Royal Tour ni sumaku ya kisiasa Mkakati wa Kenya una changamoto chanya kwa Tanzania

Royal Tour ni sumaku ya kisiasa Mkakati wa Kenya una changamoto chanya kwa Tanzania

Basics tu zinatushinda kama nishati ni aghali bidhaa zetu bei juu finished product haiwezi kupambana na products za nje unataka tufanye biashara gani ambayo hatufanyi sasa hivi (kuwauzia nchi na kuwapa raw materials wakati sisi tunanunua finished products kutoka kwao)!!!

Ndani tu tumeshindwa kuweka mambo sawa unategemea nje tutaweza collectively...

Of course mmoja mmoja wanaweza kina Bhakresa kusupply chakula huko nje au vijana kazi zao (kina Diamond kuuza nje) hii dunia ishakuwa kijiji na mwiba wala sio wananchi bali ni fikra za viongozi.... (Short Sightedness) na shortcuts za kutafuta mwarobaini

By the way watalii hawaji kuona Serengeti sababu ya Filamu waliyoiona bali sababu its a Natural Wonder of the Earth...
 
Sasa kuna Diaspora alizuiwa kuja kuwekeza hapa Tanzania?

Kwani ukiwa Mtanzania Diaspora,huwezi kuja kufanya maendeleo yako na familia yako hapa?

Sema wazi!
kinachopiganiwa hapa ni kupata Uraia Pacha ili mkiisha beba maboksi kwa miaka mingi huko basi muambulie na Pensheni zinaoendana na Maisha yao.

Wengi wa wakenya walioko nje wanajitambua kilichowapeleka huko.
Tofauti na Watanzania ambao wameondoka wenyewe kwa hiari zao.na kufika huko mnabaki kulilia Uraia Pacha!

For your Own interests na msisingizie ooh Maendeleo ya nchi wala nini!

Tunaposema Uraia Pacha bado hatujajiandaa nao kwa sasa.
Ni kwa maslahi mapana ya kitaifa.

Ila ukiwasikiliza huko Spaces na Club houses wanalalama siasa tupu.

Ukimuuliza what have you done since ever umekaa huko!

Utaishia kuambiwa wewe na Watanzania wenzio ni waoga sana kuchukua maamuzi magumu!

Wengine ndio hao kina Lissu,ambao watoto na familia zao wana Uraia wa nje tayari.

Lakini kazi yao ku-Snitch na makampuni ya nje kisha kubaki wakituzodoa baada ya kufanikiwa kuzisaidia hizo kampuni.

Sasa hivi tu bado tuna Uraia wa nchi moja,lakini Wapinzani wa kisiasa Tanzania,wanapishana Uzunguni kuomba msaada wa kuiondoa Serikali Madarakani.

Je!
Uraia Pacha wakiupata? Itakuwaje??

Na kama mnaona Uraia wetu unazingua kwa nini msiombe wa huko mlipo na kuukana U-Bongo

Jibu ni kwamba nyingi wengi wenu sio material ambazo zinaweza pewa uraia wa huko kirahisi.

Sababu elimu pia ni ya kuungaunga!

Unless Otherwise Uolewe au Kuowa huko.
Umeandika ujinga mtupu.Akili na mawazo yako niyakijima sana.
 
Umeandika ujinga mtupu.Akili na mawazo yako niyakijima sana.
Kama kupewa uraia Pacha ndio Ujanja kwako,lazima utaniona mjinga sana!

Kama kuwabia ukweli kwamba hata nyinyi huko Ughaibuni mnaonekana wajinga,mlioenda kuponesha Matumbo yenu huko kwao kwa kukimbia njaa zenu makwenu.

Hata mkipewa uraia wao,bado mtaendelea kuonekana wa hivyo hivyo mlivyoenda!
 
Mada ni nzuri, lakini imechanganywa na mambo mengi yasiyoijengea nguvu.

Kwa mfano, sioni maana ya kuchanganya Royal Tour na Diaspora, kama mfano mmoja tu wa mkanganyiko.

Lakini ngoja niache tarakimu kidogo hapa kuunga mkono mada.

