Ndio nasema hilo haliwezekani Ni kazi ya serikali kutengeneza mazingira mwafaka kwa sekta binafsi na wafanyabiashara kufanya biashara zao na wakati huohuo kuhakikisha kwamba inaziba mianya yoyote, kwa njia ya sheria, kanuni, n.k., ya kuliingiza hasara taifa na kupoteza mapato halali kwa njia ya kodi. Inavyoonekana ni kama vile tulitaka Rostam asitumie mianya iliyokuwepo na ambayo ipo ya kumfanya apate faida haraka na kubwa, I bet hili haliwezekani kwa mfanyabiashara yeyote, simply because hiyo sio kazi yake!
CCM walipoamua kuwakumbatia wafanyabiashara waliamua pia kukumbatia utapeli na ujanjaujanja wa wafanyabiashara kama akina Rostam. Rostam anasema wazazi wake walianza biashara tangu 1852, sasa cha kujiuliza ni kwa nini yeye amejulikana kuanzia kipindi cha wakati wa Mwinyi na kushamirisha biashara zake kipindi cha kampeni za urais wa 2005? Ni kwamba huko nyuma hapakuwa na loop holes za kijinga kama zilivyo sasa.
Tuache kuwa simplistic because simplicity is the enemy of truth. Hatuwezi kuishinda vita ya ufisadi kwa kuwashambulia mawakala wa ufisadi; ifike mahala tuamue ama kuwashambulia wazalisha ufisadi CCM au kama, hatuwawezi, tukae kimya na tukubaliane kwamba hayo ndiyo maisha yetu!