Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Re: In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Quote: Pundit

tatizo langu ni kuwa rule of law haikufuatwa.



Quote: Field Marshall ES

Mkuu Pundit,

No question kwamba you are an-intelligent man, lakini hapa kwenye hii topic unachanganya ishus mkuu, iliyomkuta Lowassa ni the rule of politics sio the rule of law,

Warioba na Butiku, kama kweli wako concerned na the rule of law wangesikitika kwamba Daniel Yona na Rostam Aziz, wameitwa kisheria na kamati teule ya bunge na wamekataa kwenda, na nothing happened to them, nilifikiri wewe Pundit na Warioba na Butiku, mngekuwa concerned zaidi na hilo badala ya noneishu ya sheria ambayo haikumhukumu Lowassa, ila Lowassa kukimbia kivulichake mwenyewe, kutokana na the rule of politics!
[/
B]

Quote: Wabunge Dodoma

Alisema Rostam katajwa kuwa na uhusiano na Richmond na pia anatajwa kuwa na uhusiano na kampuni ya Dowans inayoendesha shughuli za Richmond kwa sasa na akahoji kwa nini Mbunge huyo na Waziri wa zamani, Daniel Yona, wasichukuliwe hatua kwa kugoma kwenda kutoa ushahidi mbele ya kamati ya Bunge.

Mkuu Pundit,

Heshima mbele mkuu, sasa wabunge wameanza kuongea lugha yetu hapa JF tuliyoisema majuzi, ona mwenyewe quotes hizo, as a nation haya ndiyo tunayoyataka mkuu!
 
bom.jpg

SOON...............boom....kitaeleweka nani yumo nani hayumo
 
Ni kwa nini huyu Rostam Aziz hakuwepo bungeni wakati anajua issue yake inajadiliwa? Bado analileltea bunge jeuri; bora bunge lenyewe lianze kumuadhibu then CCM wafuate(kama wana ubavu) halafu vyombo vya dola vichukue mkondo wake. siku zote hawa Watz wenye asili ya kiasia huwa sio wazalendo kabisa.
BIG UP! UNAPOSEMA WATU HAWA HAWANA U
ZALENDO VIBARAKA WAO WATAINUKA NA KUANZA KUTETEA KUWA SASA TUNALETA UBAGUZI, WHILE IN REAL SENSE "HAWANA UZALENDO NA NJI HII"
 
Inatia moyo sana, hapa JF tuna best political analyst in Tanzania. Huyu Rweyemamu tulisha mzungumzia kwamba anachangia kufight kupeteza scandal ya Richmond. Lakini JF tulisimama kidete and fight hard against this cheaters.

I am feeling sadly, this people knew from beggining that we have beeen traped.
 
Heshima Mbele wakuu wangu,
Mwanzoni watu waliposikia EL amejiuzulu wengine walimsifu na wengine baadaye walimsifu JK kwa kuvunja baraza la mawaziri na kuunda jipya. Mimi nilikuwa na shaka kwanza nilikuwa nona kama ni same Babali game.
Sasa hapa inakuwa inatuchanganya sana baadhoi yetu, which one is likely to take a course, Rule of Law, rule of politics, rules of Party, au utaratibu wa bunge. Kuna suala la immunity vilevile, na hawa jamaa ni wabunge halali wa chama cha Mapinduzi na vilevile ni wajumbe wa vyombo vikubwa vya chama. Pamoja na yanayosemwa bungeni na else where tunaweza tukawa tunachezewa shere, huenda huwa jamaa wataishia kuwekwa kando tu, na hawatafanywa lolote!
 
Unajua natafuta adhabu ya kumfanya Rostam azizi mfano kwa wenzie wote. Dawa yake ni kumshusha pale Manzese kisha vijana wangu waambie yule ndio Rostam Azizi aliyesababisha watoto wenu wasikalie madawati, yule ndio aliyesababisha mabomba ya maji ya kipasuka yasitengenezwa, yule ndio amesababisha watoto wenu wasisome usiku sababu umeme unakatika, sababu yule ndio aliyekula pesa zenu, sasa nyinyi ndio majudge mfanyieni hukumu.

Vijana wangu watapiga gabachori yule, na hiyo ndio mwisho wake.
 
