Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Ndio maana tunasema, yahitaji sana maandalizi kumtuhumu mtu kwani yawezekana ukajikuta we mwenyewe una dosari kibao sasa angalia mzee mzima Mtikila kaumbuka hasa kwa kukiri kuwa RA ni rafiki wa siku nyingi kiasi hata cha kwenda kopa pesa!
 
tuvute muda tu hii ngoma ya ufisadi ikiendelea kupigwa tutagundua na wajomba zetu kumbe wamo, tusubiri ripoti ya bagamoyo safari ni ndefu tukaze buti..
 
Hivi MLIMUWEKA kundi gani huyu "Mchungaji"? Inaelekea wengi mnashangazwa na yeye "kukopa" kwa RA. Mimi nilishangazwa naye tangu alipoanza kumshambulia Mwalimu kwa HOJA na MANENO ya ajabuajabu na aliendelea kumshambulia hata baada ya kuwa amefariki. Mmewahi kusikia DP anayoiongoza tangu imesajiliwa ina VIKAO?
 
Mtikila Mbabaishaji Tu...wapambanaji Wa Kweli Tutawajua As Day Goes On.....pesa Mbaya Itawatokea Puani Tu
 
Mtikila Anatumia Siasa Za Kuwabomoa The So Called Magabachori ON PUBLIC,Ili Apate Kuishi on the backend(anakwenda kulamba)....the Serious Upinzani Should Not Involve Him In Any Serious Discussions.
 
....Mmewahi kusikia DP anayoiongoza tangu imesajiliwa ina VIKAO?
Deconstructing Mtikila!
....pesa Mbaya Itawatokea Puani Tu
Pesa mwanaharamu!

Mtikila Anatumia Siasa Za Kuwabomoa The So Called Magabachori ON PUBLIC,Ili Apate Kuishi on the backend(anakwenda kulamba)....the Serious Upinzani Should Not Involve Him In Any Serious Discussions.
Hahaha, siri inaanza kufichuka sasa. Yani wanampoza sio? Basi upinzani una safari ndefu katika kuangalia watu wa kushirikiana nao.
 
Mtikila sasa anachoka kisiasa anasema anaenda kufungua kesi dhidi ya RA amegushi sahihi yake ile.Sasa wakati anapokea kinote toka kwa RA hakuakiki?au hakusaini yeye?
Sasa fedha alisaini vp na alipokeaje?
 
invisible tunakazi..si ndogo...hata baadhi ya wapiga domo Bungeni wanapiga ili kupandisha price zao kwa mafisadi...the more anapopiga domo price yake kwa mafisadi inakuwa kubwa...ikiwa mtu anachukua 3M maana price yake ipo chini...
 
Deconstructing Mtikila!
Pesa mwanaharamu!

Hahaha, siri inaanza kufichuka sasa. Yani wanampoza sio? Basi upinzani una safari ndefu katika kuangalia watu wa kushirikiana nao.

Sasa watu wataanza kutia akili kwanini Mbowe, Dr Slaa na Mnyika wamewahi kumpinga Mtikila kwa namna mbalimbali. Sasa mtaelewa kwanini DP kazi yake ni kuishambulia CHADEMA mara kwa mara. Sasa mtaelewa kwanini Mtikila aliweka pingamizi kwa CHADEMA isigombee urais na kwanini baada ya uchaguzi DP ikafungua kesi ya kutaka CHADEMA inyang'anywe wabunge wote na isipewe ruzuku

Mtikila ni toilet paper.....hao wanaomtumia sasa nao waangalie, atawaacha njia panda na kurudi kwa Rostam. Kwake yeye suala ni dau kubwa tu!

Rostam ashinikizwe ataje ni watu gani hao anaosema wanamhujumu? Na aseme ni wakina nani anawakopesha fedha ikiwemo orodha ya wale wabunge wa CCM alioko kwenye payroll yake!



Asha
 
" Uzuri" wa hawa wenzetu wenye kujua kuweka " social capital" through kick backs..wanaweka kumbukumbu ya nani kachukua nini, lini na wapi ..for future reference.Mchungaji si ajabu alishasahau kuwa alionja na yeye matunda ya ufisadi wa RA.
Wengine waanze kutia kichwa maji kwani wembe wa kinyozi unaendelea kufanya kazi.
The singing has just begun
 
...ikiwa mtu anachukua 3M maana price yake ipo chini...
Mkuu, najaribu kufikiria MILIONI 3 ikuumbue hivi? Hivi watu wanashangaza sana. Hizi njaa mbaya sana. Three million...! Incredible I may say. Ingekuwa Three million USD naweza kusema inashawishi, mkopo wa milioni 3...! Wonderful
 
mwanakijiji,

1. Kuhusu Richmond Na Dowans, Bunge Lenu Lilichunguza Likasema Hakuna Sehemu Walipoona Kwamba Mh. Rostam Aziz Anahusika... Sasa Nini Kifanyike Tena...

