Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Video ya Rais William Ruto akiongea na wakenya waishio ughaibuni (diaspora) siku za karibuni, imejaa kila aina ya somo jema kwa uhai wa miaka mingi wa Tanzania yetu.
Ruto kawa muwazi kwa wakenya kwamba anabariki jitihada zao za kutafuta maisha huko ughaibuni, kwamba wanachokipata huko kinapokelewa kwa mikono miwili kinaporudishwa Kenya. Huu ni mtazamo chanya wa Kenya kimataifa na Ruto sio kiongozi wa kwanza kuwa na maono ya aina hii.
Kenya ni nchi imejengwa kibepari, inaruhusu raia wa nchi yake kwenda huko nje kupambania mkate wa kila siku na kurudisha nchini mwao faida (remittance) inayopatikana. Wanatumia kila sekunde ya kujenga nchi katika kujenga raia wenye uwezo wa kushindana katika soko la ajira.
Anachowaambia raia wa Kenya ughaibuni ni ule msingi wanaoujenga miaka na miaka wa kuandaa nguvu kazi zenye kutakiwa na soko la wakati husika ndani ya muda wowote.
Naona kama TZ tunazidi kukwama linapokuja suala la utayari wa nguvu kazi yetu kupambana kimataifa, bado mpaka leo tuna mijadala ya kiswahili na kingereza eti ni ipi lugha yenye soko na itakayowapa raia wetu ile faida ya asili katika kupigania soko la kimataifa la ajira!.
Royal Tour ulikuwa ni mkakati wa kitaifa wa kukaribisha wageni waje wafanye utalii, lakini siuoni uwiano wa Royal Tour na ile jeuri kama aliyoifanya Ruto ya kuwaambia wakenya waende huko nje wakapambanie ajira kwa nia ya kuja na mrejesho chanya kiuchumi. Je kwa mikakati kama Royal Tour tunajiandaa kuwa wapokeaji wa kudumu wa wageni tusiozifahamu faida za sisi kuwa sehemu ya soko pana la ajira huko duniani?.
Watalii kuja kwao ni kuitikia ile nguvu ya matangazo ya kiserikali na binafsi kuhusu kuitangaza TZ. Lakini wanapokuwa hapa tunakuza vipi uhusiano wa kibiashara na wao ili matokeo yake yawe ni kukua kwa uchumi kusikoyumba kirahisi?.
Jina TZ na thamani yake linapanda zaidi iwapo tunakuwa na nguvu kazi isiyo na uoga kujieleza, isiyo na uoga kuaminisha watu kuwa sisi ni taifa makini. Jina TZ linapanda hadhi na viwango iwapo tunabadilika haswa hizi tabia zetu za kila siku zenye kutukwaza kimataifa.
Yapo mengi yanayoshusha thamani jitihada zIlizokula pesa nyingi za Royal Tour. Na ule muonekano mzima chanya wa wanadiplomasia waliosomeshwa kwa nguvu na fedha ili siku moja waje kufanya mengi mema kwa ajili ya TZ.