi wa serikali.
Alidai ana ushahidi wa kutosha hadi hospitali aliyozaliwa mbunge huyo na kwamba hadi sasa wazazi wake wanaishi nchini Iran.
Rostam ni rafiki yangu mkuu, lakini siwezi kumtetea kuliko nchi yangu. Hata maandiko matakatifu yanaonya kuwa msimtawaze mgeni kuwa kiongozi wenu ila atoke kati yenu. Ushahidi upo kuwa bado ni raia wa Iran na hajawahi kuomba uraia mwingine popote, alisema Mtikila.
Ameapa kwamba kama Rostam hatakamatwa atashirikiana na wananchi kumkamata na kumfikisha mahakamani pamoja na wale waliomfanyia mpango akapata nafasi ya kuwa mbunge.
Mtikila alisema kuwa katiba ya Tanzania inatamka kuwa mgeni yeyote ambaye wazazi wake si raia wa Tanzania, hata kama amezaliwa nchini, akitaka kuwa raia sharti kwanza akane uraia wa wazazi wake, kisha aombe uraia wa Tanzania kwa kutangaza kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi, ili kama wananchi wana pingamizi waweke.
Alisema Rostam alipoingia nchini akiwa mfanyabiashara wa ngozi, akakutana na baadhi ya viongozi walioingia nao urafiki kwa ahadi kuwa atawasaidia kwenye uchaguzi mkuu, kisha akanunua kiwanda kimoja cha ngozi mkoani Morogoro kwa msaada wa nchi ya Iran.
Mtikila alisema wakati Rostam akiwa nchini, aliyekuwa mbunge wa Igunga wakati huo, Charles Kabeho, alifariki ndipo viongozi waliokuwa wakimbeba wakampatia jimbo hilo, ambalo amedai kuwa anaamini lipo wazi hadi uchaguzi utakapoitishwa na kumpata mbunge mzawa.
Iwapo hatakamatwa kwa kudanganya uraia, wananchi tutamkamata, kwani ushahidi upo hata hospitali aliyozaliwa jina tunalo, alisisitiza.
Aidha, Mchungaji Mtikila alisema wana-CCM wanakwenda kufanya mkutano Butiama ili kuungama madhambi waliyotenda kutokana na kutofuata maagizo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Alihoji uhalali wa mkuatano wa CCM unataotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kufanyikia Butiama, wakati walimdhihaki Mwalimu Nyerere kwa kuuza nchi.
Aliwashauri viongozi wa chama hicho wanaotarajiwa kwenda katika mkutano huo utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu, kujiuzulu nyadhifa zao na kutubu makosa kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere.
Wanapelekana alikozikwa Mwalimu Nyerere waliyemuumiza moyo akafa kabla ya siku zake, kwa kupora nchi na kuiuza...ni vema kama wote wanakwenda kuungama na kujiuzulu, lakini kama wanakwenda kuusanifu mzimu wa Mwalimu Nyerere, utawamaliza.
My Take:
Je hili laweza kuelezea kwanini Bunge wanashindwa kusema Rostam alisoma shule gani ya msingi na sekondari, au hata chuo kikuu? Maana hawawezi kusema alisoma shule ya Msingi ya Igunga mwaka fulani wakati waliosoma wapo watamuumbua? Rostam alizaliwa wapi, na wazazi wake wako wapi?