2. Mamlaka Za Kuchunguza Zinachunguza Kukiwa Na Hoja,,, Sio Kila Anachosema Mwanakijiji Kichunguzwe... Wanapoona Unaongea Utumbo Wanakuacha Na Utumbo Wako.

3. Mpaka Sasa Ni Mambo Ya Umbea Tu... Hakuna Kitu Tangible Hata Kimoja... Umaskini Wenu Tu... Kila Mkimuona Mtu Tajiri Mnadhani Ameiba...

4. Narudia... Tunaomba Kuona -ushare-holding Wa Rostam Aziz, Kwenye Hizo Kampuni Mnazozungumzia Kama Hamna... Acheni Mambo Ya Kitoto Hapa!

Absolutely Rubbish
 
Mkuu, najaribu kufikiria MILIONI 3 ikuumbue hivi? Hivi watu wanashangaza sana. Hizi njaa mbaya sana. Three million...! Incredible I may say. Ingekuwa Three million USD naweza kusema inashawishi, mkopo wa milioni 3...! Wonderful

hahahaha,
Mkuu kuna watu wanapokea dau chini ya hapo.Ni njaa tu zinawasumbua akiamua kuwataja mbona wengi wataumbuka tena sana tu.
 
Rostam azua mapya

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti

KAULI alizotoa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM) wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam juzi, zimepokewa kwa maoni na mtazamo tofauti na watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wanasiasa na wasomi waliozungumza na Tanzania Daima.

Wakizungumza katika mahojiano ya ana kwa ana na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wasomi na wanasiasa walizielezea kauli hizo za Rostam kuwa zinazofungua ukurasa mpya katika mwenendo wa mahusiano ya kisiasa na kijamii nchini.

Mmoja wa wanasiasa maarufu ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) na mshauri wa karibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Jussa Ismail Ladhu, alieleza kuguswa na kauli zilizotolewa na mbunge huyo ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiandamwa na jinamizi la ufisadi.

Akifafanua, Jussa alisema hoja ya Rostam kuhusu kuanza kuwapo kwa ubaguzi katika masuala ya siasa kwa upande wa Tanzania Bara, ni jambo la hatari kwa umoja na mshikamano wa kitaifa kwani ndilo limekuwa likivitafuna visiwa viwili vya Pemba na Unguja kwa miaka mingi, na tayari athari za jambo hilo zimekuwa zina madhara makubwa.

‘‘Ninaungana naye kusikitika kwamba, tatizo la ubaguzi wa rangi ambalo limekuwa linatukwamisha sana huku Zanzibar, sasa limeanza kuingia Tanzania Bara. Hii ni hatari,” alisema Jussa.

Alisema kauli hiyo ya Rostam inapaswa kufanyiwa kazi kwa haraka na kwamba, iwapo itathibitika kuwa alichokisema si jambo la kweli, basi atalazimika kuwajibika kwa kulieleza taifa uongo.

Jussa alieleza kwamba, tamko la juzi la Rostam limekumbusha masikitiko ya watu wengi, ambao waliguswa na uamuzi wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta wa kumzuia kutoa utetezi wake kuhusu uhusiano wake na Richmond na Dowans, tena baada ya Bunge lenyewe kumtaka afanye hivyo awali.

‘‘Inasikitisha kwamba leo Rostam anatoa maelezo hayo miezi kadhaa baada ya Spika kumzuia kutoa utetezi wake bungeni, kuhusu Richmond na Dowans, hata kusababisha hivi sasa Watanzania kubakia kizani kwa sababu tu ya kukosekana kwa fursa hiyo ambayo ilitokana na agizo la Bunge hilo hilo,” alisema Jussa.

Mbali ya hilo, Jussa alieleza kusikitishwa na kile alichokielezea kuwa ni unafiki wa wanasiasa, kama ule unaoonyeshwa na Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye wanaita baadhi ya watu mashetani na wao wenyewe wakawa wa kwanza kwenda kwao kuomba.