Beatrice alisema kwamba tangu kutolewa kwa ripoti hiyo kuna baadhi ya watu wamekuwa wanatishiwa na akatoa mfano kuwa familia yake, yeye na mume wake, William Shelukindo, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kutokana na kukazania suala hilo hadi likaundiwa tume, sasa wanatishiwa maisha.

“Mimi na Mzee Shelukindo tumeanza sasa kujihoji kuwa labda tuandike wosia tukabidhi kwa mwanasheria kutokana na hali hii ilivyo sasa, lakini hatuogopi maana tunatetea maslahi ya taifa,” alisema Beatrice. Alisema haogopi mtu, kwani anafahamu kuwa mlinzi pekee wa maisha ya mtu ni Mungu.

Tanzania tunaelekea pabaya. CCM ndiyo iliyotufikisha hapa.
 
Jamani,

Someni ile thread ya Richmond: The facts iliyopo pale juu. Wengine tulishawaambia kabla ya haya mambo long time ago kuwa Muungwana anahusika hamkutaka kusikia..................!

Sasa.................?
 
Tanzania tunaelekea pabaya. CCM ndiyo iliyotufikisha hapa.

pia angalia vyema mkuu nukuu yako inaonyesha ni jinsi gani kuwa hoja hii iliibuliwa bungeni na CCM na sio upinzani kama wanavyotaka wananchi waamini.


na hata ukifatilia utaona jinsi gani wabunge wa CCM walivyo wakali zaidi kuliko hata wa upande wa pili.
 
pia angalia vyema mkuu nukuu yako inaonyesha ni jinsi gani kuwa hoja hii iliibuliwa bungeni na CCM na sio upinzani kama wanavyotaka wananchi waamini.


na hata ukifatilia utaona jinsi gani wabunge wa CCM walivyo wakali zaidi kuliko hata wa upande wa pili.

....huna hata aibu mpuuzi wewe!
 
pia angalia vyema mkuu nukuu yako inaonyesha ni jinsi gani kuwa hoja hii iliibuliwa bungeni na CCM na sio upinzani kama wanavyotaka wananchi waamini.


na hata ukifatilia utaona jinsi gani wabunge wa CCM walivyo wakali zaidi kuliko hata wa upande wa pili.

Mtu wa pwani, mtu wa pwani!

najua unataka na wewe kuwa maarufu humu, lakini post zako kutokana na kutofanya homework ya kutosha unaishia kuwa moja ya vilaza kwenye hii forum. Mama kilango moja ya watu ambao ni wasemaji wazuri kabisa amesema mbele ya taifa kuwa CCM iliwaachia wakina kabwe kuikosoa na akasema kuwa sasa hivi na wao wameamka. Sasa hao ccm unaotaka kuwasifia kuwa ndiyo wameleta hoja walikuwa wapi siku zote. Kwa taarifa yako ukiona mpinzania wako anagombana na mke wake inabidi ukae kimya ila wajimalize wenyewe kwa jamii ukiaanza kusema sana watashtuka?
Kwa hiyo wapinzani wamekaa kimya wakati chama unachokipenda kikijikaanga chenyewe kwa mafuta yake na ukifika muda wa kukitafuna itakuwa rahisi. OMBI nakuomba ufanye utafiti inalau kidogo unapoleta hoja yako iwe na nguvu na kumbuka kuwa unaongea na Tanzania yote na sio watu wa Pwani pekee
 
Watazidi kugawanyika na ukweli utaonekana!


