Royal Tour yajibu! Ndani ya miezi 11 tu watalii waliotembelea Tanzania wafikia milioni 1.2

Royal Tour yajibu! Ndani ya miezi 11 tu watalii waliotembelea Tanzania wafikia milioni 1.2

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
Hongera na kazi wadau.

Nitumie fursa hii kueleza habari njema za Royal Tour.

Idadi ya Watalii Waliotembelea Tanzania kwa miezi 11 ya mwaka 2022 wamefikia Milioni Moja na Laki mbili(1,200,000).

Hizi Ni habari njema zikizoletwa na Royal tour na bila shaka Hadi Mwisho wa mwezi wa 12 Idadi ya Watalii itavuka 1.3Mil.

Bila Shaka huko tuendako Mambo yanaweza kuwa mazuri ikizingatia Tanzania umeweka lengo la kufikia Idadi ya Watalii mil.5 mwaka 2025.

Hongera zenu Ila bado sana kuwafikia Egypt, Morocco, South Africa nk.👇

 
Utalii hauko hivyo acheni ujinga nyie, marketing ikifanyika mwaka jana utalii utajibu kuanzia mwaka huu na kuendelea!

Utalii ni gharama kubwa so wazungu huwa wana save kwa muda mrefu then ndio afanye booking ya tour.

Chawa wasio na akili.
 
Watalii wakisoma kuhusu ngorongoro wanaambiwa kuwa ni mbuga pekee ambayo wanyama wanaishi na MAASAI.

Wakifika wanakuta hola, Maasai Walishaondoshwa Kwa Mtutu.

Vumilia eeeee Tanzania, baada ya Kiza line, hatimaye KUTAPAMBAZUKA.

Aamen.
 
Angalia takwimu za miaka iliyopita [emoji116]
IMG-20221214-WA0000.jpg
 
Hongera na kazi wadau..

Nitumie fursa hii kueleza habari Njema za Royal tour..

Idadi ya Watalii Waliotembelea Tanzania kwa miezi 11 ya mwaka 2022 wamefikia Milioni Moja na Laki mbili(1,200,000).

Hizi Ni habari njema zikizoletwa na Royal tour na bila shaka Hadi Mwisho wa mwezi wa 12 Idadi ya Watalii itavuka 1.3Mil.

Bila Shaka huko tuendako Mambo yanaweza kuwa mazuri ikizingatia Tanzania umeweka lengo la kufikia Idadi ya Watalii mil.5 mwaka 2025.

Hongera zenu Ila bado Sana kuwafikia Egypt, Morocco, South Africa nk.👇



Bora ungetafuta cha kuandika badala ya huu uchawa usio na ukweli hata 25%!

Sekta ya utalii ilifunguka baada ya Covid19 kupunguza makali yake!

Na hapo awali wageni wengi walikwishalipia safari zao,kabla ya katizo la covid19.

Hivyo ilipofunguka wote walimiminika kuja nchini wakiwa katika makundi mawili.ambayo ni wale waliokuwa wamelipa awali bila kuchukuwa pesa zao.

Na wale waliokuwa wanakuja kurekebisha akili zao baada ya quarantine ya muda mrefu huko makwao.

Mataifa yaliyoongoza kwa kuja nchini ikuwa ni Russia na Ukraine kabla ya vita kuanza.

Na hata ushahidi ni pale baadhi yao walipokwama Zanzibar kwa miezi kadhaa baada ya vita kuanza huko Ukraine.

Mpaka Royal tour inazinduliwa na Peter huko USA. Warusi na wa Ukraine walikuwa wakiendelea kumwagika.

Kundi la pili ni la Waisrael wa kundi la "Shromo" almaarufu kama "Another World" wao mpaka sasa wanaendelea kuja na madege yao yakiwasubiri pale KIA.

Hiyo Impact yako ya Royal Tour sijui umeitolea wapi?

TTB wao wanatoa rekodi bila kutaja vyanzo vya wageni hao,ukiwa ni mtindo endelevu wa uchawa uliokomaa nchi hii.

Mpaka sasa mataifa yanayoongoza kwa kuingiza wageni nchi sio Marekani.

Ni Wajerumani, waspanniola,na mataifa mengineyo.

Ukitaka data za ukweli nenda kwa Tour Operators watakueleza na kukusaidia ili ukamilishe azna yako.

Nimecopy kutoka kwa Member VOICER.
 
Hawa mambuzi tushukuru Mlima KILIMANJARO hauhamishiki,

Ungeshahamishiwa Dubeiiiiiii!!!!
Halafu anataka kutufumba midomo kwa kujificha kwenye ushahidi, ni sawa na mtu aulize sehemu kuku anapotolea kinyesi wakati upepo unapuliza.....
 
Back
Top Bottom