RPC Geita: Askari haruhusiwi kumpiga mtu, anatakiwa kumueleza kosa lake na amfikishe Kituoni

RPC Geita: Askari haruhusiwi kumpiga mtu, anatakiwa kumueleza kosa lake na amfikishe Kituoni

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi SACP Safia Jongo ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita amesema hakuna mtu akiwemo Askari Polisi anayeruhusiwa kumpiga mtu bali anatakiwa amueleze kosa lake na amfikishe Kituo cha Polisi.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Safia Jongo ametoa kauli hiyo wakati wa Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, yaliyotolewa kwa Watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa wenye viti na Maafisa Tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Video: Star TV
 
Askari wa Tz au Huko Dunia ya kwanza? 😅
 
Hicho kitambulisho kwa wasiokuwa kusoma ni mtihani,waende kwa mtendaji.Silaha wanazokuja nazo nalo ni tatizo,watu wanaogopa silaha.
 
Police wa Tz bana😂...mnasema ndoto zA Alnacha...labda mfutwe kazi wote waajiriwe wengine na wasiajiriwe na serkal ya ccm
 
Back
Top Bottom