Leo Alhamisi Septemba 02, 2021 Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa eneo la Tegeta Jijini Dar es Salaam amewaeleza Watanzania faida ya kipindi cha filamu maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa kwenye eneo la vivutio vya utalii, maeneo ya uwekezaji, sanaa na utamaduni wa watu wa Tanzania ambayo anaiigiza maeneo mbalimbali ya vivutio Tanzania akiwa kama Mhusika Mkuu.
Rais Samia amesema filamu hiyo ina lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa na itazinduliwa Marekani na kuonyeshwa ulimwengu mzima. Filamu hiyo itakapotoka itasaidia:-
1️⃣ Kuleta Wawekezaji na Watalii wengi zaidi Tanzania na itaonyesha ulimwengu Tanzania ni kina nani na siasa zetu na maisha yetu yakoje na tunajiendeshaje.
2️⃣ Pia filamu hii itasaidia kuweka ukweli na kuondoa uongo unaoenezwa na Watanzania wenzetu nje ya nje (kama ule uongo wa akina Lissu na wenzake) na kuwamimina zaidi Wawekezaji, Watalii, Wafanyabiashara kuja nchini kufanya biashara, utalii na uwekezaji.
Tayari Rais Samia ameanza kurekodi filamu hiyo katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar na sasa anaendelea na Bagamoyo.
Bwanku M Bwanku.