Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Rostam azua mapya
Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliuelezea mjadala unaozingira suala hili zima kuwa usio na msingi, na ambao unapaswa kukomeshwa.
Hata hivyo, Zitto alisema Rostam alipaswa kutambua kuwa, mbegu za ubaguzi ambazo zinajionyesha leo hii katika taifa, chimbuko lake ni kundi la mtandao ndani ya CCM, ambalo mbunge huyo wa Igunga alikuwa mmoja wao.
Alisema harakati za kibaguzi zilizoendeshwa na kundi hilo la mtandao dhidi ya mwanasiasa na mwanadiplomasia Dk. Salim Ahmed Salim, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala, ndiyo msingi wa vitendo vya kibaguzi leo hii.
Baadhi yetu tulipata kuonya mapema kuhusu utamaduni wa kibaguzi, uliokuwa ukiratibiwa na kundi la mtandao, ambalo Rostam ni mmoja wao, wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005. Tuliwaeleza mapema kabisa kwamba ipo siku mambo haya yatawarudia, alisema Zitto mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika nchini.
Hata hivyo, Zitto alisema alikuwa akiamini kwa dhati kuwa, kama Mtanzania, Rostam Aziz alikuwa na haki ya kualikwa na kwenda katika hafla ya Kanisa la Kiinjili ya Kilutheri.
Alisema angepata nafasi ya kumshauri Rostam kabla ya kwenda pale, angemtaka aende akashiriki katika shughuli ile na kutoa mchango wake na kuondoka pasipo kusema neno.
Kilichowastua watu wengi ni yale maneno aliyoyasema alipokuwa kanisani, na si kwenda kwake pale kwani mimi naamini kama Mtanzania alikuwa na haki ya kuitikia wito na hata ikibidi kuchangia, alisema Zitto.
Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Rostam kuwa kuna kundi la watu maarufu na wazito ambao wana ajenda ya kuchafua baadhi ya watu, Zitto alikuwa na haya ya kusema: Mbona unaniuliza kitu ambacho hata wewe unakijua? Ni jambo la kweli kwamba kuna makundi, na wewe unalijua hilo. Ninachosema mimi mjadala mzima huu hauongezi tija yoyote.
Yes, I couldn't have said it better. Lazima tuliangalie hili jambo katika picha kubwa. Hawa jamaa wamekuwa wakituchezea mchezo wa chesi; wanaunda kamati wakijifanya kushughulikia ufisadi kumbe wana lengo la kuchafuana na kusafishana. Damu hii ya ubaguzi inaanza kuwatafuna ndani kwa ndani na wenyewe kwa wenyewe na itawamaliza wote. Walimtafuna kiongozi wetu shupavu Salim Ahmed Salim wakijua ndio mwisho. Walisahau kwamba mchawi hawezi kuishi bila kuloga. Uzuri ni kwamba mchawi huwa halogi nje ya ukoo wake, sasa watatafuna hadi wa mwisho. Watazunguka wee mwisho wa yote watamfikia boss wao JK na uponyaji wa taifa letu ndipo utakapoanza.
Zitto hapa amekomelea msumari wa mwisho.