Richmond yaigawa CCM

na Mwandishi Wetu


UPEPO mbaya wa kisiasa unavuma ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa tisa wa Tanzania, Edward Lowassa.
Habari za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zilizoifikia Tanzania Daima zimeeleza kuwa, kishindo cha kujiuzulu kwa Lowassa kimewagawa vigogo na makada maarufu wa CCM, jambo linalotishia uhai na uimara wake.
Habari hizo zimeeleza baada ya Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura, ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya Marekani, Dk. Harrison Mwakyembe, kusoma ripoti ya kamati hiyo bungeni wiki iliyopita na kumtaja aliyekuwa Waziri Mkuu Lowassa kuwa mhusika mkuu wa kashfa hiyo, makada wa chama hicho waligawanyika makundi mawili, kundi moja likiiunga mkono ripoti hiyo na jingine likiipinga.
Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya CCM vimelidokeza gazeti hili kuwa, baadhi ya wabunge, makada wa chama hicho tawala na waliokuwa mawaziri katika baraza lililovunjwa wiki iliyopita hawakubaliani na ripoti ya Dk. Mwakyembe kwa madai kuwa ilipikwa kwa ajili ya kumuangamiza Lowassa.
Kundi hilo linadai kwamba ripoti hiyo ilitengenezwa makusudi kwa ajili ya kummaliza Lowassa kisiasa na watu walioandaliwa na kundi la mahasimu wake kisiasa.
Taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili kutoka kwa watu walio karibu na Lowassa kikazi zilieleza kuwa, ripoti ya Dk. Mwakyembe iliyomtaja Lowassa kuwa mhusika mkuu katika sakata la Richmond, ni kisasi cha kisiasa dhidi ya kundi la wanamtandao ambalo katika siku za karibuni limekuwa likiangaliwa kwa jicho baya na baadhi ya wana CCM wasiokuwa wanamtandao.
Zinaeleza zaidi kwamba, baada ya kundi la wanamtandao kubaini vita inayopiganwa dhidi yao, pamoja na kushitushwa na hatua zinazochukuliwa sasa na Rais Jakaya Kikwete za kuisafisha serikali yake, kundi hilo liliamua kukaa kimya likisubiri kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri kabla halijachukua msimamo wa jinsi ya kutetea nafasi ya kuwepo kwake ndani ya chama hicho.
Habari zaidi zinaeleza kwamba, kukosekana kwa Dk. Mwakyembe au mjumbe mwingine yeyote wa kamati yake katika baraza jipya la mawaziri kumechukuliwa kuwa ni ushindi wa kundi linalomtetea Lowassa na rafiki yake wa karibu Rostam Aziz, wanasiasa wanaotajwa kuwa maadui wakubwa wa kisiasa wa wana CCM wasio wana mtandao.
Watu hao wanaojumuisha mawaziri waliorejeshwa katika serikali mpya wanasema, uteuzi huo wa rais wa kuwaweka kando kina Mwakyembe na wabunge wote wa CCM waliomshambulia Lowassa na wenzake waliotajwa ndani ya Richmond unaonyesha kwamba, hakufurahishwa na namna kamati hiyo ilivyofanya kazi yake.
Kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, muda mfupi tu baada ya Bunge kuthibitisha uteuzi wake wa asilimia 98.9 mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusu ripoti hiyo ni ushahidi wa kutosha kwamba taarifa za mgawanyiko huo zimefika ngazi za juu.
Pinda katika kauli yake hiyo aliwataka wabunge kuachana na imani za kuiona ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Mwakyembe kuwa iliyo fanya kazi kwa lengo baya la kumuumiza mtu fulani.
Baadhi ya wajumbe wa kundi hilo la wanamtandao wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM na wale wa Sekretarieti ya chama hicho ambao mwishoni mwa wiki iliyopita waliongoza mapokezi ya kimya kimya ya kumpokea Lowassa alipofika Dar es Saalam akitokea Dodoma, wamekaririwa wakieleza kuwa, tayari walikuwa wameshajipanga kujibu mapigo.
Wakati hali ikiwa hivyo, kundi jingine linalodaiwa kuwa limeundwa mahususi kwa ajili ya kuwashughulikia wanamtandao huo wa Lowassa na Rostam likiongozwa na mmoja wa viongozi wa juu katika moja ya taasisi tatu zinazoongoza dola (ambaye ni mwanamtandao aliyeasi), linaamini kuwa ushahidi uliotumika kumtia hatiani Lowassa ni sehemu ndogo tu ya kashfa zinazomuandama kiongozi huyo.
Baadhi ya watu wazito kutoka ndani ya kundi hilo waliozungumza na gazeti hili hivi karibuni kwa nyakati tofauti, walieleza kuwa ushahidi iliomtia matatani Lowassa ni sehemu ndogo tu ya ushahidi kamili ambao kamati hiyo inao.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo alieleza kuwa kama ripoti hiyo ingetoa ushahidi wote uliokuwa ukimgusa Lowassa katika sakata hilo, serikali ingepata mtikisiko mkubwa ambao ungeweza kuiyumbisha.
Habari zaidi zinaeleza kuwa, Kamati ya Dk. Mwakyembe ilipokea ushahidi mwingi uliokuwa ukimuhusisha Lowassa na kashfa hiyo lakini ilifanya kila linalowezekana ili kulinda hadhi ya waziri mkuu. Zinaeleza zaidi kwamba, ingawa wajumbe wa kamati hiyo waliapa kutomwangalia mtu bali masilahi ya taifa, walifanya kila njia kuhahakisha hadhi ya waziri mkuu inalindwa kwa kutotoa ukweli wote dhidi yake. Baadhi ya watu hao wanasema iwapo watathibitisha pasipo shaka kwamba, wanashambuliwa, basi upo uwezekano wa wao kuhakikisha kila kitu kuhusu Richmond na namna kinavyomgusa Lowassa na Rostam watakianika ndani ya Bunge baada ya mjadala kuhusu suala hilo unaoanza leo.
 
Mchungaji Kishoka tutafasirie maandiko:

"Hakuna ushkaji mkubwa kuliko huu, wa fisadi mmoja kuutema ulaji kwa ajili ya washkaji zake" (Richmonduli 8:18)

"Kwa maana jinsi hii Lowassa alimpenda JK, hata akautema u-PM, ili kila aliyerichimondi asilowaswe bali awe na ulaji wa milele" (Bangusilo 3:16)

Inaitwa Kufa kufaana. Kwenye kisa cha Wajinga ndio walia, wakumbuka walivyofikiri kuwa kila mtu ni mjinga na mwadhana akasema "mwalimu umenibaini, moja yangu moja yako"?

Hawa jamaa walifikiri sisi ni Wajinga, Wapumbavu na Wazubafu. Wasipoangalia na kuwa wakweli kwa dhamiri na utiifu, wataangamia kwa kupigwa mawe.

JK has deep "sheet" in his hands. He has crisis that is about to explode like Oldonyo Lengai! Yeye anafanya mambo Kiswahili akifikiri basi moto atautuliza.

What he keeps forgeting is a base of enemies he created by building Mtandao and allow Mtandao to deep their fingers on national treasure!

Sasa sijui hii recklessness ni kwa ajili ya gumzo eti "mzungu bye bye" na 2010 ataachia ngazi na EL kuanza kujiandaa au ndio typical character ya uswahili, never take things seriously!

Yetu macho! He better see the writings on the wall "VDG, VDG, unaangamiza Taifa"!
 
Unajua natafuta adhabu ya kumfanya Rostam azizi mfano kwa wenzie wote. Dawa yake ni kumshusha pale Manzese kisha vijana wangu waambie yule ndio Rostam Azizi aliyesababisha watoto wenu wasikalie madawati, yule ndio aliyesababisha mabomba ya maji ya kipasuka yasitengenezwa, yule ndio amesababisha watoto wenu wasisome usiku sababu umeme unakatika, sababu yule ndio aliyekula pesa zenu, sasa nyinyi ndio majudge mfanyieni hukumu.

Vijana wangu watapiga gabachori yule, na hiyo ndio mwisho wake.

huyu dawa yake apelekwe KEKO au UKONGA au MAWENI(tanga, huko ndo ataiona joto ya jiwe! kwa jinsi alivyo na sura tamu wallah wata mgombea kama nn! halafu ile ngozi ikishika ukurutu na kuliwa na kunguni atajuta majuto yote ya wazee wake na mashetani waliomtuma kudhulumu maskini!!!!
............ mbona wana mchelewesha sana???? hivi angekuwa ni kabwela kama yule mbunge wa kihansi alie mtaja kuwa alipelekwa ndani kwa kutaka kuangusha nguzo maana zinapeleka umeme kwa hao hao mafisadi na kuwaweka wao wenye chanzo gizani! ........hapa ndio naanza kupata shaka kuwa HAWAKO PEKE YAO hili deal linaweza kuwa la wengi........tena wakubwa zaidi yao..... kwenye hotuba ya muungwana tumemsikia akimwaga masifa kibao kwa white head.
...... ila tusubiri tuone......
 
Rostam Aziz akaangwa
Shadrack Sagati, Dodoma
Daily News; Friday,February 15, 2008 @00:01

BAADHI ya Wabunge wamependekeza Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), achukuliwe hatua za kisheria kutokana na kutajwa kuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya Richmond inayodaiwa kuihadaa Serikali katika makubaliano ya kuzalisha umeme wa dharura.