Diaspora Kenya mwaka uliopita wameingiza zaidi ya dollar za Marekani Billion 3. Hii ni hela nzuri sana ya nje, na ndiyo inayosaidia katika kushikiza thamani ya shilingi ya Kenya. Sisi diaspora yetu, hata Benki kuu huwa hawajisumbui sana kuitaja. Nadhani ni kama dollar million tano hivi kwa mwaka uliopita

Utalii, kwetu ni nafuu zaidi ya Kenya kwa kiasi cha pesa kinachoingia, nadhani itakuwa kwenye bilion moja na zaidi kwa mwaka uliopita. Tunawazidi Kenya, lakini siyo sana. Lakini kutokana na vivutio tulivyonavyo, tungekuwa mbali zaidi ya majirani zetu wote.

But all in all, Tanzania tunashindwa tu sisi wenyewe kutumia fursa nyingi tulizojaliwa hapahapa nyumbani hata bila ya kukimbilia huko nje. Badala yake, sasa tunatapanya tu bila ya mpangilio wowote.

Niondoke na swali: Hivi diaspora wa Kenya waliopo hapa Tanzania wanapeleka kiasi gani kwao? Nasikia tu kwamba kiasi hicho kilikuwa kinono kuliko walichopata toka Afrika Kusini, nchi ambayo huwa kinara kwao katika bara la Afrika.
Nitazungumzia tu sehemu moja ya mada yako nzuri - "Tanzania tunashindwa sisi wenyewe kutumia fursa nyingi ....". Fursa hizi zilizopo zinahitaji zaidi financial resources kuliko "kuzitambua" tu. Mifumo kadhaa ya kibenki haiwezi hata kutoa financing ya fursa ambayo haijaanza kutoa kipato. Wao wanapima kipato kilichopo ili kufanya financing - sio watu wa kuanzisha jambo jipya. Ni watu binafsi ndio wanaweza kuzitambua fursa na kuwekeza wakitamani mambo yatafanikiwa. Watu hao ni wakina nani? Hawa hawa ambao wana mashamba ya mazao yaliyo na bei ndogo? Ni hawa wafanyakazi wanaolipwa mishahara inayotosha kujikimu? Hapa ndipo linapokuja swala na diaspora - wale walioenda na kufanikiwa lakini wanataka kuwekeza pesa zao eneo lenye fursa!! Pale wanaita nyumbani!! Na ndio hawa tunawakwamisha kwa kusema hatutaki raia pacha!! Tunafanya remittances ziwe ni zile zinazoendesha maisha ya wapendwa wao - chakula, mavazi, malazi, karo za shule nk. (maeneo ambayo sio fursa). Lakini hawawezi kuanzisha kilimo au kufanya uwekezaji wowote kwa hofu kuwa vitu hivo vitapotezwa au kutokana na wao kutokuwa raia au na ndugu na marafiki zao kupitia mismanagement. Badala ya kuwaona diaspora kwa jicho la ubaya, tungejiuliza hatari ambazo wameleta kwa nchi zinazokubali uraia pacha!! Moja ya njia za kisasa za kuangalia jambo ni "mahitaji ya wakati" na sio "hasara za kuwa na jambo hilo". Tuangalie mahitaji na kisha hasara. Tumefanya hivo mara nyingi - tunakopa kwa sababu tuna mahitaji, hasara za kukopa tunazivumilia baadae. Kwanini approach hii haitumiki kwa diaspora???
 
Watanzania kushindwa kufaidika na diaspora chanzo haswa nadhani ni ule mtazamo hasi unaoanzia juu kabisa kwa viongozi wa kiserikali.

Kwamba kinachotoka nje kuja ndani ni lazima kitiliwe shaka pasipo hata kukitazama kwa kina kwa maana ya faida zake kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa zima kwa ujumla.

Tuna ile mitazamo kuwa wa nje wanakuja kutuibia, wanakuja kututapeli, kwamba hawawezi wakawa na nia njema za wazi kwa jamii yetu kwa mapana yake.

Kenya wameshavuka hatua hizi za kujiona wanyonge pale wanapoongelea taifa lao kama sehemu pana ya dunia. Tunakuwa na mitazamo ya kujihami na madhara yake ni kutofaidika kiukamilifu na ushirikiano mpana wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom