Hivi hii 'royal tour" ilikuwa ukarasa wa ngapi katika ilani yenye kurasa 303 ya CCM? Ama ni ingizo jipya?
KUKUZA UTALII
F. Kutengeneza ajira zisizopungua 7,000,000 (milioni saba) katika sekta
rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya vijana:-
(i) Kuchochea ukuaji wa uchumi, hususan katika sekta ya viwanda vinavyotumia malighafi za kilimo, mifugo, uvuvi, madini, maliasili na sekta ya huduma za kiuchumi pamoja na utalii;
(ii) Kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za ujasiriamali,
ikiwemo kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na taasisi na
asasi za utoaji mikopo yenye riba na masharti nafuu;
(iii) Kuwahamasisha na kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu
katika utamaduni, michezo na sanaa kwa ajili ya afya bora na
burudani na pia kuongeza fursa za ajira na kipato; na
(iv) Kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya kimkakati inaajiri
vijana wengi zaidi wa Kitanzania.
UKURASA WA 8
(xi) Kukuza sekta za huduma hususan utalii ili kutumia fursa
zilizopo kikamilifu na kuongeza mchango wake katika uchumi
wa Taifa. ( UKURASA WA 14)