Wakichangia ripoti ya Kamati teule ya Bunge juu ya mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura wa kampuni ya Richmond bungeni jana, wabunge hao walisema kitendo cha Mbunge huyo kugoma kwenda kutoa ushahidi katika kamati hiyo ni dharau kwa Bunge na kwa Spika aliyeiunda.

“Hatuwezi kuhoji kwa sasa kwamba Richmond ni ya akina nani. Ukweli uko wazi kuwa ni wale walioshinikiza kampuni hiyo ipewe mkataba,” alisema Mbunge wa Sikonge, Juma Mkumba (CCM).

Alisema Rostam katajwa kuwa na uhusiano na Richmond na pia anatajwa kuwa na uhusiano na kampuni ya Dowans inayoendesha shughuli za Richmond kwa sasa na akahoji kwa nini Mbunge huyo na Waziri wa zamani, Daniel Yona, wasichukuliwe hatua kwa kugoma kwenda kutoa ushahidi mbele ya kamati ya Bunge.

Alisema Rostam ni aibu kwa CCM, kwa vile ni Mbunge wa chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na kuongeza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameingia kwenye siasa ili kuficha maovu yao.

Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), alisema ni vyema Rostam achukuliwe hatua, kwa vile ni kiongozi wa CCM na yuko kwenye Halmashauri na Kamati Kuu ya chama hicho. Alisema kitendo cha Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, kunukuliwa akimtaja Rostam kuwa na uhusiano na Richmond ni ushahidi wa kutosha.

Alieleza kuwa kwa vile waliotajwa kuhusika katika mkataba huo ni viongozi wa serikali, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) halina tena jukumu la kulipa fedha kwa Dowans na badala yake serikali. Hata hivyo, wakati suala hilo linajadiliwa jana, Rostam hakuwamo katika ukumbi wa Bunge.

Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, alisema kitendo cha mawaziri kujiuzulu kwa kuhusishwa na kashfa hiyo hakiwezi kupooza suala la Richmond na badala yake alitaka fedha zote ambazo zimelipwa kwa kampuni hiyo zirudishwe na wahusika wote, bila kujali vyeo, wafilisiwe.

Beatrice alisema kwamba tangu kutolewa kwa ripoti hiyo kuna baadhi ya watu wamekuwa wanatishiwa na akatoa mfano kuwa familia yake, yeye na mume wake, William Shelukindo, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kutokana na kukazania suala hilo hadi likaundiwa tume, sasa wanatishiwa maisha.

“Mimi na Mzee Shelukindo tumeanza sasa kujihoji kuwa labda tuandike wosia tukabidhi kwa mwanasheria kutokana na hali hii ilivyo sasa, lakini hatuogopi maana tunatetea maslahi ya taifa,” alisema Beatrice. Alisema haogopi mtu, kwani anafahamu kuwa mlinzi pekee wa maisha ya mtu ni Mungu.

Kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid (Wawi-CUF) alisema hakuna haja ya watu kuandamana kufurahia watu kujiuzulu, kwani bado Watanzania wengi wako kwenye matatizo na sehemu nyingi za Tanzania ziko gizani.

“Hakuna haja ya kuandamana eti kwa vile Rais amevunja Baraza. Watu wetu bado wanateseka. Mimi naomba wabunge wenzangu tuungane kudai mikataba yote ije bungeni,” alisema. Alisema serikali ina jukumu la kuishitaki Richmond irudishe fedha zote ambazo imelipwa wakati ni kampuni ya kitapeli na akapendekeza Tanesco iache kulipa fedha ambazo zinatokana na mkataba huo wa kitapeli badala yake serikali ilipe.

Mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai (CCM), alihoji zinakokwenda fedha zinazolipwa kwa Dowans na kutaka malipo yote yasimamishwe. Alisema kama kuna Watanzania ambao wanahusika kuileta nchini au kutunga uongo ionekane ipo ni vyema wakafilisiwa na kufikishwa mahakamani.

“Sasa kusiwe na mchezo, nyie mawaziri mlioaminiwa na Rais chapeni kazi, lakini jifunzeni kwa wenzenu,” alisema Msindai ambaye katika hoja yake, pia alisisitiza Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ifumuliwe na iundwe upya.

