Rostam: Hakuna nchi duniani inajenga Uchumi wake kwa kutegemea wawekezaji wa nje, ataka wazawa wapewe kipaombele

Rostam: Hakuna nchi duniani inajenga Uchumi wake kwa kutegemea wawekezaji wa nje, ataka wazawa wapewe kipaombele

Serikali lazima iwabebe wazawa hasa wafanyabiashara wa kati kwa mfumo wa upendeleo ulio wazi wa kodi na kuwapunguzia vikwazo na masharti ya biashara.
Ni sawa kabisa? But wanaweza deliver katika capacity ya juu? Au wabebwe tu?
 
Sana Mkuu, na inaumiza sana
Wapo wanaoweza kufanya mengi ila hawapati kisa ngozi
Kuna ubaguzi wa sisi kwa sisi
. Kuna jamaa alifirisika kabisa kisa serikali, walimpa tenda ya kurebisha barabara Vijijini, kama km400 hivi, dahh walimzungusha balaa mpaka akata tamaa kufuatilia zile pesa....

. Sasa hivi ndo anapambana na mishe nyingine ili kuimarisha uchumi wake..
 
Rostam Aziz sio mzawa wa Tanzania, lakini kuna taarifa kwamba anahusishwa na kabila la Baluchi, ambalo lina asili kutoka eneo la Baluchistan, linalopatikana katika nchi za Iran, Pakistan, na Afghanistan.
Kuna Wabaluchi wazawa wa Tanzania halafu pia kuna Wasukuma, Wanyirimba n.k weusi kama chungu ambao ni wazawa wa Wamarekani lakini sio Watanzania.
 
Suala la kuzungushwa ni wakandarasi wote si weusi tu. Sote tunajua gov payment zinavyo chukua muda , wengine inawapelekew kutoa percent fulani ili malipo yao yafuatiliwe
Sasa kwa nini zichukue mda mrefu 🤔🤔, Gvt inavyotoa tenda si huwa budget imetengwa Tayari au ikoje hii??
 
. Kuna jamaa alifirisika kabisa kisa serikali, walimpa tenda ya kurebisha barabara Vijijini, kama km400 hivi, dahh walimzungusha balaa mpaka akata tamaa kufuatilia zile pesa....

. Sasa hivi ndo anapambana na mishe nyingine ili kuimarisha uchumi wake..
Wana laana hawa
Kuna mda nilikuwa kwenye site moja huko akaja mkuu kiongozi mwanamke kavaa high heels 👠 angonga gonga kiatu chini na kusema hii iko chini ya kiwango hajui lolote kuhusu ujenzi na akasitisha mradi
Mpaka leo haujaendelezwa na akamlisha hasara jamaa
Yaani kuna visa vingi sana huko
 
. Bila shaka hapo atakuwa alinyimywa posho/rushwa..🚮🚮

Tunapenda sana kurudishana nyuma sisi wenyewe kwa wenyewe, Ndo maana kila mtu akiingia serikalini/kitengo anaenda kulipiza kisasi kwa wizi aliofanyiwa uraiani akiwa kwenye hustle, na si kujenga nchi ya kimaendeleo
 
Hatutafika popote mkuu
 
Huyu ndiyo mzalendo halisi anayetumia digrii yake ya uchumi na uzoefu wa kufanya biashara kubwa ndani na nje ya Tanzania anayetoa uzoefu wa kufanya biashara na vikwazo kutoka mangi meza waajiriwa wa serikali ya CCM kwa miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
 
Hao Wazawa wakipewq deal wanatafuta mwekezajo kutoka nje! Ni usanii tu!

Mengi mwenyewe aliwahi kulilia kumilikishwa kiwanda kwa ngao ya uzawa alipopewa akakiuza kwa wahindi!
 
Nakubalina na Rostam Aziz, Wawekezaji wa Nje waje ku compliment pale ambapo Wawekezaji wa Ndani wamekwama tena Kwa Ubia.

Sasa taasisi zetu zikisia uwekezaji wao wanaweza Wazungu na hata Sasa wako busy kutafuna posho Kwa visingizio vya kuandaa majukwaa ya uwekezaji na mataifa ya Nje.

Wanapishana angani Nchi na Nchi eti kutafuta wawekezaji.Mbona hatujawahi waona Mikoani wakihamasisha huo uwekezaji Kwa wazawa? Au nyie mtuambie ni lini Investment promotion agencies za Nchi zingine Huwa zinakuja Tanzania eti kutafuta wawekezaji?

Hii mentality ya kijinga ikomeshwe mara Moja,ni lazima Serikali ijielekeze kuwezesha wazawa Kwa namna yeyote Ile.Mfani nimeona Tarura wameanzisha Samia infrastructure Bond kusaidia Wakandarasi.Taasisi zingine wanafanya nini?

Hongera bwana Rostam Kwa kuwapa shule Hawa watu wetu wasiojielewa.👇👇

View: https://youtu.be/fzFNcqqzYrw?si=WTtRcYkKL2o8DU6p

----
Mfanyabiashara na mwekezaji, Rostam Aziz amesema kuna umuhimu wa kuwakumbatia wawekezaji wa ndani katika utekelezaji wa miradi ya ndani ili kujenga uchumi wa nchi.

Rostam ameyasema hayo leo Alhamisi, Desemba 5, 2024 kwenye mjadala ulioandaliwa na Clouds Media Group unaoongelea namna Serikali imefanya uwezeshaji kwa wawekezaji wazawa. Amesema mwekezaji kutoka nje anachoangalia ni biashara na faida ya haraka kisha aangalie fursa iliyoko nchi nyingine.

“Mfanyabiashara kutoka nje akija anafanya shughuli iliyomleta kwa kutazama faida, anakuja na watu wake anaowaamini kuwapa ajira na faida atakayoipata atawekeza huko alikotoka au sehemu anayotaka kwenda kuwekeza,” amesema Rostam.

Ameshauri kwamba miradi mikubwa ya nchi kama ujenzi wa barabara, madaraja na miundombinu mbalimbali wapewe wazawa waitekeleze ili kuzungusha pesa ndani ya nchi ambapo biashara zitazaana.

Amesisitiza hakuna nchi dunani iliyojenga uchumi wake kwa kutegemea wawekezaji kutoka nje kwakuwa wawekezaji kutoka nje wanachoangalia ni masilahi yake hadi anakuja nchini lazima ahakikishe faida yake inakua kubwa na siku akimaliza anaondoka.

“Serikali ijiwekeze katika kupendelea wawekezaji wa ndani ndio wawe na matumizi makubwa wa pesa za Serikali za miradi kwasababu ikibaki nchini watanzania wengi watanufaika. Kodi zitalipwa biashara zitazunguka,” amesema Rostam.

Chanzo: Mwananchi

Mbona alishabikia Bandari Bandari kuuzwa kwa DP WORLD?
 
Back
Top Bottom