Kada huyu jamaa kakurupuka kujibu. Hili ndio tatizo la wana siasa wenye zero exposure ya legal system. This can backfire and become a nightmare if things will unfolding.
Kama unaweza kusoma tone ya maandishi then unaweza kuona kwamba Rostam anaonyesha hajui ni nini anachoongea. Yeye peke yake anasema analipa $100 Million kwenye tax, jee Tanzania imekusanya how much in tax last year and what percentage does Rostam contributed on total tax margin?
There is no way in earth vikampuni vya rostam vikawa na net profit margin ya $400 million. What is he selling? Ni ngumu kuniconvice kwanya kuna biashara unknown inayoweza kuingiza all that profit annual. Sababu under the corparate tax code 25% in ndio $100M. Sasa you do the math.
Again hakuna hard question kutoka kwa waandishi wa habari, huyu jamaa unamuuliza maswali mazito moja kwa moja. What business are you owning? What is annual growth? How long? Can you prove it? Then the next thing unasikia amekata simu.
You cant fool all of us at the same time. Unausika na Dowans.
Huyu Rostam ni mkandarasi wa kuaminika. Amekuwa na kazi nyingi sana za kujenga mabarabara, majumba na minara ya simu.
Ndugu zangu wana JF, tatizo letu ni kwamba tulio wengi hapa tuko nje ya Tanzania kwa miaka mingi sana hivyo hatuelewi nini kinaendelea katika Tanzania zaidi ya kupata habari kwa njia ya simu ama mtandao. Lakini ule ukweli wenyewe ni kwamba Tanzania kwa sasa vitu vinakwenda kwa kasi mno na hayo mabiashara makubwa ya kuweza kupata mamilion ya madola yapo, na malipo mengi kwa sasa ni kwa dola ama kwa rate ya dola.
Kuhusu suala la Richmond yeye Rostam alisha sema toka awali kwamba hakuhusika na mpaka sasa bado anasema hakuhusika. Kama ushahidi upo wa yeye kuhusika katika hilo suala kwanini tusimpeleke mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe badala ya kupiga kelele?. Nina amini kabisa wana JF ni watanzania halisi ambao wanaweza kutumia haki yao kimsingi na kikatiba katika kumpeleka Rostam mahakamani pamoja na mafisadi wengine. Lakini kelele za kila siku hapa katika bodi bila matendo husika ni sawa na kutayarisha shamba vizuri lakini hupandi mbegu.
Mtambo Juma Mtambo (Jitu la mahasira)