Royal Tour: Rais Samia aeleza Watanzania faida ya kutangaza utalii kimataifa

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
652
Reaction score
442
Leo Alhamisi Septemba 02, 2021 Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa eneo la Tegeta Jijini Dar es Salaam amewaeleza Watanzania faida ya kipindi cha filamu maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa kwenye eneo la vivutio vya utalii, maeneo ya uwekezaji, sanaa na utamaduni wa watu wa Tanzania ambayo anaiigiza maeneo mbalimbali ya vivutio Tanzania akiwa kama Mhusika Mkuu.

Rais Samia amesema filamu hiyo ina lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa na itazinduliwa Marekani na kuonyeshwa ulimwengu mzima. Filamu hiyo itakapotoka itasaidia:-

1️⃣ Kuleta Wawekezaji na Watalii wengi zaidi Tanzania na itaonyesha ulimwengu Tanzania ni kina nani na siasa zetu na maisha yetu yakoje na tunajiendeshaje.

2️⃣ Pia filamu hii itasaidia kuweka ukweli na kuondoa uongo unaoenezwa na Watanzania wenzetu nje ya nje (kama ule uongo wa akina Lissu na wenzake) na kuwamimina zaidi Wawekezaji, Watalii, Wafanyabiashara kuja nchini kufanya biashara, utalii na uwekezaji.

Tayari Rais Samia ameanza kurekodi filamu hiyo katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar na sasa anaendelea na Bagamoyo.

Bwanku M Bwanku.

msemajimkuuwaserikali~p~CTUIP2gKy0v~1.jpg
 
Ngoja tusubiri tuone! Inawezekana hamuamini Mwanamke mwenzake aliyemteua kwenye ile Wizara ya Mambo ya nje!
 
Ndio inafaida kubwa Sana Kama Rwanda

USSR
 
Mtalii gani atakuja katika country ambayo watu hawataki chanjo, kuna magaidi na hakuna democracy
 
Movie star Mh. Rais wa Tanzania....!!

Ngoja tuone kama kweli itaongeza watalii na wawekezaji. Wasiache tu kutupa marejesho.
 
Na hii COVID-19 ni mtalii gani anayetaka kuja kwenye nchi ambayo inaficha idadi ya maambukzi ya ugonjwa huo ya kila siku? Hiyo Royal Tour ni kampun ya nani? imesajiliwa nchi gani na imelipwa kiasi gani cha pesa? Pesa hizi zimeidhinishwa na Bunge?

Leo Alhamisi Septemba 02, 2021 Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa eneo la Tegeta Jijini Dar es Salaam amewaeleza Watanzania faida ya kipindi cha filamu maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa kwenye eneo la vivutio vya utalii, maeneo ya uwekezaji, sanaa na utamaduni wa watu wa Tanzania ambayo anaiigiza maeneo mbalimbali ya vivutio Tanzania akiwa kama Mhusika Mkuu.

Rais Samia amesema filamu hiyo ina lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa na itazinduliwa Marekani na kuonyeshwa ulimwengu mzima. Filamu hiyo itakapotoka itasaidia:-

1️⃣ Kuleta Wawekezaji na Watalii wengi zaidi Tanzania na itaonyesha ulimwengu Tanzania ni kina nani na siasa zetu na maisha yetu yakoje na tunajiendeshaje.

2️⃣ Pia filamu hii itasaidia kuweka ukweli na kuondoa uongo unaoenezwa na Watanzania wenzetu nje ya nje (kama ule uongo wa akina Lissu na wenzake) na kuwamimina zaidi Wawekezaji, Watalii, Wafanyabiashara kuja nchini kufanya biashara, utalii na uwekezaji.

Tayari Rais Samia ameanza kurekodi filamu hiyo katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar na sasa anaendelea na Bagamoyo.

Bwanku M Bwanku.

View attachment 1921326
 
Habari wadau..!
Naomba tujadili kichwa cha habari hapo juu kuhusu hii "The Royal Tour" ndio nini??

Kwa nini rais ahache majukumu mengine ya msingi afanye hii kitu ambayo ingeweza fanywa hata na ma miss utaliii???.

Kwa nini tusiende kwa PK kuiba maujuzi ya kutangaza utalii maana naona kama PK yeye amefanikiwa sana katika kutangaza utalii.

Je huu ushauri nani alimpatia rais wetu??Kiukweli binafsi sielewi kitu chochote na natumia haki yangu ya kikatiba kuhoji,na kuomba kuelimishwa.

Wajuzi naomba mjibu kwa hoja.
 
hivi unafkiri kila mtu anajua PK nini. Mwingine atasema PaKa.
Wachache tunajua nn unamaanisha.
Andikeni vitu vinavyoeleweka
 
Hiyo kazi ingefanywa vizuri zaidi na Diaspora wa kitanzania au hata TBC, Vinginevyo kuna kundi la wapambe pembeni wanaonufaika na usanii huu.
 
Msisahau kutangaza na hifadhi ya Ruaha kwenye hiyo "Royal Tour yenu".
 
Tulitaka kutangaza utalii...rais kalivaa mazima....tunazingua tena.... mh
 
Leo Alhamisi Septemba 02, 2021 Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa eneo la Tegeta Jijini Dar es Salaam amewaeleza Watanzania faida ya kipindi cha filamu maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa kwenye eneo la vivutio vya utalii, maeneo ya uwekezaji, sanaa na utamaduni wa watu wa Tanzania ambayo anaiigiza maeneo mbalimbali ya vivutio Tanzania akiwa kama Mhusika Mkuu.

Rais Samia amesema filamu hiyo ina lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa na itazinduliwa Marekani na kuonyeshwa ulimwengu mzima. Filamu hiyo itakapotoka itasaidia:-

1️⃣ Kuleta Wawekezaji na Watalii wengi zaidi Tanzania na itaonyesha ulimwengu Tanzania ni kina nani na siasa zetu na maisha yetu yakoje na tunajiendeshaje.

2️⃣ Pia filamu hii itasaidia kuweka ukweli na kuondoa uongo unaoenezwa na Watanzania wenzetu nje ya nje (kama ule uongo wa akina Lissu na wenzake) na kuwamimina zaidi Wawekezaji, Watalii, Wafanyabiashara kuja nchini kufanya biashara, utalii na uwekezaji.

Tayari Rais Samia ameanza kurekodi filamu hiyo katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar na sasa anaendelea na Bagamoyo.

Bwanku M Bwanku.

View attachment 1921326
Hii ni television programme ambayo inalenga mahususi viongozi wa nchi kutambulisha nchi yao. Si ya Tanzania peke yake. Maelezo zaidi utayapata hapa:

Amandla...
 
Raisi itakuwa keshakatiwa chake ,hawa wasanii wa bongo movie wakifanya igizo wanachukue hela ndefu kiasi ,sa unafikiri Raisi kakubali kwa kiasi gani,nahisi sio bure aingie tu kwenye igizo bure bure ,mbona inatoka akilini badala ya kuingia.
 
Back
Top Bottom