‘‘Lililotia aibu katika mazungumzo yale ya Rostam, ni hili la kuwa na wanasiasa wanafiki kama Mtikila. Watu wa namna hii wamekuwa wanaitukanisha siasa na wanasiasa. Huyu mtu anamwita mwingine ibilisi, halafu fedha ya huyo huyo anayemwita shetani unaichukua. Kama mtu ni shetani, basi hata fedha yake pia ni ya shetani. Kama haikuwa safi kwa kuomba, pia haitakuwa safi kwa mkopo,” alisema akionyesha kukerwa na kitendo cha Mtikila kuchukua fedha kutoka kwa Rostam.

Mbali ya hilo, alisema kikubwa katika kauli aliyoitoa Rostam juzi, ni ule wito wake wa tahadhari kwamba taifa linaelekea kubaya, hasa kutokana na kuanza kuibuka kwa watu wanaozushia wengine uongo.

Alisema alikuwa akikubaliana na Rostam kwa asilimia 100 kwamba, juhudi kubwa inayofanyika hivi sasa kwa watu kuzungumzia watu, kama ingeelekezwa katika masuala mengine yenye tija, basi taifa lingepiga hatua kubwa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliuelezea mjadala unaozingira suala hili zima kuwa usio na msingi, na ambao unapaswa kukomeshwa.

Hata hivyo, Zitto alisema Rostam alipaswa kutambua kuwa, mbegu za ubaguzi ambazo zinajionyesha leo hii katika taifa, chimbuko lake ni kundi la mtandao ndani ya CCM, ambalo mbunge huyo wa Igunga alikuwa mmoja wao.

Alisema harakati za kibaguzi zilizoendeshwa na kundi hilo la mtandao dhidi ya mwanasiasa na mwanadiplomasia Dk. Salim Ahmed Salim, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala, ndiyo msingi wa vitendo vya kibaguzi leo hii.

‘‘Baadhi yetu tulipata kuonya mapema kuhusu utamaduni wa kibaguzi, uliokuwa ukiratibiwa na kundi la mtandao, ambalo Rostam ni mmoja wao, wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005. Tuliwaeleza mapema kabisa kwamba ipo siku mambo haya yatawarudia,” alisema Zitto mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika nchini.

Hata hivyo, Zitto alisema alikuwa akiamini kwa dhati kuwa, kama Mtanzania, Rostam Aziz alikuwa na haki ya kualikwa na kwenda katika hafla ya Kanisa la Kiinjili ya Kilutheri.

Alisema angepata nafasi ya kumshauri Rostam kabla ya kwenda pale, angemtaka aende akashiriki katika shughuli ile na kutoa mchango wake na kuondoka pasipo kusema neno.

‘‘Kilichowastua watu wengi ni yale maneno aliyoyasema alipokuwa kanisani, na si kwenda kwake pale kwani mimi naamini kama Mtanzania alikuwa na haki ya kuitikia wito na hata ikibidi kuchangia,” alisema Zitto.

Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Rostam kuwa kuna kundi la watu maarufu na wazito ambao wana ajenda ya kuchafua baadhi ya watu, Zitto alikuwa na haya ya kusema: ‘‘Mbona unaniuliza kitu ambacho hata wewe unakijua? Ni jambo la kweli kwamba kuna makundi, na wewe unalijua hilo. Ninachosema mimi mjadala mzima huu hauongezi tija yoyote.”

Kuhusu mjadala wa ufisadi kuteka ajenda zote nyingine muhimu, Zitto mbali ya kusema hoja hiyo ina ukweli, alisema suala hili linalojadiliwa ni muhimu sana na linapaswa kujadiliwa hadi hapo hatua zinazostahili zitakapochukuliwa.

Alisema kushindwa kwa serikali kuchukua hatua za mara moja juu ya mambo yanayohusu ufisadi, ndiyo chanzo kikuu cha kuendelea kushamiri kwa hoja hizi za ufisadi kila kukicha.

‘‘Ni kweli mjadala wa ufisadi umechukua muda mrefu sana. Hata hivyo, ni jambo ambalo hatuna budi kuendelea kulipigia kelele hadi hapo serikali itakapochukua hatua. Kushindwa kuchukua hatua za mara moja kwa serikali, ndiyo chanzo kikuu cha kuendelea kwa kelele na meneno mengi,” alisema Zitto.

Alieleza kushangazwa kwake na kushindwa kwa serikali kuchukua hatua zinazopaswa hata katika suala kama la Richmond, ambalo Kamati Teule ya Bunge ilishatoa ripoti yake Februari mwaka huu.

