Rostam Aziz, Watanzania tukueleweje? Unawauzia Wakenya Gesi yako Bei Chee na kwa Watanzania unatuuzia Bei Juu?

Rostam Aziz, Watanzania tukueleweje? Unawauzia Wakenya Gesi yako Bei Chee na kwa Watanzania unatuuzia Bei Juu?

Shida sio Rostam Azizi, shida ni viongozi wetu. Ruto anatarajia kutangaza hayo kutokana na kusamehe kodi kibao kwenye gesi. Je hapa kwetu ili gesi imfikie mtumiaji inakuwa imetozwa kodi kiasi gani?
ukistajabu ya gesi utashangaa ya mbolea kuwekwa mchanga ili wapge dili.hii ndo bongo bwana kila mtu anakula chake mapema tu
 
Tanzania ni shamba la bibi mkuu.

Ile fursa ya utajiri iliyokuwepo awamu ya pili ikajirudia tena awamu ya nne sasa imekuja tena awamu ya sita.

Watu wanapiga hela tu mkuu.
Rostam alipiga hela kibao wakati wa kashfa ya EPA na hakuna aliyemgusa ! Msisahau kuwa enzi ya Kikwete alikuwa mweka hazina wa ccm na upigaji ulishamiri; awamu hii he is taking advantage of the leadership na ndio maana anaongozana nao kuingia mikataba ya biashara in their presence huku hawaelewi uwepo wao kwenye kutia sign hiyo mikataba huko nje maana yake serikali inadhamini makubaliano hayo hivyo kubebesha nchi mzigo unknowingly in the event of a default!
Hilo bomba la gesi linalotakiwa kujengwa kutoka kusini mwa Tanzania mpaka Mombasa litabeba gesi ya kuagiza nje au ya Tanzania? Kama ni ya Tanzania why not satisfy local demand before exporting it to Kenya?
 
Tunamengi ya kujifunza kutoka kwa majirani zetu maana wasomi wetu bado hawajaamua kutumia elimu zao kuliendeleza taifa letu
 
Kamanda isome hii:

Mtungi wa gesi kg 13 huko Kenya huuzwa kwa Ksh 403 sawa na shilingi za kitanzania 7366
Mtungi wa gesi Kg 14.5 Tanzania huuzwa shilingi za kitanzania Tsh 55,000 sawa na Ksh3012

Tofauti
Kenya mtungi wa kg 13 ni shilingi za kitanzania Tsh 7316
Tanzania mtungi wa kg 14.5 shilingi za kitanzania Tsh 55,000

Swali: Kenya wanachota gesi baharini?

Cc Erythrocyte
 
"Kuanzia Mwezi wa Tano nategemea Kutangaza Kuuzwa kwa Gesi zote nchini Kenya kwa Tsh 500/ ya Kenya ( kama Tsh 9,500/ hadi Tsh 10,000/ tu za Tanzania ) kwani tayari Rafiki yetu kutoka Tanzania Rostam ameshakuja Kuwekeza hapa Kwetu hivyo nataka Wakenya wafurahie Maisha na wapate Gesi kwa gharama ndogo" amesema Rais William Ruto wa Kenya Juzi.

Chanzo Taarifa: Nipashe Radio One

Tunajitahidi mno Kumsahau Jemedari na Mtetezi wa Watanzania Hayati Rais Dkt. Magufuli ila tunashindwa kutokana na Kutuumiza hivi Watanzania wakati huko nje mnawafanyie Wema na Kuwaonea Huruma.

Laleni salama huko mliko Viongozi wangu Wapendwa na mlioifanyia Mema Tanzania yetu hii Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

GENTAMYCINE huwa siishii tu Kuwakumbukeni huku nikiionea Huruma Tanzania yangu na inakokwenda bali huwa Nalia mno nikiona Watanzania tunafanywa Wapumbavu ( Mapopoma ) na Watanzania wachache waliojipa Hatimiliki yote ya Mama Tanzania na Familia zao.

Endeleeni tu ila haya yote yana mwisho.

Gharama za uendeshaji Kenya zonalingana na Tanzania? Profit margins zinalingana? Ujue mtaji hauna mipaka, na siku zote utaenda kule kwenye faida zaidi.
 
KUNA ILE KITU WANASEMA KULINDA VIWANDA VYA NDANI (SEKTA ZA NDANI).....KWAKUWA GESI TUNAZALISHA WENYEWE BASI KUAGIZA YA NJE UMATOZWA KODI KUBWA ILI KULINDA VYANDANI.....GESI YA ROSTAM NIYA NJE BEI CHEE HASA UKIZINGATIA URUSI SOKO LAKE LA ULAYA NA AMERICA LIMESHUKA KUTOKANA NA VIKWAZO BASI AFRICA TUNAUZIWA TU KWA Bei RAHISI........BEI YA GESI KWETU INATOKANA NA GHARAMA ZA UZALISHAJI NA KODI KIUJUMLA NA SIDHANI KAMA TUNAAGIZA ZAIDI YA KUWAUZIA LABDA WA NJE.KWASASA GESI YA URUSI IPO CHINI IYO NI FURSA KWA WAUZAJI KUJICHOTEA ILA KUIINGIZA TZ JIANDAE KWA KOSI KUBWA HII NI KAMA ILE YA VITENGE TOKA NJE MFANO WAKE.
 
"Kuanzia Mwezi wa Tano nategemea Kutangaza Kuuzwa kwa Gesi zote nchini Kenya kwa Tsh 500/ ya Kenya ( kama Tsh 9,500/ hadi Tsh 10,000/ tu za Tanzania ) kwani tayari Rafiki yetu kutoka Tanzania Rostam ameshakuja Kuwekeza hapa Kwetu hivyo nataka Wakenya wafurahie Maisha na wapate Gesi kwa gharama ndogo" amesema Rais William Ruto wa Kenya Juzi.

Chanzo Taarifa: Nipashe Radio One

Tunajitahidi mno Kumsahau Jemedari na Mtetezi wa Watanzania Hayati Rais Dkt. Magufuli ila tunashindwa kutokana na Kutuumiza hivi Watanzania wakati huko nje mnawafanyie Wema na Kuwaonea Huruma.

Laleni salama huko mliko Viongozi wangu Wapendwa na mlioifanyia Mema Tanzania yetu hii Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

GENTAMYCINE huwa siishii tu Kuwakumbukeni huku nikiionea Huruma Tanzania yangu na inakokwenda bali huwa Nalia mno nikiona Watanzania tunafanywa Wapumbavu ( Mapopoma ) na Watanzania wachache waliojipa Hatimiliki yote ya Mama Tanzania na Familia zao.

Endeleeni tu ila haya yote yana mwisho.
Hakika kila lenye mwanzo lina mwisho wake !!
 
Kama linchi lenu limejaa makodi kibaaao ya ajabu ajabu kwanini asikimbilie Kenya ambako anasamehewa kila kitu na anauza kwa bei chee na faida anapata? Tusijitoe ufahamu nchi iko muhimbili tena ICU, yule kijana wa Nala Bw.Fernandes naye kapeleka makao makuu ya kampuni yake kenya kisa milolongo kibaaao mara tiisiiaraei mara sijui takataka gani mara wamuombe rushwa , hatuwezi kuendelea kwa staili hii, wenye akili hawawekezi Tanzania.
 
Back
Top Bottom