Re: Rostam Kuunguruma Kilimanjaro kempisk
1. anasema "mimi si miongoni mwa wale walioshindwa kuishi na wake zao na kuchangamkia watoto wadogo wanaolingana na mabinti zao au wajukuu zao"
Hapa amemsema Six, Mzindakaya, na Flani, lakini huu sio ufisadi kuoa mtoto mdogo sio sawa na wizi kwa taifa.
2. familia yake anasema imekuwa ikifanya biashara 1852 kule Tabora...
Hii ni kweli kabisa sio uongo, lakini it has nothing to do na ufisadi anaotuhumiwa, kwa sababu kampuni ya Dowans na Kagoda hazikuwepo since 1852, hapa hakusema ukweli unaoatakiwa, ila amesema ukweli nusu, swali ni kwa nini?.
3. toba... bomu... "Mtikila mwenyewee alikuwa kuniomba Shs milioni 3 za kuendeleza Kanisa lake na kumpatia, hili la kuwaambia wengine fedha zangu ni dhambi wakati yeye anazipokea ni unafiki, nawapa ushahidi wa malipo hayo kwa Mtikila"!
Hili nilishasema siku nyingi sana kuwa Mtikila huwa sio kiongozi wa kweli, niliwahi kusema huko nyuma kuwa hata CCM wameshamlipia sana nauli za nje ya nchi, hapa Rostam ame-score big point tena big time.
4. anasema huko nyuma alishughulikia kutoa mchango wa kulisaidia Kanisa hilo huko nyuma kwa mwaliko wa Mzee wa Kanisa hilo Mhe. Samuel Sitta...
Sawa sawa again big point kwa Rostam, lakini sasa hivi Six, anamkosesha usingizi ndani ya bunge yeye na wenziwe, yaani mafisadi na najua it is only a matter of time kabla hawajamng'oa u-Spika, ambao ukweli ni huyu huyu Rostam ndiye aliyempa, pia Spika hajasema kitu so far kuhusu Rostam kuto ahle akwa kanisa lake, lakini still badi ni big point kwa Rostam.
5. anahoji mbona wafanyabiashara wa Kikristu wanaoneshwa wakitoa misaada katika ujenzi wa Misikiti, iweje leo muislamu kutoa msaada kanisani?
Hapa hapana, anapandikiza chuki za kidini kwa sababu hao wafanyabiashara wengine waliotoa misaada kanisani au misikitini, yaani anamsema Mengi, sio wabunge na mafisadi kama yeye kwenye hili hapana amekosea.
6. anasema "natoa changamoto kwa mtu yeyote mwenye ushahidi wa vitendo vya uvisadi awakilishe hayo kwenye vyombo vya sheria"
Kama angekuwa na ukweli kwenye hili, basi angeenda kwenye kamati ya bunge alipoitwa na Mwakyembe, halafu anasema hivi kwa sababu anajua kuwa hivyo vyombo vyote vimeshikiliwa na kundi lake,
Hata Balali alisema maneno kama haya wakati ule, ambayo the bottom line au reading between the lines ni kwamba hapa ameweka msingi mzito sana kwa viongozi wengine kuwa be careful nitawasema ninawajua vizuri sana, kwenye hilo ninakubali kuwa Rostam, akiamua kusema ukweli wa viongozi karibu wote aliowahi kuwapa hela, itakuwa aibu ya mwaka Tanzania, yaani ndio siku wa-Tanzania tutalia kilio cha damu kuwajua viongozi wetu mashuhuri wa CCM na Upinzani, ambao wamewahi kupewa hela na Rostam.
Hakujibu swali muhimu la ufisadi wake, ambao ndio hasa uliofanya wananchi kulalamika alipokwenda kutoa sadaka kanisani. Lakini ninaamini pole pole we are getting there, next time huyu atazungumzia viongozi aliowahi kuwapa hela, ndiyo itakuwa siku ya siku! Lakini Rostam with all this bado ni fisadi tu!