Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts


Huyu Rostam ni mkandarasi wa kuaminika. Amekuwa na kazi nyingi sana za kujenga mabarabara, majumba na minara ya simu.
Ndugu zangu wana JF, tatizo letu ni kwamba tulio wengi hapa tuko nje ya Tanzania kwa miaka mingi sana hivyo hatuelewi nini kinaendelea katika Tanzania zaidi ya kupata habari kwa njia ya simu ama mtandao. Lakini ule ukweli wenyewe ni kwamba Tanzania kwa sasa vitu vinakwenda kwa kasi mno na hayo mabiashara makubwa ya kuweza kupata mamilion ya madola yapo, na malipo mengi kwa sasa ni kwa dola ama kwa rate ya dola.

Kuhusu suala la Richmond yeye Rostam alisha sema toka awali kwamba hakuhusika na mpaka sasa bado anasema hakuhusika. Kama ushahidi upo wa yeye kuhusika katika hilo suala kwanini tusimpeleke mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe badala ya kupiga kelele?. Nina amini kabisa wana JF ni watanzania halisi ambao wanaweza kutumia haki yao kimsingi na kikatiba katika kumpeleka Rostam mahakamani pamoja na mafisadi wengine. Lakini kelele za kila siku hapa katika bodi bila matendo husika ni sawa na kutayarisha shamba vizuri lakini hupandi mbegu.

Mtambo Juma Mtambo (Jitu la mahasira)
 

Kama bank kuu yetu sehemu ambapo pesa zinachapishwa wana Net working ya dolla 600,000 na sio Million. Huyo rostam azizi peke yake anaweza kuwa na biashara inayotengeneza dolla Million 400 kwa mwaka? Does that story make sense in your ears?

Kampuni yenye Net profit margin ya Million $400 kwa mwaka si kampuni ya kuchezea, labda unazungumzia kampuni ambayo mauzo yake ni karibu na billion, believe me hata Vodacom hawana hiyo profit margin ya aina hiyo. That is alot of profit. Rostam ana capital ya shilling ngapi ambayo inaweza kuproduce that amount of return? Jee asset zake zinaworth Billion dollar?

Hizi story za kijiweni jamani msizilete Jambo, maana hapa watu wanadeep in kabla ya kuamua. There is no realistic on that story.Unajua haya mambo ya biashara inategemea unampa adisi hizo nani. kama unampa muandishi wa TSJ then unaweza kumshika, lakini kama unampa muandishi anaye fanya homework yake, then huwezi kumsumbua hata dakika.
 
Kuna kodi za aina nyingi Tanzania:

Corporate taz 30%,VAT 20%Custom na excice duties etc etc may be kwa ujumla wake huyo Rosyam makampuni yake hulipa kodi zote hufikia hizo!
Au huenda amekurupuka tu na figure hizo!
 
Mtanganyika,
Hands down umemaliza! I couldn't agree with you more! Hapo alikurupuka, sasa je yuko tayari kuthibitisha mapato yake au...?
 
Kuhusu waandishi wetu kutokuuliza maswali ya msingi, nadhani wakati mwingine huenda tunawaonea tu, si ajabu wao wanauliza maswali yanayotakiwa lakini habari kabla ya kuchapishwa mhariri anayaengua yale anayoona ni "mazito" na ambayo yanamharibia "mlo" wake, matokeo yake tunaishia kuwalaumu waandishi au kuwaona vilaza, wakati si ajabu tatizo haliko upande wao.
 

Mi ningemuuliza tu kuwa hizi siasa za Tanzania kuanza kutumika "vibaya" yeye kaanza kuziona au kagundua lini?Je mwaka 2005 wakati yeye akiwaongoza kina Kikwete na fisadi Lowassa kuwamaliza kina Salim,Sumaye,etc,siasa hapo zilitumikaje?As to his claims of paying taxes,that's simply paranoid,naona jamaa anaelekea mwisho sasa...kwani definitely that which has the beginning must have an end,as to what kind of an end only your destiny will determine.Rostam kaa na tulia tu mwisho wako ndo ushafika hivyo.
 

Mtambo i bet you are better than that!! Hivi unajua katika kampuni zote TZ Kampuni Ya Sigara Tz ndio inaongoza kwa kulipa KODI hadi 2007? Huyo Rostam hela zake hizo zinaenda wapi???

Hakuna anaepiga kelele hapa kama wewe unapiga kelele endelea kupiga kelele!
 

Lol..so how much of the 100billion is yours??..wewe sio mzalendo kabisaaa..eti mahakamani..kama serikali yako unayo itetea imeshindwa kupeleka wezi wa EPA mahakamani ndo sisi tuweze??Sisi tutakaa hapa na kusema ambayo wewe unaogopa kusema!! Ndugu zako wanasota kijijini kwenu (elimu duni,hakuna kazi, hakuna maendeleo), umeme sasa hivi utakatika hapo kwako!! (kataaa kama unaweza??) and here you are defending people like Rostam....pole sana..
 