Alisema ni jambo jema kwamba katika historia ya Tanzania, tatizo la ufisadi ambalo lipo, halijapata kuzungumzwa kwa uwazi na kwa mapana kama ilivyo sasa, hatua aliyosema tulipaswa kuipitia.

Hata hivyo, alisema kushindwa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kuhusu ufisadi, ni moja ya mambo ambayo yamesababisha watu kama aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daud Ballali afariki dunia kabla hajaeleza kile alichokuwa akikijua kwa upande wake, juu ya wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

‘‘Suluhisho ni kwa masuala haya kushughulikiwa mara moja, na matokeo ya kuchelewa huku ndiyo yaliyosababisha mtu kama Ballali afariki dunia kabla hajapata haki ya kujitetea au kueleza upande wake. Utamaduni wetu wa kukalia mambo umetufikisha hapa tulipo leo,” alisema Zitto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia, alisema sasa nchi inaelekea kubaya zaidi kwani watu wameajikita zaidi katika kuzungumzia masuala ya mtu mmoja mmoja badala ya kuzungumzia masuala ya kitaifa.

Alisema hivi sasa nguvu nyingi inaonekana kutumika kuzungumzia ugomvi wa mtu mmoja mmoja badala ya kuzungumzia umasikini uliokithiri wa wananchi.

Mbatia alisema kama hali hiyo itaendelea, kuna hatari ya taifa kukatika vipande vipande, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa Tanzania inayosifika kuwa ni nchi yenye amani na utulivu.

“Ndugu yangu, nilishawaeleza kuwa kama waandishi, mna jukumu kubwa sana la kuhakikisha taifa linarejea katika mstari wake, na wala si kuendekeza vita vya watu wasioangalia matatizo ya wananchi,” alisema Mbatia.

Alisema vielelezo alivyovitoa Rostam ni ishara tosha ya kile kinachofanyika katika nchi hii, ambayo kila kukicha, watu wamekuwa wakiangalia namna ya kuendeleza mapambano yanayotishia ustawi wa maisha ya Watanzania walio katika lindi la umasikini.

Kwa upande wake, Profesa mstaafu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Issa Shivji, alisema mchakato wa kisiasa hivi sasa unaelekea kubaya zaidi, kwani watu wameshaanza kukosa mwelekeo wa kulipeleka taifa sehemu inayotakiwa.

Alisema alichokisema Rostam ni maoni yake, na hata vielelezo alivyovitoa vipo wazi, hivyo yeyote mwenye kupinga au kuwa na hoja nyingine, atumie utaratibu wa kisheria.

“Nionavyo, siasa haielekei pazuri hata kidogo, na hiyo ni ishara mbaya kwa taifa, sina cha kusema katika kile alichokisema Rostam,” alisema Shivji.

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema yeye alimtaka Mchungaji Christopher Mtikila na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kumuomba radhi Rostam kwa kudai hawatapokea fedha zake ilihali wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda mrefu.

Mrema ambaye ni Mlutheri kiimani, alisema ili Mtikila na KKKT wajisafishe, ni vema wakarejesha fedha za mbunge huyo ambaye tangu zamani amekuwa bega kwa bega akishirikiana nao katika shughuli zao za maendeleo ya makanisa yao.

Alisema ni udhalilishaji wa hali ya juu na kumkosea heshima Rostam ambaye anatumia fedha kutoa misaada kila anapoombwa kufanya hivyo na KKKT na Mtikila.

“Wao kama wanaona hawataki fedha za Rostam, ni vema wakarudisha fedha zake tangu alipoanza kuwasaidia, lakini si vema kumdhalilisha kama wanavyofanya hivi sasa,” alisema Mrema.

Alisema Mtikila kamwe hawezi kuepuka lawama, kwani amekuwa akipiga kelele kuhusu ufisadi, wakati yeye mwenyewe amekuwa akiwazunguka watu kwa kwenda kupokea fedha za Rostam, ambazo ni hivi karibuni tu alidai zilitokana na ufisadi.

Mrema alisema vita ya ufisadi kamwe haiwezi kutokomezwa kama watu wanazungukana na kutumia fedha zinazotokana na mazingira yanayolalamikiwa.

Aidha, kuhusu kauli ya Mtikila kukopa fedha kwa Rostam, Mrema alisema hoja hiyo haina nguvu, bali kinachotakiwa hivi sasa ni kwa Mtikila kuzirejesha, na si kuanza kuwaambia watu kuwa fedha hizo ni za serikali au alikopa kwa mradi binafsi.

