Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Hapa naona manahangaika tu...
Tatizo ni lipo kwenye mfumo mzima wa BUNGE letu... Nguvu ni imewekwa kwa wananchi kuamua kuwa Mbunge walio mteua anawafaa au la - na kwa Mheshimiwa Rostam ni watu wa Igunga wenye uamuzi huo! Ambao wao pia ni sehemu ya taifa.
Wemeshamteua huyo jamaa mara mbili sasa (kama sikosei) na wao ndio wenye nguvu kikatiba yakusema anafaa.
Kama tunahisi huyu mtu ametumia pesa kuwanunua wapigakura -- katika macho ya waTanzania na sheria zetu itabaki amepita kihalali kabisa na ni Mbunge bora kama wataendelea kumchagua na mjenga taifa.
Kama hatukubaliani na hayo basi tutizame mfumo mzima wa BUNGE na UBUNGE
mkuu,
sidhani kama suala la "kuchaguliwa" pekee ndiyo kigezo. Unajua Kibaki anadai kuwa amechaguliwa na wananchi wa Kenya, Mugabe wa Zimbabwe "anachaguliwa" kwa kishindo huko kwenye chaguzi zake.
Huyu Rostam anahusishwa na wizi mkubwa sana wa pesa za walipa kodi na pia anahusishwa na Richmond (kupitia Dowans) kuinyonya nchi yetu. Kwa vyovyote vile ana uwezo wa "kushinda" uchaguzi wowote akitaka kwa kutumia hata asilimia moja tu ya pesa zake. Swali kubwa hapa, Je Rostam ni mfano wa kuigwa Tanzania?