Rostam: Hakuna nchi duniani inajenga Uchumi wake kwa kutegemea wawekezaji wa nje, ataka wazawa wapewe kipaombele

Rostam: Hakuna nchi duniani inajenga Uchumi wake kwa kutegemea wawekezaji wa nje, ataka wazawa wapewe kipaombele

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
Nakubalina na Rostam Aziz, Wawekezaji wa Nje waje ku compliment pale ambapo Wawekezaji wa Ndani wamekwama tena Kwa Ubia.

Sasa taasisi zetu zikisia uwekezaji wao wanaweza Wazungu na hata Sasa wako busy kutafuna posho Kwa visingizio vya kuandaa majukwaa ya uwekezaji na mataifa ya Nje.

Wanapishana angani Nchi na Nchi eti kutafuta wawekezaji. Mbona hatujawahi waona Mikoani wakihamasisha huo uwekezaji Kwa wazawa? Au nyie mtuambie ni lini Investment promotion agencies za Nchi zingine Huwa zinakuja Tanzania eti kutafuta wawekezaji?

Hii mentality ya kijinga ikomeshwe mara Moja,ni lazima Serikali ijielekeze kuwezesha wazawa Kwa namna yeyote Ile.Mfani nimeona Tarura wameanzisha Samia infrastructure Bond kusaidia Wakandarasi.Taasisi zingine wanafanya nini?

Hongera bwana Rostam Kwa kuwapa shule Hawa watu wetu wasiojielewa.👇👇


View: https://youtu.be/fzFNcqqzYrw?si=WTtRcYkKL2o8DU6p

----
Mfanyabiashara na mwekezaji, Rostam Aziz amesema kuna umuhimu wa kuwakumbatia wawekezaji wa ndani katika utekelezaji wa miradi ya ndani ili kujenga uchumi wa nchi.

Rostam ameyasema hayo leo Alhamisi, Desemba 5, 2024 kwenye mjadala ulioandaliwa na Clouds Media Group unaoongelea namna Serikali imefanya uwezeshaji kwa wawekezaji wazawa. Amesema mwekezaji kutoka nje anachoangalia ni biashara na faida ya haraka kisha aangalie fursa iliyoko nchi nyingine.

“Mfanyabiashara kutoka nje akija anafanya shughuli iliyomleta kwa kutazama faida, anakuja na watu wake anaowaamini kuwapa ajira na faida atakayoipata atawekeza huko alikotoka au sehemu anayotaka kwenda kuwekeza,” amesema Rostam.

Ameshauri kwamba miradi mikubwa ya nchi kama ujenzi wa barabara, madaraja na miundombinu mbalimbali wapewe wazawa waitekeleze ili kuzungusha pesa ndani ya nchi ambapo biashara zitazaana.

Amesisitiza hakuna nchi dunani iliyojenga uchumi wake kwa kutegemea wawekezaji kutoka nje kwakuwa wawekezaji kutoka nje wanachoangalia ni masilahi yake hadi anakuja nchini lazima ahakikishe faida yake inakua kubwa na siku akimaliza anaondoka.

“Serikali ijiwekeze katika kupendelea wawekezaji wa ndani ndio wawe na matumizi makubwa wa pesa za Serikali za miradi kwasababu ikibaki nchini watanzania wengi watanufaika. Kodi zitalipwa biashara zitazunguka,” amesema Rostam.



View: https://www.instagram.com/reel/DDMK6Asqp20/?igsh=MnFmdDYzZmN0ZWp3

Chanzo: Mwananchi
 
Wewe kama kipele hueleweki, kutwa unaleta porojo la wawekezaji kuongezeka na kukuza uchumi. Hapa tena unakubaliana na rostam uchumi haukuzwi na watu kutoka nje

Wewe ni kama baamedi, unaangalia meza yenye bia nyingi
Wawekezaji ni wa muhimu lakini wanatakiwa ku compliment na sio kushika Kila kitu
 
Wazawa wana uwezo? Wana capacity ya ku deliver or wapewe tu sababu ni wazawa hata kama hawana capacity
Wengi wapo na uwezo, changamoto huwa inakuja kwenye malipo baada ya mkandarasi mweusi kumaliza kazi yake.. ( huwa wanazungushwa sana na serikali, inafika hatua mkandarasi anatoa rushwa ili alipwe stahiki zake)
 
Wengi wapo na uwezo, changamoto huwa inakuja kwenye malipo baada ya mkandarasi mweusi kumaliza kazi yake.. ( huwa wanazungushwa sana na serikali, inafika hatua mkandarasi anatoa rushwa ili alipwe stahiki zake)
Na wa nje wakija wanaongezewa na hela juu ili awakatie na chao hao fisi
Sasa unakuta amepewa hela nyingi sana mpaka vifaa vyake vyote alivyofanyia kazi anaamua kuchimba shimo kubwa na kuyazika yote
Kwani amepewa hela nyingi mpaka malori na graders anaona ni uchafu ayapeleke wapi maana hata kuyauza hana mda
 
Back
Top Bottom