“Kwani Mtikila hajui vyombo vya kukopa fedha mpaka akaenda kwa Rostam, tena kwa nguvu ya kusema ni za ujenzi wa kanisa? Azirejeshe ndipo awe na nguvu ya kuukemea ufisadi,” alisema Mrema.

Pia aliigeukia KKKT kuwa haina haki za kuuambia umma kuwa wanasiasa waliache kanisa kwani lenyewe ndilo lililojiingiza katika siasa mwaka 2005, pale walipotagaza kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu.

“Nimeshangazwa kweli na tamko la KKKT kuwa, wanasiasa waliache, wao ndiyo wanaojiingiza katika siasa kwa kuwaaminisha Watanzania kuwa kiongozi fulani ndiye anayefaa,” alisema Mrema.

Alisema wanasiasa ndiyo watu wanaopaswa kuliambia kanisa liachane na masuala ya siasa, lakini si kanisa ambalo limeonekana dhahiri kuwa na upendeleo.
 
invisible tunakazi..si ndogo...hata baadhi ya wapiga domo Bungeni wanapiga ili kupandisha price zao kwa mafisadi...the more anapopiga domo price yake kwa mafisadi inakuwa kubwa...ikiwa mtu anachukua 3M maana price yake ipo chini...

Unamkumbuka mzee wa "VIBOMU" Mzindakaya?
 
Sasa tunamwomba akija hapa USA...RATIBA YAKE ISASAHAU KULITEMBELEA KWANZA KABURI LA BALLALI!
NAMWAMBIA TENA KAMA HAWEZI URAIS AJIUZULU MARA MOJA!
LA SIVYO WASHINGTON ASIRUKE!
TENA NA HIVI ANAMTETEA BASHIR KWA KUJIDAI ETI NI MSIMAMO WA AU?!

MMELIWA!

kwi!kwi!kwi!
Jmushi itabidi mmtime akitua tu hapo US mmshambulie kwa maswali ya papo hapo.Msipe mwanya wa kujiandaa.
Alfu muulize kwa nini huko US anapiga sana trip wkt kuna baadhi ya sehemu toka achaguliwe kuwa RAIS hajawahi kutembelea au kuzuru?Au nyie huko mnamgharamia safari hizi za huko nauli,msosi.kulala,shopping n.k tunaomba majibu jmushi.
 
Unamkumbuka mzee wa "VIBOMU" Mzindakaya?

Huyu walimpooza kwa kumpatia mkopo wa Mabilioni kutoka BOT ambao serikali na BOT ndio ambao wamemwekea dhamana.

Ila kwani mlikuwa mnamchukulia Reverend kuwa yupo serious?

Kumbukeni wakati Dr.Slaa alipoitoa list of shame ama JK 11 huyu alimwendea.

TAHADHARI, KWA WALE mnaoandika huyu Pastor kuweni makini kwani anaweza kuiburuza JF mahakamani .

Nawatakia kheri.
 
Sasa naamini kuwa Mtikila ni FISADI na aliweza kupewa fedha na Rostam kiasi cha shilingi milioni 3 ili kulipeleka gazeti la mwanahalisi mahakamani.

Siku ambayo Mtikila alilipwa ,kwa mujibu wa tarehe zilizoko kwenye vocha aliyoonyesha Rostam ndio siku hiyo hiyo alifungua kesi ya madai dhidi ya gazeti la mwanahalisi kuwa limemchafua.

Pili siku hiyo hiyo ndio siku ambayo Rostam alifungua kesi dhidi ya gazeti la mwanahalisi ya madai kuwa gazeti lilimchafua.

Kila mmoja anadai mabilioni kwenye kesi hizo.

Swali ni kwanini siku hiyo hiyo wafungue kesi wote kwa pamoja?
Kwa nini hiyo siku ndio iwe siku ya Mtikila kuchukua pesa kwa Rostam?

Namalizia kwa kusema kuwa huyu Mtikila ni fisadi.
 
Huyu mchungaji nilishawaambia ni muhuni na kuna wahuni wengi sana katika hizi harakati. Uzuri ni kwamba ni swala la muda; wataambuka moja baada ya mwingine. Sasa nani atamsikiliza tena Mtikila, kwisha habari yake na hao mawakala wa ufisadi hawatamhitaji tena!
 
Katika kipindi hicho hicho Mtikila alienda mahakamani kulishitaki gazeti la Tanzania Daima kuwa limemchafua na anadai bilioni 3.

Huyu ndio reverend Mtikila na kesi zote hizo zipo mahakama kuu kanda ya DSM .

HUYU NI FISADI.
 
Back
Top Bottom