Nakuhurumia Dar-es-salaam,yaani hadi sasa hujaelewa watu wanamlalamikia Rostam kwa lipi?Rostam kama kiongozi wa umma anahusishwa na kuliingizia taifa hasara na ufisadi hizo ndizo tuhuma zake kwenye richmond na mambo mengine.Hayo mambo yote ni ya kijinai,mwananchi wa kawaida hawezi kushtaki sijui nikuwekee hapa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ndio uelewe,au tu nikupe link kwa faida yako tembelea
www.parliament.go.tz sehemu ya documents,click acts,halafu tafuta hiyo sheria,ndiyo inayoongoza mashtaka nchini.Usibwabwaje kama hauna research.DPP ndiye mkuu wa mashtaka hata ukianzisha private prosecution bado yeye ana uwezo wa ku-continue au kudiscontinue proceedings.Pia kasome katiba ya Tanzania mabadiliko ya kumi na nne halafu ndio uje hapa.Kutokana na legal technicality ya kifungu cha 190 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,mwananchi wa kawaida hawezi practically kufungua hayo mashtaka ya jinai na ndio maana wewe ukienda kushtaki polisi,mahakamani unageuka kuwa shahidi(PW1) na jamhuri ndio inatakeover kila kitu. Kama kuna mtu anakushauri basi anakushauri vibaya,usiiingilie professional.Tulia tukueleze wenye field.
Kama Rostam angekuwa amemdhulumu mwananchi yeyote mbuzi shamba au jogoo ungeshaona kesi pale kisutu,lakini kwa kuwa suala ni wizi na udanganyifu kwenye mali ya umma,linarudi palepale kwenye penal code cap.16 chini ya DPP.Mi nakupa shule ya bure tu hulipii wala nini hivyo usikonde leta maswali yako tu,umekutana na reseacher.Wote tunangoja sheria zifuate mkondo wake lakini kwakuwa zimekuwa hazifuati huo mkondo na ndio maana tunatumia uhuru na haki yetu inayolindwa na ibara ya 18 ya katiba,ibara ya 8 ya katiba na ibara ya 27 ya katiba na kukusaidia tu nitakunukulia hapa ibara ya 8 na ya 27 manaake najua ibara ya 18 unaijua.
8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni
ustawi wa wananchi;
(c)
Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
mwenzetu ibara ya 8(b) unaielewaje? au ustawi unaozungumziwa hapo ni ustawi wa ninyi mafisadi wachache? basi wafute hapo waseme mafisadi.na wanaposema serikali itawajibika kwa wananchi wana maana gani?hujui nyamaza
27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri
ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote
inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali
ya mtu mwingine.
(2)
Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya
mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu
na ubadhilifu,
na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama
watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.
Ibara ya 27(1) unaielewa? kama ndiyo wajibu wako wewe ni nini chini ya ibara hiyo?hebu nenda mbele zaidi angalia ibara ya 27(2)
katiba inaposema wananchi ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao ina maana gani?
Kwa hakika wewe unasema unampenda jk kwa kweli humpendi kabisa kwani anayempenda jk atamwambia ukweli.He need to be told the truth,hata kama unamuuna.Yupo jaji mmoja kule Uganda anaitwa kanyeihamba ni jaji pekee anayeweza kumface m-7 na kumwambia unayofanya sio,m-7 alimchukia sana lakini,siku moja alipomwita ili amponde mbele ya waandishi wa habari kutokana na hukumu yake aliyoitoa dhi ya besigye Kanyeihamba alikuwa wa kwanza kuchangia mada ya Rais na kumwambia, "Mhe.umeongea vizuri sana na wasikilizaji wako kukupigia makofi,lakini hawahawa waliokupigia makofi leo,ndio hao hao walinipigia makofi mimi hadi ukaniteua kuwa jaji,lakini leo wanakupigia makofi wewe kwa kuiponda hukumu yangu kwakuwa ilikuwa dhidi yako,Mhe.Rais kati ya mimi na hawa nani anakupenda zaidi? mimi nayekwambia ukweli au hawa wanafiki?
M-7 alikosa cha kuongea,matokeo yake,M-7 anamheshimu sana kanyeihamba.
Hivyo hata kikwete yapo mambo mengi sana ya kumjadili yeye kama yeye,yapo tunayompongeza,yapo tunayomponda na yapo ambayo tunamwonesha njia.Kiongozi mzuri ni yule anayekubali kukosolewa sio wewe Dar-es-salaam.