Grace Kiwelu (Viti Maalumu -Chadema) alipendekeza waliotajwa katika kashfa ya Richmond wanyang’anywe hati za kusafiria ili wasitoroke nchini wakati wakisubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na wanaolalamika kuwa hawakutendewa haki na Kamati ya Bunge waende mahakamani wakasikilizwe madai yao.

Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja (CCM), ambaye aliwahi kuwa Waziri alisema hivi sasa kuna wimbi la watu kuiba fedha za umma kwa kutumia kalamu na kampuni hewa. Alitoa mwito kwa serikali kuhakikisha wanapambana na eneo hilo kama ilivyofanya kwa ujambazi.

Hoja hiyo itahitimishwa leo kwa mtoa hoja, Dk. Harrison Mwakyembe, kujibu yaliyoelezwa na wabunge. Baadaye Bunge litayajadili mapendekezo yaliyotolewa na Kamati na kuyaboresha kabla ya kupeleka maazimio Serikalini.







Wasemavyo wasomaji:
BRAVO GRACE, UMEONGEA POINT. KEEP IT UP
 
.hapa ndio naanza kupata shaka kuwa HAWAKO PEKE YAO hili deal linaweza kuwa la wengi........tena wakubwa zaidi yao..... kwenye hotuba ya muungwana tumemsikia akimwaga masifa kibao kwa white head.
...... ila tusubiri tuone......

jana sikuamini masikio yangu niliposikia hotuba ya muungwana jinsi ilivo kuwa nyepesi nyepesi yenye mizaha mizaha wakati taifa lipo katika mtikisikoo mkubwa namna hii.

Naelekea kuamini kabisa kwamba Tatizo kubwa tulilo nalo Tanzania ni raisi wetu ndo maana upuuzi wote huu umeendelea akiuona na pengine kuubariki!

Njia ya kujikomboa ni kuondoa kiini cha tatizo, vinginevyo tutaendelea tibu jipu la mguuni kesho linaibukia usoni kwani damu bado inabakia kuwa chafu!( Nukuu bunge la jana)
 
pia angalia vyema mkuu nukuu yako inaonyesha ni jinsi gani kuwa hoja hii iliibuliwa bungeni na CCM na sio upinzani kama wanavyotaka wananchi waamini.


na hata ukifatilia utaona jinsi gani wabunge wa CCM walivyo wakali zaidi kuliko hata wa upande wa pili.

Sina haja ya kujua kama wewe ni sisiemu ama la, ila ningependa kukukosoa kwamba hoja hizi za kufichua uozo kule kwenye Richmond na kwingineko zililetwa na wapinzani sio sisiemu kama wewe na mwenzako Kpt. John Chiligati mnavyotaka kutuaminisha.
Long Live Tanzania!
 
Sina haja ya kujua kama wewe ni sisiemu ama la, ila ningependa kukukosoa kwamba hoja hizi za kufichua uozo kule kwenye Richmond na kwingineko zililetwa na wapinzani sio sisiemu kama wewe na mwenzako Kpt. John Chiligati mnavyotaka kutuaminisha.
Long Live Tanzania!

HOJA SI WABUNGE WA SISIEM KUWA WAKALI. ILA ELEWA WALIOANZISHA HII MOTION NI OPOSITION NA MEDIA.HAWA JAMAA WAMEIRUKIA BAADA YA KUONA NGOMA NI NZITO NA HAWANA JINSI YA KUNUSURU CHAMA CHAO. SUBIRI UONE WATAKAVYO IRUKIA YA BUZWAGI. WATASAHAU KAMA WALIMUADHIBU NAYO ZITTO.
 
Mtu wa Pwani-waswahili husema kuwa mbwa akitaka kufa huwa anaziba pua zake mwenyewe.

CCM hapa wamepigwa bao hawana budi kukubali na kujiandaa kujipanga kusonga mbele ,wasiangalie wameangukia wapi ila waangalie walijikwaa wapi.

Mwisho wa sppining ni huu na hapa wananchi wameamka kuliko hapo miak ya 70 ndio maana hata wakina Kingunge et-all walipojitokeza kumpinga DR,slaa wananchi walisimama kidete na kusema ukweli bila hofu wala woga.

Long live Tanzania .....long way to 2010.
 
Back
Top Bottom