Huyu fisadi alipotumia siasa kujitajirisha yeye na mafisadi wenzie hakuona kama siasa zinatumika vibaya. Wameamua kumuanika kwa ufisadi wake, sasa analalama!
 
Mhe. RA unategemea tukuamini? If not Richmond, then EPA?
 
ROSTAM WEWE NDIO UATUMIA SIASA HIZO VIBAYA, unazitumia kutuibia, una-abuse siasa za Tanzania. Umetumia ujanja mzuri kuwalaumu wengine!
 

Ibambasi hili ni swali gumu sana!

Kampeni ya kuchafua watu iliongozwa na Membe na Lowasa, kisha Rostam akatumia vyombo vyake vya habari - magazeti ya Mtanzania, Rai na mengineyo kuwachafua wana ccm kuanzia Malecela, Sumaye na kikubwa zaidi kumchafua Dr Salim ambaye alionekana kuwa ni tishio kwenye uteuzi wa Kikwete!

The guy amevuruga watu wengi sana kisiasa ndani na nje ya ccm. Huu mchezo ameucheza sana na kisha kutumia nafasi yake ccm kuiba mabilioni ya pesa za watanzania (kumbuka Kagoda imeachwa kabisa na Kikwete).

Leo anaanza kulia baada ya kuona kuwa JF haongwi mtu na kuna watu kwenye magazeti kama Thisday wamekataa kabisa kununuliwa na pesa zake za wizi.

Rostam Azizi tulia tuli kabisa.... kesi yako ya wizi ikiisha jua kuwa tunapanga kuchunguza uraia wako... maana report zote zaonesha jamaa hakuzaliwa Tanzania na alipata uraia kwa udanganyifu. Hata ukijaribu kufoji hapa jua tu siku yoyote Pal wako Kikwete akitoka madarakani mimi nitakuandamana hadi nikuone ukiwa Keko kwa wizi na kujipatia uraia wa Tanzania kwa udanganyifu!
 
Habari zinazoifikia intelligence unit hapa zinasema kuwa uraia wa Rostam Azizi una utata na kuna uwezekano amefoji kupata uraia wa Tanzania. Intelligence report zinaonyesha kuwa hakuna report za kuthibitisha na kuonyesha Rostam Azizi alizaliwa wapi na lini hapo Tanzania kama wengi wanavyodai.

Intelligence report zinaonyesha pia kuwa kuna utata wa namna Rostam Azizi alivyojipatia passport na uraia wa Tanzania. Habari zingine zinaonyesha kuwa documents alizotumia ni za kufoji na kuwa kuna utata sana hata kwenye tarehe inayotumika kwenye file lake kuwa ni yake ya kuzaliwa.

Hii habari bado ni moto na Mwafrika wa kike anatoa wito kwa serikali ya Kikwete - hasa waziri wa mambo ya ndani - kufuatilia suala la uraia wa Rostam Azizi. Huu ni mwanzo wa habari za uchunguzi ambazo zitatolewa kwenye magazeti huru ya Tanzania in the next two weeks.

Wale watetezi wa Rostam Hapa jamvini kina Zephania Anjela kwa sasa mnaweza kuthibitisha uraia wa Rostam Azizi wakati uchunguzi rasmi ukisubiriwa.
 


Hii habari bado ni moto na Mwafrika wa kike anatoa wito kwa serikali ya Kikwete - hasa waziri wa mambo ya ndani - kufuatilia suala la uraia wa Rostam Azizi. .

Una maana MASHA amchunguze ROSTAM? yangu macho ingawa nakuhakikishia huko ulipo kuwa hilo ni moja ya maswala nyeti yanayoenda kuibuka BUTIAMA labda "busara" za JK zichukue mkondo wake.........

Tanzanianjema
 
Una maana MASHA amchunguze ROSTAM? yangu macho ingawa nakuhakikishia huko ulipo kuwa hilo ni moja ya maswala nyeti yanayoenda kuibuka BUTIAMA labda "busara" za JK zichukue mkondo wake.........

Tanzanianjema

Tanzania njema,

Hii habari hata inatokea huko huko Butiama na nina imani kuwa Kikwete atatumia "busara zake" kufanya the right thing hapa!
 

You said it my sister,
nadhani jamaa anaanza kupre-empty destiny yake na matokeo ya mkutano wa Butiama,kwamba likimfika la kumpata aanze kulalama kuwa siasa zinatumika kumbagua/kumchafua.Huyu bwana ni mwizi asiye na aibu na sijui tu ni kwa nini kikwete anamuacha mtu machafu sana kama huyu anayeigawa nchi kwa ulafi wake wa fedha chafu.Au ndo ule msemo "Show me your friends and I will tell you who you are",is Rostam a replica of Kikwete's inner being?

