Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Hebu tuangalie upande mwingine kidogo:
i) Mtikila ni muhuni, ni bahati bahati mbaya kwamba uhuni wake haujulikani kwa watu wengi. Nakumbuka mwaka jana (naomba wenzangu tuliokuwa wote wanisamehe kwa kuleta hii habari hapa) tulikuwa tunataka kufungua kesi fulani kuhusu tume ya uchaguzi ikihusisha vyama vya upinzani na tukaamua kumshirikisha Mtikila. Tulipompa hili wazo alijichodai cha kwanza ni kwamba apewe sh. mi.10 (milioni kumi) ndipo atakubali kushiriki kwenye hiyo kesi. Tukaachana naye kwa sababu alitaka kugeuzi hii issue kama mtaji.
Kuna ushahidi wa kutosha pia kwamba amekuwa na tabia ya kwenda kuchukua pesa kwa watu fulani wenye matatizo ya kisiasa ili asiwaseme, na kuna habari kwamba Sumaye aliwahi kumtolea nje maombi yake ya pesa na ndiyo ikawa chanzo cha yeye kumchafua Sumaye kwa madai ambayo maskini wa Mungu yalikujua kujulikana kwamba hayakuwa na ukweli wowote, na guess what? Waliomtumia kumchafua Sumaye ni hawa akina Rostam na JK. Mimi binafsi nashukuru sana hii incidence ya Rostam kanisani imejitokeza na na inasaidia kumjua Mtikila vizuri zaidi. Ukweli ni kwamba kwa tukio hili, hata apayuke au watu wamtetee namna gani, Mtikila will never be the same; Shetani kaamua kuonyesha uchafuka wake na amechafuka hasa na sioni sabuni ya kumsafisha tena hata kama atatumia magadi!
ii) Rostam: Hajawahi kuwa mtumishi wa serikali kwa maana ya uwaziri, katibu mkuu, n.k. Kwa hiyo, technically, Rostam hajawahi kushiriki kufanya maamuzi yeyote yenye tija au athari kwa serikali. Basis ya madai ya ufisadi wa Rostam ni makampuni yake kupata tenda za serikali kwa njia ya kitapeli.
Ok, hebu tukubaliane kwa muda kwamba Rostam kajitajirisha kwa tenda za kitapeli alizozipata serikalini, swali langu linakuja, kwa nini tumlaumu yeye? Hiyo tenda alijipa au alipewa? Hizo kanuni za tenda ni yeye ndiye aliyetunga? Kwa hiyo ukichunguza kwa makini utagundua kwamba tunarusha silaha zetu kwa mtu mwingine na tunamwacha adui. Ningekuwa kwenye kamati ya Mwakyembe ningechambua kwa makini nyaraka zilizompatia tenda Rostam, kisha, kama ningegundua loop hole katika tenda, ninge-deal na hao waliotengeneza hizo tender documents na kujua kwa hakika kulikuwa na motive gani behind it. Lakini so far hatuskii hao watumishi wa serikali wakishughulishwa kwa kuingiza nchi hasara iliyotokana na uzembe, ulafi au ujinga wao katika maswala ya tenda ya Richmond na Dowans. Kwa maneno mengine kuna watu serikali wanapata easy ride na ndio maana hawawi makini na kazi zao.
In other words, kwa mara ya kwanza katika mapambano ya rushwa, mtoa rushwa (Rostam) ndiye anaonekana mbaya zaidi kuliko mpokeajii rushwa, which is, to me, a bit strange.
So, yes Rostam kashiriki kutuingiza hasara kwa tenda za kitapeli. Lakini tusisahau alichofanya Rostam ni kutumia ulafi, ujinga, uzembe na kutokujali kwa watu wetu serikalini. Mfanyabiashara yeyote atatumia loop holes za kumpa faida. Si kazi ya mfanyabiashara kuziba mianya ya rushwa na ufisadi katika serikali; hiyo ni kazi ya serikali! CCM walipoamua kukumbatia wafanyabiashara badala ya traditional followers-wakulima na wafanya kazi-walikuwa wanatengeneza the untouchables, akina Rostam. Kwa hiyo tunapomlaumu Rostam leo kwa kutajirika kifisadi utaona kwamba inasaidia nyoyo zetu kujifurahisha na kujiridhisha kwa kuwa tunapata mtu wa kutolea hasira zetu.
Kwa maana ingine, tunachokifanya hapa ni kukiri kwamba CCM hatuwawezi, wapo juu sana ya uwezo wetu wa kupambana nao; inabidi tutafute kibonde wa kumuonea, akina Rostam. Hii ni njia ya kawaida kisaikolojia inayotumiwa na wanyonge katika kujiridhisha (consolation), lakini ni njia ambayo kwa hakika haisaidi kutatua tatizo walilonalo. Kwa maana ingine, so long as tumeamua kuwalenga vibonde wetu, akina Rostam, kwa kuwa tumegundua kuwa haya majamaa ya CCM-JK na wenzake, hatuyawezi, tutaendelea kujifurahisha kwa kuwazomea akina Rostam na akina Mkapa (waliokwisha toka madarakani) lakini tutaendelea kubaki na ufisadi wetu. Of course it hurts, it really does!