Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Tina nina ombi moja tu. Je huoni kama kuna umuhimu wa kuliweka ili hadharani mapema? Hii inaweza kusaidia kama mali zote hizo hazijahamishiwa SA zingine zikazuiwa na hivyo kubaki Bongo.
 
Tina nakubaliana na wewe kabisa maana huyu RA ameshaaga kabisa aliowalazimisha wamchangue/wampe ubunge zaidi soma HAPA lakini kwa jinsi serikali yetu ilivo bongolala aka wezi, sisi JF tunajua lakini wao wanamchekea tu..... na ataondoka hivi hivi hakuna atakae mgusa
 
Am swallowing bitterly ili nikija kumzaa mtoto aje kuwa na hisia kama zangu.....
uhuni unaimaliza nchi na ninaamini kuwa wahujumu uchumi hawa wanabebwa na principles (zisizo rasmi) fulani serikalini au hata ikulu......

We are dying, we got no education, we strave we....... oh!

anyway nikoradhi kumng'oa mtu kichwa ili mradi akina mama na watoto wasikatishwe maisha yao zidi kwa kukosekana kwa huduma bora....
 
Woooooooooooooooooooooooooute tutawachukulia hatua uchukuzi samahani uchunguzi utakapomalizika ,sasa hivi tumekaribia hatua za mwisho na tutawataja wote waliohusika na hatua tutakazo wachukulia ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani ,bado hajakimbia mtu wapo wanatusubiri tumalize uchunguzi wetu wa uhakika si mmesikia mali zao zote zimekuwa freezed (hili neno tafsiri yake sijaliona kwenye kiswahili).
WaTanzania kaeni mkao wa kula kwani fedha waliochukua pia wameanza kurudisha.
Mambo ya wenzetu hawa yananihuzunisha na kuniumisha kichwa sana lakini tutayatanzua kiukamilifu. Tusubirianeni watu hawa hawataki papala ni lazima kama nilivyosema uchunguzi dhidi yao unaendelea,
 
TINA you are so beatiful, NAKUPENDA maana ni bora kuwa muwazi. Naomba contact zako niwasiliane na wewe
 
Boma kweli unasema haya kwenye mada nzito kama hii ? Ulishindw akutumia akili kidogo uka MP yakaishia huko badala ya kujaza nafasi na ku divert mjadala ?
 
Habari hii kutoka kwenye vyanzo vingine inathibitisha kuwa ni kweli.... ngoja tuifuatilie...
 
Jamani Sheria ya TCRA inasemaje kuhusu hisa za wazalendo? Naaambiwa inakataza wageni kumiliki hisa zaidi ya 65% lakini RA anataka kuzipeleka nje zote. Inadaiwa kwamba wanatoa kisingizio cha UFISADI alioufanya Mkapa kwa kuuza kinyemela hisa za serikali katika Mobitel (sasa TIGO) na hivyo Tigo sasa inamilikiwa kwa asilimia 100 na wageni lakini sheria inakataza. Wanajaribu kutoa tafsiri ya kisheria kupotosha kwamba eti sheria ilikua na maana na kuanzishwa tu then baadaye mzalendo anaweza kuuza popote wakitoa mfano wa TIGO walkati TIGO ni UFISADI wa Mkapa na genge lake. Sasa Chenge (akiwa Miundombinu) aliandika waraka kwa AG Mwanyika akitoa maeleekezo ya kutaka RA aachiwe auze hisa zake. AG inasemekana alikataa kabla ya kubanwa na kulegeza kamba, na baaaye Bodi ya TCRA ikagawanyika kabla ya kupitisha lakini Management hadi sasa ina maoni tofauti kuhusu uamuzi wa bodi, Inasema sawa, bodi ina uamuzi lakini si kukiuka sheria, sasa kazi ipo maana wanaandaa mabadiliko ya Sheria Ndogo (regulation) ambayo zamani ilikua Waziri anaweza kubadili tu kwa kutangaza katika gazeti la serikali (GN) lakini sasa Samuel Sitta, anaelezwa kuwa kizingiti kwa kuunda kamati ya bunge ya Sheria Ndogo ambayo sasa italazmika kupitia kwanza sheria ndogo kabla haijatangazwa katika GN. Ndio maana kulikua na mkakati maalumu wa kumng'oa Sitta ili kuruhusu hiyo regulation tena inabadilishwa kwa sababu ya mtu mmoja tu, RA. Hizo ni HABARI ZA UHAKIKA MNO!!!!!!

Habari zaidi kuhusu ufisadi wa Chenge, RA na EL tutawaleteeni soon,na kwa wale waliosikiliza Bunge leo, wafuatilie Mchango wa Mbunge mmoja mwanamke wa Chadema, anayetoka mkoani Kilimanjar, aliyeuliza fedha za Barabara ya MSata-Bagamoyo na fedha za uwanja wa Ndege wa Mwanza
 
yaani hii nchi sheria inabadilishwa kwa ajili ya mtu mmmoja tu!! kweli ccm kiboko yao sasa nimeamini.
na hao wabunge wa ccm wote wamekaa tu kaa wapuuzi, wanamuacha mtu aondoke na mali ya umma. walichaguliwa ubunge kwa sababu gani? kwenda kujifunza jinsi ya kumuibia mtanzania tu basi au
 
duh Mwanawane sijui atajificha wapi??!!!!!!!.....mie nadhani ile tetesi iliyotokea kwamba kanywa sumu sasa inakaribia kua kweli..ngoja tuone
 
Habari za uhakikia kabisa ni kwamba Rostam Aziz ameanza kuhamishia mali zake nje ya nchi, sababu anahofia mambo yanavyokwenda serikalini kwa sasa. Kwa ushahidi tayari ameweka rehani hisa zake zote 35pc za Vodacom Afrika Kusini. Kabla ya kuhamishia hisa zake, alikua amenunua hisa za Planetel za mwenzake Peter Noni na mkewe, naye alifanya hivyo kuhofia mambo yanavyokwenda ofisini kwake BoT. Rostam alichukua hisa zote 35pc za Watanzania kupitia kampuni zake za Caspian na Mirambo. Nimethibitisha kwa macho yangu mwenyewe nikiwa bongo kwamba Chenge akiwa Waziri wa miundombinu alimsaidia kwa nguvu zake zote Rostam kufanikisha mkakati wake huo wa kuhamisha hisa zake nje kwa kisingizio cha kuweka rehani. Kuna watu serikalini walipinga (na wanaendelea kupinga) lakini jamaa aliwazidi kete kwa kusadiwa na Chenge na sasa inaelekea amefanikiwa kwa kiasi. Zaidi nitawaletea maana naharakisha kurejea majuu. Nitamwachia Invisible mambo yote ili siku mwafaka amwage hadharani

dada tina mbona story yako inachanganya?hapa unatuleza kuwa rostam anahamisha mali zake,halafu unasema kuwa 'eti'Peter Noni na mkewe waliuza hisa zao kwa RA kwa kuofia mambo yanavyokwenda ofisini kwake.
unajua VODACOM ililetwa na nani hapa nchini?unajua kuwa noni aliuza hisa zake mwaka gani?kwa taharifa yako PLANETEL ndio iliyoileta VODA hapa nchini na noni aliuza hisa zake kabla jakaya hajaingia madarakani,hivyo nakushauri nenda kamuulize vizuri huyo aliyekupa hizi story
 
Jamani Sheria ya TCRA inasemaje kuhusu hisa za wazalendo? Naaambiwa inakataza wageni kumiliki hisa zaidi ya 65% lakini RA anataka kuzipeleka nje zote. Inadaiwa kwamba wanatoa kisingizio cha UFISADI alioufanya Mkapa kwa kuuza kinyemela hisa za serikali katika Mobitel (sasa TIGO) na hivyo Tigo sasa inamilikiwa kwa asilimia 100 na wageni lakini sheria inakataza. Wanajaribu kutoa tafsiri ya kisheria kupotosha kwamba eti sheria ilikua na maana na kuanzishwa tu then baadaye mzalendo anaweza kuuza popote wakitoa mfano wa TIGO walkati TIGO ni UFISADI wa Mkapa na genge lake. Sasa Chenge (akiwa Miundombinu) aliandika waraka kwa AG Mwanyika akitoa maeleekezo ya kutaka RA aachiwe auze hisa zake. AG inasemekana alikataa kabla ya kubanwa na kulegeza kamba, na baaaye Bodi ya TCRA ikagawanyika kabla ya kupitisha lakini Management hadi sasa ina maoni tofauti kuhusu uamuzi wa bodi, Inasema sawa, bodi ina uamuzi lakini si kukiuka sheria, sasa kazi ipo maana wanaandaa mabadiliko ya Sheria Ndogo (regulation) ambayo zamani ilikua Waziri anaweza kubadili tu kwa kutangaza katika gazeti la serikali (GN) lakini sasa Samuel Sitta, anaelezwa kuwa kizingiti kwa kuunda kamati ya bunge ya Sheria Ndogo ambayo sasa italazmika kupitia kwanza sheria ndogo kabla haijatangazwa katika GN. Ndio maana kulikua na mkakati maalumu wa kumng'oa Sitta ili kuruhusu hiyo regulation tena inabadilishwa kwa sababu ya mtu mmoja tu, RA. Hizo ni HABARI ZA UHAKIKA MNO!!!!!!

Habari zaidi kuhusu ufisadi wa Chenge, RA na EL tutawaleteeni soon,na kwa wale waliosikiliza Bunge leo, wafuatilie Mchango wa Mbunge mmoja mwanamke wa Chadema, anayetoka mkoani Kilimanjar, aliyeuliza fedha za Barabara ya MSata-Bagamoyo na fedha za uwanja wa Ndege wa Mwanza

Hivi hapa Tanzania hakuna Kamati za Usimamizi katika bunge letu?

Kubadilisha sheria kama mbadala wa kuongeza Ufisadi ni Ufisadi!

Hii, isikubalike kabisa.Mtawanyo wa hela na hisa- hatimaye huyu jamaa akimbie nchi. Na kama yumo kwenye listi za mafisadi, basi sharti watoe kwenye hilo hilo gazeti kuwa anyanganywe hati ya kusafiria mpaka hapo atakapo safisha jina lake!

Kuna umuhimu wa wapinzani kuleta hoja hiyo bungeni -Walio na Wanao- husika katika Ufisadi na Ubadirifu wa mali ya mlipa kodi wa Tanzania na mwenye uwezo wa kukimbilia Ng'ambo wanyang'anywe hati hizo mara moja!

Ikiendela hivi itatishia-mwelekeo wa Viongozi wetu na hatimaye siasa za CCM.

Bunge lisimame kidete...Hongera Bwana Sitta kama hii ni thubutu yako.
 
Habari za uhakikia kabisa ni kwamba Rostam Aziz ameanza kuhamishia mali zake nje ya nchi, sababu anahofia mambo yanavyokwenda serikalini kwa sasa. Kwa ushahidi tayari ameweka rehani hisa zake zote 35pc za Vodacom Afrika Kusini. Kabla ya kuhamishia hisa zake, alikua amenunua hisa za Planetel za mwenzake Peter Noni na mkewe, naye alifanya hivyo kuhofia mambo yanavyokwenda ofisini kwake BoT. Rostam alichukua hisa zote 35pc za Watanzania kupitia kampuni zake za Caspian na Mirambo. Nimethibitisha kwa macho yangu mwenyewe nikiwa bongo kwamba Chenge akiwa Waziri wa miundombinu alimsaidia kwa nguvu zake zote Rostam kufanikisha mkakati wake huo wa kuhamisha hisa zake nje kwa kisingizio cha kuweka rehani. Kuna watu serikalini walipinga (na wanaendelea kupinga) lakini jamaa aliwazidi kete kwa kusadiwa na Chenge na sasa inaelekea amefanikiwa kwa kiasi. Zaidi nitawaletea maana naharakisha kurejea majuu. Nitamwachia Invisible mambo yote ili siku mwafaka amwage hadharani

Sistery mbona hapo umeniacha kwenye mataa umeshuhudia kwa macho yako hayo yakifanyika wapi? kwenye soko la hisa, au wapi?

Mwaka huu kazi ipo....
 
dada tina mbona story yako inachanganya?hapa unatuleza kuwa rostam anahamisha mali zake,halafu unasema kuwa 'eti'Peter Noni na mkewe waliuza hisa zao kwa RA kwa kuofia mambo yanavyokwenda ofisini kwake.
unajua VODACOM ililetwa na nani hapa nchini?unajua kuwa noni aliuza hisa zake mwaka gani?kwa taharifa yako PLANETEL ndio iliyoileta VODA hapa nchini na noni aliuza hisa zake kabla jakaya hajaingia madarakani,hivyo nakushauri nenda kamuulize vizuri huyo aliyekupa hizi story

Nilikuwa naangalia tuu jinsi members walivyo kuwa na haraka kudandia story ya tina..hisa za vodacom sio za watanzania msipotoshwe..serikali ya tanzania haijawahi kumiliki shares in vodacom..tuwe makini na wewe mwanakijiji huna haibu umethibitisha wapi?? tuwe makini na habari zingine..
 
Tina,

Asante kwa taarifa nzuri, lakini ungetupa undani ili tujue na sisi tuanze vipi kulifuatilia jambo hili kwa undani ikibidi hatua za kisheria au tuanze kile kitu waingereza wanasema, "name and shame game"

Tafadhali tusaidie maelezo ya undani mama.
 
Back
Top Bottom