KwetuKwanza
Senior Member
- Mar 13, 2023
- 127
- 245
AIBU YA CCM SIMIYU LEO TAR 22.0 JESHI LA POLICE LA SHIRIKI KUSOMBA WAJUMBE WA CCM KWENDA KWENYE MKUTANO WA MAKALA BARIADI.!!!*
Na Mzee madiba
Simiyu -bariadi.
Leo tar 22.03.2025 mkoani Simiyu Kuna kitu walichokiita sherehe za miaka minne ya Samia.
Hii ni issue iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa Kwa kushirikisha makada wachache wa chama Cha mapinduzi mkoani Simiyu. Tumeshuhudia misululu ya malori yakitokea vijijini yakiwa yamebeba wajumbe waliohudhuria mkutano wa makala mwenezi wa CCM.
Yote hayo sishangazwi nayo kilichonifanya nichukue Karam yangu na kuanza kuandika hili ni Hali ambayo sikuwahi kuiona Kwa macho kuona magari ya police yakishiriki kusomba watu kuwaleta kwenye mkutano WA CCM ili makala ajaze watu na kamera zionyeshe wingi wa watu.
Shida Iko wapi!?
Tatizo hapa ni magari ya umma Tena ya jeshi letu ambalo mara nyingi limekuwa likijinasibu kuwa halina chama, halina upande, halitumiki kisiasa,. kulitumiki kwenye shughuri za kiasiasa kwenye chama cha mapinduzi ccm.
Jeshi la police mkoani Simiyu linaweza kutuaminishaje kuwa sio ccm B!!? RPC SIMIYU tukisema Leo katumia Kodi zetu, magari yetu ya umma kwa kufanya shughuri za ccm atatubishia Kwa utetezi upi?
Kuwa na Imani na jeshi letu la police ni sawa na kuamini kuwa watanzania tunaweza kupata bikira kwenye wodi ya wazazi. Jeshi letu limekuwa likituhumiwa kuwa ni wasaidizi wa CCM kwenye chaguzi za kiserikali dhidi ya vyama vya upinzani, wamekuwa wakituhumiwa kwa kuwaumiza mahasimu wa chama Cha mapinduzi ccm. Wananchi na wapinzani kwa Nini tusiamini pasipo shaka kuwa jeshi la police Simiyu limetudhibitishia kuwa SI sehemu ya ulinzi wa watu na Mali zao Bali ni ccm B.? Na niwalinzi wa chama Cha mapinduzi.
Tunajua j.mosi ijayo makam m/kiti wa CCM taifa WASIRA atakuwa na ziara mkoani Simiyu naye atatumia jeshi letu kuhakikisha linamsaidia kumletea wanachama WA CCM kwenye mkutano wake watatumia magari yetu ya umma, mafuta yetu ya umma ambayo yangeliweza kuwahi matukio ya wizi ama ya kuokoa uhalifu mbalimbali ndani ya mkoa wetu.
Hii ni kuonyesha wazi kuwa wananchi wamedhalaulika tunaonekana hatufai na hatuna la kuhoji dhidi ya ujinga huu.
Kiufupi mambo mengi ambayo yamekuwa yakiendelea mkoani Simiyu ni program za viongozi kupiga pesa kupigitia matukio yanayotengenezwa kwa mgongo wa kupongeza, matamasha mbalimbali yasiyo wanufaisha wananchi Kwa lolote ikiwemo hili la sherehe za mama Samia miaka minne. sherehe hizi zinasaidia Nini Kwa Jamii? Je ni sehemu ya kutatua changamoto zetu kama vile ukosekanaji wa huduma Bora za Afya, huduma za Maji safi na salama, Elimu, miundombinu na ukosefu wa ajira kwetu sisi walimu??
Kuna pesa zinapigwa kupitia michango kutoka kwenye mashirika mbalimbali kwa kigezo Cha kuchagia shughuri hizo. ikiwemo mabank, wafanya biashara, na wachimbaji walioko mkoani Simiyu. Tunavijana walioaminiwa na mhe Rais kama wateule ni wezi na soon tutatoa ubadhirifu wote wanaoufanya viongozi wa mkoa wa Simiyu. Tutawaonyesha namna wananchi wa mkoa wa Simiyu wanavyoibiwa huku wakiwa wanakufa Kwa kukosa dawa hospital, kukosa miundombinu za Barbara na Maji safi na salama.
My take.
Mhe Rais piga marufuku hizi program zinazotengenezwa na wateule wako maana asilimia 90 ni wizi mtupu unaoendeshwa wa kuibia watu, hii ni sehemu ya mianya ya kupigia pesa viongozi kwenye mikoa yetu. Ukisikia Samia marathon, sherehe za mama, Samia jogging ni sehem ya watu kupiga pesa.
Picha hii kwa sababu ni wawakilishi wa mhe Rais wanaofanya haya imekuwa ni kuchafua sura ya mhe Rais. Na hii itatufanya tujue kuwa sura ya mteule itakuwa the same to boss.
Jeshi la police hatuwezi kuliamini Tena hasa kwenye shughuri zote za kusimamia mambo kama chaguzi maana tayari limeonyesha wazi ni sehemu ya chama cha mapinduzi hivyo tunapaswa kulikabili kama tunavyoweza kuikabili ccm kwenye chaguzi zote za kiserikali.
RPC SIMIYU JUDITH SWEEBE. Kwa vile tumeona kuwa jeshi lako ni sehemu ya chama cha mapinduzi tutapaswa kuwambia wananchi namna msivyoweza kuaminika mahala popote pale. Na unapaswa utoe mwongozo wako kupitia PGO kama ni sahihi kutumia magari ya police ambayo ni Mali ya walipakodi wa Tanzania kusomba wanaccm kwenda kwenye mikutano Yao.
Kuna mengi ninayo kuhusu mkoa wa Simiyu soon tutaanika uozo mlionao viongozi wa mkoa KENANI RABAN KIHONGOSI.
NIWATAKIE MFUNGO MWEMA WA KWALEZIMA.
NIWATAKIE MFUNGO MWEMA WA RAMADHAN.