Royal Tour ni sumaku ya kisiasa Mkakati wa Kenya una changamoto chanya kwa Tanzania

Basics tu zinatushinda kama nishati ni aghali bidhaa zetu bei juu finished product haiwezi kupambana na products za nje unataka tufanye biashara gani ambayo hatufanyi sasa hivi (kuwauzia nchi na kuwapa raw materials wakati sisi tunanunua finished products kutoka kwao)!!!

Ndani tu tumeshindwa kuweka mambo sawa unategemea nje tutaweza collectively...

Of course mmoja mmoja wanaweza kina Bhakresa kusupply chakula huko nje au vijana kazi zao (kina Diamond kuuza nje) hii dunia ishakuwa kijiji na mwiba wala sio wananchi bali ni fikra za viongozi.... (Short Sightedness) na shortcuts za kutafuta mwarobaini

By the way watalii hawaji kuona Serengeti sababu ya Filamu waliyoiona bali sababu its a Natural Wonder of the Earth...
 
Umeandika ujinga mtupu.Akili na mawazo yako niyakijima sana.
 
Umeandika ujinga mtupu.Akili na mawazo yako niyakijima sana.
Kama kupewa uraia Pacha ndio Ujanja kwako,lazima utaniona mjinga sana!

Kama kuwabia ukweli kwamba hata nyinyi huko Ughaibuni mnaonekana wajinga,mlioenda kuponesha Matumbo yenu huko kwao kwa kukimbia njaa zenu makwenu.

Hata mkipewa uraia wao,bado mtaendelea kuonekana wa hivyo hivyo mlivyoenda!
 
Nitazungumzia tu sehemu moja ya mada yako nzuri - "Tanzania tunashindwa sisi wenyewe kutumia fursa nyingi ....". Fursa hizi zilizopo zinahitaji zaidi financial resources kuliko "kuzitambua" tu. Mifumo kadhaa ya kibenki haiwezi hata kutoa financing ya fursa ambayo haijaanza kutoa kipato. Wao wanapima kipato kilichopo ili kufanya financing - sio watu wa kuanzisha jambo jipya. Ni watu binafsi ndio wanaweza kuzitambua fursa na kuwekeza wakitamani mambo yatafanikiwa. Watu hao ni wakina nani? Hawa hawa ambao wana mashamba ya mazao yaliyo na bei ndogo? Ni hawa wafanyakazi wanaolipwa mishahara inayotosha kujikimu? Hapa ndipo linapokuja swala na diaspora - wale walioenda na kufanikiwa lakini wanataka kuwekeza pesa zao eneo lenye fursa!! Pale wanaita nyumbani!! Na ndio hawa tunawakwamisha kwa kusema hatutaki raia pacha!! Tunafanya remittances ziwe ni zile zinazoendesha maisha ya wapendwa wao - chakula, mavazi, malazi, karo za shule nk. (maeneo ambayo sio fursa). Lakini hawawezi kuanzisha kilimo au kufanya uwekezaji wowote kwa hofu kuwa vitu hivo vitapotezwa au kutokana na wao kutokuwa raia au na ndugu na marafiki zao kupitia mismanagement. Badala ya kuwaona diaspora kwa jicho la ubaya, tungejiuliza hatari ambazo wameleta kwa nchi zinazokubali uraia pacha!! Moja ya njia za kisasa za kuangalia jambo ni "mahitaji ya wakati" na sio "hasara za kuwa na jambo hilo". Tuangalie mahitaji na kisha hasara. Tumefanya hivo mara nyingi - tunakopa kwa sababu tuna mahitaji, hasara za kukopa tunazivumilia baadae. Kwanini approach hii haitumiki kwa diaspora???
 
Watanzania kushindwa kufaidika na diaspora chanzo haswa nadhani ni ule mtazamo hasi unaoanzia juu kabisa kwa viongozi wa kiserikali.

Kwamba kinachotoka nje kuja ndani ni lazima kitiliwe shaka pasipo hata kukitazama kwa kina kwa maana ya faida zake kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa zima kwa ujumla.

Tuna ile mitazamo kuwa wa nje wanakuja kutuibia, wanakuja kututapeli, kwamba hawawezi wakawa na nia njema za wazi kwa jamii yetu kwa mapana yake.

Kenya wameshavuka hatua hizi za kujiona wanyonge pale wanapoongelea taifa lao kama sehemu pana ya dunia. Tunakuwa na mitazamo ya kujihami na madhara yake ni kutofaidika kiukamilifu na ushirikiano mpana wa kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…