Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,962
- 721
Huyu RA mbona hajatoa risiti zingine? Naamini pesa yake chafu ilitumika katika sana 2005. Atoe risiti zote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mjenga nchi ni mwananchi.Mwanakijiji,
1. Kuhusu Richmond na Dowans, Bunge lenu lilichunguza likasema hakuna sehemu walipoona kwamba Mh. Rostam Aziz anahusika... sasa nini kifanyike tena...
2. Mamlaka za kuchunguza zinachunguza kukiwa na hoja,,, sio kila anachosema mwanakijiji kichunguzwe... wanapoona unaongea utumbo wanakuacha na utumbo wako.
3. Mpaka sasa ni Mambo ya Umbea tu... hakuna kitu Tangible hata kimoja... umaskini wenu tu... kila mkimuona mtu tajiri mnadhani ameiba...
4. Narudia... tunaomba kuona -ushare-holding wa Rostam Aziz, kwenye hizo kampuni mnazozungumzia kama hamna... acheni mambo ya kitoto hapa!
tatizo lako JMushi1 huamini katika mawazo ya kujitegemea; unafikiri kila mtu anayetofautiana na msimamo wa "wengi" atakuwa ametumwa! Mawazo kama ya kwako hayo yanafukuza watu wengi kwenye forum hii kwa kuogopwa kuwa labelled. Jirekibishe!
Tunahitaji Dikteta wakati huu kuliko kipindi chochote katika historia yetu kama taifa.Dada Asha,
Rule of law. Tukitaka kuwa kama usemavyo basi itakuwa ni UDIKTETA!
thanks Kitila! Asante Kasheshe!
Kitila, Nashukuru Kwa Kumvua Nguo Mtikila, Huyu Ni Mtu Mbaya Sana! Na Hivi Majuzi Alipokuja Na Madai Kuwa Ra Ni Raia Wa Iran, Nadhani Alikuwa Anataka Kuvuta Mshiko Mwingine Kutoka Kwa Ra, Na Wala Sio Kumshtaki Na Kusaidia Taifa! Mtikila Hana Tofauti Na Akwilombe, Tambwe Hiza! Wote Hawa Hupiga Domo Si Kwa Masilahi Ya Taifa Bali Tumbo Zao!
Narudia Tena Watanzania Tunapenda Sana Kuongea (na Udaku Ndani Yake) .. Bila Ya Kuwa Na Vitendo! Hivi Watanzania Milioni 40 Hakuna Hata Mmoja Mwenye Ushahidi Wa Kumshtaki Ra? Je Wenye Ushahidi Wako Wapi?
Mtikila Anadai Anamjua Ra Ni Raia Wa Iran, Sasa Anangoja Nini Kumburuza Ra Mahakamani? Humu Jf Mbona Hamkujitokeza Kwenye Kamati Ya Mwakyembe Kuelezea Kuwa Richmond Ni Ra! Ile Kamati Mpaka Imemaliza Kazi Yake, Imeshindwa Kujibu Swali La "richmond Ni Nani". Mwakyembe Alilalamika Sana Kwenye Vyombo Vya Habari Watanzania Mnapenda Sana Kuongea Njooni Kwenye Kamati Kutoa Ushahidi! Hakuna Mtu!!
Ndio Sikatai Ra Anaharufu Ya Ufisadi Lakini Huu Wapi Ushahidi Wa Moja Kwa Moja? Naye Anajigamba Mwenye Ushahidi Amburuze Mahakamani, Lakini Matokeo Yake Watanzania Tunaendelea Kulia Lia "fisadi Wewe" "fisadi Wewe"! Yuko Wapi "hero" Wa Kumburuza Ra Mahakamani, Ili Kizazi Chetu Kimwekee Alama Ya Ndiyo!
Yuko Wapi "hero" Wa Kuwaburuza Mafisadi Mahakamani, Ili Kizazi Chetu Kimwekee Alama Ya Ndiyo!
Wimbo Wa "fisadi Wewe" "fisadi Wewe" Ni Mzuri Lakini For The Long Run Ulemaza Na Kupumbaza Akili!
Hongera ASKOFU MOKIWA.ROSTAM -MALASUSA-MTIKILA
Wenzangu mimi nisingependa kuingilia sana swala la Kama ROSTAM anu umiliki wa DOWANS au RICHMOND, ila ninalotaka tulijadili hapa ni kuhusu kuuli za wachungaji wetu wa type ya akina Malasusa na Mtikila ambao wamekuwa sikuzote mstari a mbelee kuwaandikia kadi za mialiko watu wenye pesa zao kwa aijili ya kuchangisha Pesa Kwa aijili ya makanisa yao!Swali linakuja hivi!Je kabla ya mialiko huwa wanaachukua kigezo gani kumualika mtu kama sio pesa zke tu?arafu hili kanisa La KKKT wao kama kanisa je wana haki ya kumhukumu mtu hata kama amepatikana na kosa?,Je kila kwaya au jumuiya yoyote ya kidini kwenye vigango wakitaka kumualika mtu wamekuwa wakiujulisha uongozi wa juu?na Je Spika Yeye sio Fisadi kwa matumizi ya ofisi yake ya bunge ambayo yameonyesha kwamba amepeleka risiti feki mara kwa mara je Malasusa hilo Halioni.
