Royal Tour! kulikoni wagharimiaji hawatajwi hadharani? Tunaishia kuambiwa ni Watu Binafsi

Huwakosi akina Rostam hapo likely na wale wa Loliondo gate.

Kama tuna wananchi wenye mahaba kwa nchi yao kiasi hicho,kwa nini tusiwachangishe tukalipa mapunjo na malimbikizo ya mishahara ya watumishi?

"Wakata viuno" walituambia Mama yao anaongoza nchi kwa uwazi,akikopa anasema sasa si awataje na hao jamaa tujue!

Mbona IMF na WB anawataja bila kujiuma.
 
Watanzania tumepigwa na kitu kizito.​

CCM tunaomba 2025 tuleteeni mgombea mwingine tuko tayari kuwapa kura za kishindo.​

Ukiwa ni mtu mwenye maono yanayotazama mbali utaiangalia Royal Tour miaka mitano au zaidi kuanzia leo ukiwa ni mtu wa makundi au hizi team msoga na team JPM utajikuta unajenga hoja za kishabiki.

Tazama kila mwafrika asiye na maono alivyokuwa akihoji Visit Rwanda wakati Kagame alivyoingia mkataba na Arsenal lakini leo hii kila mtu yupo kimya baada ya kuwaona Messi na Neymar wakiwa wamevaa jezi hizo hizo.

Maono ya hiyo Tour ni zaidi ya pesa zimetoka kwa nani zikaenda kwa nani, hizo huwa ni siasa tu za majibizano.
 
Ndo NCHI yetu ilivyo, wengine walipohoji matumiz ya ile 1.5trl waliishia kufukuzwa kaz 😂😂
 
Watanzania tumepigwa na kitu kizito.​

CCM tunaomba 2025 tuleteeni mgombea mwingine tuko tayari kuwapa kura za kishindo.​

Mtanyooka tu na bado yupoyupo sana na tuna mpango wa kumuongezeaa muda! Kama mlivyotaka kufanya enzi zenu. Mama atake asitake tutaaa..muongezeaaaaa!!!
 
Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?
Transparency.kila kitu lazima kiwekwe wazi kwa watz sababu wao ndo walipa kodi na wanahaki ya kuhoji pesa zao zinatumikaje.
 
Hiyo hoja yako wewe
 
kifupi ni kwamba sio kila anayesaidia anapenda kutangazwa

hata iman zetu zinasema hivyo
 
Kwani zile hela za plea bargaining mbona hamuulizi ziliendaga wapi
 
Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?
Kwa nini wewe kila likija swala mhimu na lenye tija kwa nchi,kazi yako ni kupinga tu? Kila michango yako wewe ni kutetea ufisadi na uharifu? Au wewe hiyo ndio kazi yako?, unalipwa kwa kazi hii?
 
Kilichopo kila mtu ana wazo yake Jambo ambalo ni haki ya msingi ya kibinadamu lakini je,kwakutofanya au kufanya hayo ambayo yanatokana na wazo lako binafsi ni KINYUME cha sheria ipi?
Au ndiyo kutumia fursa za uwezo wa kuandika HOJA ili ionekane kila anachofanya amekosea kwasababu hakuweza kutabiri fikra ulizonazo ambazo zilikuwa zimejificha ndani ya ubongo wako!
 
Mkuu sio hivyo tu bali hata mama kasema uongo. Huu mkakati ulianzia nyuma sana enzi ya Kigwangalla na Rostam ame play role kubwa sana kwenye hili jambo.
 
Kwa nini wewe kila likija swala mhimu na lenye tija kwa nchi,kazi yako ni kupinga tu? Kila michango yako wewe ni kutetea ufisadi na uharifu? Au wewe hiyo ndio kazi yako?, unalipwa kwa kazi hii?
Hao ndio Msoga team!
 
Transparency.kila kitu lazima kiwekwe wazi kwa watz sababu wao ndo walipa kodi na wanahaki ya kuhoji pesa zao zinatumikaje.
Ukweli ndio huo.
 
Hapa mimi ni mlipa kodi wa nchi hii pia.
Nina haki ya kujua matumizi sahihi ya kodi yangu ninayolipa.
Watanzania wanahitaji serikali iliyo wazi kwenye matumizi yake.
Wewe kama hujui na huna uwezo wa kuhoji au ni mmoja wa wanufaika wa wizi wa raslimali zetu.
Kaa kimya wenye kuhoji ni haki yetu.
 
Hatuongelei umuhimu wa Royal Tour na faida zake huko mbeleni.
Tunachotaka ni uwazi wa serikali kwenye matumizi yake.
Pia ieleweke kwamba endapo kutakuwa na kashfa yoyote kuihusu serikali kwenye suala la utengenezaji wa makala hii.

Inaleta madhara zaidi kuliko faida.
Wazungu huwa hawataki kashfa.
Sisi wananchi ndio tunaokamuliwa kila uchao kwa kodi mbalimbali na hatimae serikali kuweza kujiendesha.

Hoja ni matumizi au ufadhili kuwekwa wazi.
Unapomficha mfadhili wa 7bilion.
Ni hatari kwa usalama wa Taifa letu.
Hatujui nia na malengo yake.
 
Mkuu sio hivyo tu bali hata mama kasema uongo. Huu mkakati ulianzia nyuma sana enzi ya Kigwangalla na Rostam ame play role kubwa sana kwenye hili jambo.
Wafanyabiashara wakubwa ndio wanaotoa direction ya hii nchi kwa sasa.
 
Kama kweli waliochanga ni wadau Kwa Nini mchakato wa kuchanga ulikuwa wa Siri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…