Mpuuzi sana huyu mwizi wa kiirani!!
 
Asili Yake Ni Iran - - Ana Ndugu Zake Wa Karibu Pale Mtaa Wa Jamhuri Akina Razi And So On Ndio Maana Hata Kampuni Yake Inaitwa Caspian ( Angalia Mitambo Ya Umeme Pale Ubungo Imejengwa Na Caspian )kuna Uhusiani Na Caspian Sea Ama ???

Mwafrika Wa Kike Nafikiri Unataka Kutupotosha Mambo Mengi Kuhusu Rostam Aziz Na Watu Wengine Ambao Umeendelea Kuwataja Sasa Hivi

Mbona Maswali Kuhusu Rostam Aziz Unauliza Sasa Hivi Usingeuliza Na Kuchunguza Toka Mwanzo Kwa Sababu Yeye Ni Asili Ya Persia Mweupe ? Huu Ni Ubaguzi Wa Rangi Kwa Hakika Na Kwa Kweli Kwa Mwanaharakani Kama Wewe Na Kwa Heshima Uliyonayo Sidhani Kama Inaleta Maana Yoyote Ile Kuanza Kuuliza Vitu Hivyo -- Niseme Ukweli Inatia Mashaka Uwezo Wako Wa Mambo Mengine Zaidi .

Kama Unauliza Uraia Wa Rostam Aziz Kwa Sababu Tu Ana Asili Ya Persia Basi Kuna Kabila La Wairaq Kule Arusha Wana Asili Ya Persia Na Sehemu Zengine Za Usomali

Kuna Wachaga Moshi Pale Wana Asili Ya Kenya Kwa Baadhi Ya Mambo Yao Hawa Nao Sasa Tutawauliza Asili Zao Wakija Katika Kugombea Uongozi Au Kitu Chochote Kile .

Tunapokosa Hoja Tusilete Vihoja Ni Aibu Na Fedheha Kwa Jambo Forum Na Wanachama Wake Wote , Mods Tunaomba Mada Na Hoja Zozote Zenye Hisia Za Kibaguzi Kama Hizi Au Zinazochochea Ubaguzi Zifutwe Au Zikaguliwe Kabla Ya Kuingizwa Jukwaani

Hii Itasaidia Kuweka Jukwaa Huru Na La Kizalendo Zaidi Hatutaki Kuonekana Jamboforum Ni La Kabisa Au Dhehebu Fulani Au Kikundi Fulani Cha Watu Ahsante
 
Sakata la Richmond: Rostam mambo magumu

2008-03-17 19:09:42


Mambo ndiyo yanayosemwa hayo. Mwafrika wa kike upo? Je uraia wa mwanahabari wa Ikulu Salva rweyemamu nao ni tata, Je JK amezungukwa na wa kuja? Au anawakumbatia zaidi wageni?

NIMEKUTANA NA BWANA MTIKILA JIONI HII PALE HAIDERLY PLAZA KATIKA MGAHAWA WA KAHAWA KUONGEA NAE MACHACHE KUHUSU KAULI ZAKE HIZI KWA HAKIKA ANAONEKANA ANATUMIWA NA BAADHI YA WATU KUZUSHA MAMBO

NI VIZURI BWANA MTIKILA ATOE UDHIBITISHO WA HIVYO VYETI VYA URAIA WA ROSTAM AU AINA NYINGINE YOYOTE YA UDHIBITISHO KWAMBA KWELI YEYE SIO RAIA

WATANZANIA TUMECHOKA NA KAULI TATA AMBAZO HAZINA UKWELI NA ZINAZOKUJA WAKATI WATU WAKO BUSY KUJIPANGA NA MAMBO MENGINE TUNATAKA WANASIASA AMBAO NI WAZALENDO NA WASEMA UKWELI .

MTIKILA TUNAOMBA UTULETEE UDHIBITISHO WA KARATASI ZA URAIA WA ROSTAM AZIZ NAAMINI UTAKUWA NAZO AU UNAJUA ZILIPO
 

Shy,

Swali rahisi tu kwako,

je unajua kwa hakika Rostam Azizi alizaliwa wapi hapo Tanzania?
Unaweza kutaja jina la hospitali au kwa kungwi ambako Rostam Azizi alizaliwa? Je unaweza kwa hakika kutaja tarehe yake ya kuzaliwa?

Haya ni maswali muhimu sana na hayana ubaguzi hata kidogo. Hili ni swali ambalo mtu yeyote anaweza kuulizwa hapo Tanzania anytime
 

nina hofu kwamba atasema alisikia toka kwa mtu fulani !Na hapo ndipo cred. yake itakapokuwa kwenye free fall. lakini hili suala la kusema kila mtu achunguzwe asilia yake, nadhani raia kamili "tutabaki" wachache !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…