Ndugu mtikila nilishasema tangu mwanzo kwamba tumuache kwani kila mmoja wetu anamuelewa kuhusu "Up stairs" yake kwamba imejengwa kwa cement feki kama ya Maghorofa ya Ilala
Pride Goes Before Fall And Fools Rush Where Angels Fear To Tread.kitila,
Nilishakutabiria Mambo Makubwa Kwa Muda Mrefu!!! Post Yako Ina Make Sense Sana... Ndio Maana Ni Muhimu Watu Kama Ninyi Kuja Hapa Kuandika Mapema... Ili Kutoacha Kujaziwa Kurasa Za Utumbo Na Ukanjanja.
Simply That Is It!!!
Ahadi Kwako Mkuu; 2010 Nitakuunga Mkono Ukigombea Nafasi Yoyote Mkuu... Na Kwa Chama Chochote Hata Kama Ni Mgombea Binafsi... Tuombe Mungu Ccm Na Serikali Yake Waridhie Ushauri Wa Mahakama Kuu.
Mtikila asituchezee akili na anachofanya anajua,hii ndio sample ya viongozi wengi serikalini..matapeli watupu!
JMushi1: Umekosea tena. Kuwa mwanachama wa chama cha siasa au la haina uhusiano kabisa na uhuru wa kifikra. Unaweza ukawa sio mwanachama wa chama chochote cha siasa na ukawa na utegemezi wa kutisha wa kimawazo and vice versa.
Kuna watu hapa ambao wametangaza kuwa hawana vyama vya siasa lakini ndio wategemezi wa kutisha wa mawazo. Kila waandikapo unaona jinsi wanavyojiegesha kwa mawazo ya mtu fulani, hawawezi kujitegemea. Wakisikia fulani ni fisadi na wao mbiombio kujiunga kwenye kampeni za kulaani. Wakisikia fulani ni hero kwa sababu alimshutumu mtu fulani bungeni hawachelewi kuunga behewe la kumwaga sifa. Huo ndio utegemezi wa mawazo.
Anyway, hatutachoka kukuelimisha maana wengine ndio kazi tuliosomea na inayotuweka mjini!
Nduguzanguni,
Mnajadili nini wakati Bwana Mkubwa kasema mfunge midomo?! Quelle arrogance!
Mwaka 1852 Waarabu waliokuwepo nchini Tanganyika ni wale waliokuja kufanya biashara za kununua watumwa na kwenda kuwauza kwa Waarabu wengine huko kwao. Mheshimiwa Rostam asitake watu wakaanza kumkashifu bure kwa statement zake ambazo zinadhihirisha dharau kubwa aliyonayo kwa Watanzania wenziwe. Utawaambiaje watu wanaojadili jambo muhimu wafunge midomo yao eti kwa vile tu hawana ushahidi wa kupeleka jambo hilo Mahakamani? Kama aliamua kuingia kwenye siasa na kuanza kusuguana mabega na viongozi basi asichukie kujadiliwa. Anajadiliwa Mkapa aliyekuwa mkuu wa nchi, itakuwa yeye mfanyabiashara?
Jamani Mtikila pamoja na shortcomings zake ana nia njema na Taifa la Tanzania kama si Tanganyika! Kama nimeelewa nilichosoma maana ni magazeti mengi yametoa nukuu tofauti tofauti za hotuba ya Rostam, kuna mahali wanasema Rostam alimpa Mtikila masaada kama anavyofanya kwenye makanisa mengine na akaweka signature kwamba amepokea hizo pesa. Kama ilikuwa ni msaada signature ni ya nini? Ukimsaidia mtu humuombi aweke sahihi kwamba umemsaidia. Kwa hiyo, kama Mtikila aliweka sahihi basi anachosema ni kweli kwamba alikopeshwa fedha hizo na hakusaidia kama walivyosaidiwa wana Kwaya wa KKKT na wengine ambao sasa hivi wanaadhiriwa kwa kutajwa kwamba walikuwa 'ombaomba'!

Bibi Ntilie, hapa umesema kitu muhimu sana. Msaada usio na masharti hautiliwi saini. Swali moja ambalo hamtalisoma kwenye magazeti (unaweza kumsikiliza mwenyewe Rostam) ni kuhusu misaada yake kwa watu wengine, ambapo aliulizwa na mmoja wa waandishi kama anaorodha/majina ya watu wengine aliowapa misaada? Jibu lake lilikuwa ni kuwa watu hao wasiwe na wasiwasi, kwani alitoa misaada tu na hana sababu ya kuwataja.
JE CHADEMA ILIKUMBWA NA KASHFA AMA IMEGUSWA NA KASHFA YA EPA?
Naomba jibu tafadhali...
Maana sasa tunajuwa hata ile pointi yetu ya wabunge kutangaza maslahi yao IME PREVAIL...JE NA WEWE UKO RADHI KUTANGAZA YAKO?