TANZIA Rubani aliyetorosha ndege baada ya kuvunjika EAC, Captain Narzis Mapunda afariki dunia

TANZIA Rubani aliyetorosha ndege baada ya kuvunjika EAC, Captain Narzis Mapunda afariki dunia

Director of Ops mstaafu wa Air Tanzania Captain, Narzis Mapunda jana asubuhi tarehe 23/05/2021. RIP Capt. Mapunda..
Ndiyo Rubani aliyekuwa na Vituko kuwahi kutokea katika Historia ya ATC na sidhani kama yupo mwingine aliyetokea Kuuiga ' Uchakaramu ' wake huo.

Alikuwa haruki bila Kuzimua kidogo na alikuwa ni makini na Safari za dakika 90 Yeye atatumia dakika 60 au 75. Alikuwa na Chumba chake cha Kuzimulia ' Gambe ' pale KIA.

Na ni Yeye Marehemu aliyeanzisha Mtindo wa kila mkienda KIA kama hali ya Hewa ni nzuri Anganj kabla ya Kutua atawapigisheni sana ' raundi ' Mlima Kilimanjaro ( kwa nbali ) ili muuone vizuri.

Wanafunzi wa Kitanzania waliokuwa wakisoma nchini Uganda kati ya mwaka 1995 hadi 2000 watamkumbuka kwa mengi hasa alipokuwa ana bahati ya kuwa Rubani aliyekuwa akipiga mno ' Ruti ' za Dar - Entebbe - Dar na kubahatika ' Kurushwa ' nae angani.

Pole zangu nyingi kwa Familia yake Mkewe, Watoto pamoja na ATCL kwa ujumla kwa Kuondokewa na Rubani huyu Mahiri, Mzoefu, Mweledi na Mcheshi mno Captain Mapunda aliyenifanya nitamani kuwa Rubani kama Yeye, ila bahati mbaya Malaika wa Fizikia, Jiografia na Hisabati ( PGM ) walinikataa Kidarasani.
 
Mbele yake, nyuma yetu.

Poleni sana wafiwa
 
Ndege za miaka iyo zilikuwa zinapendeza ukilinganisha za sasa hivi.
Kubadilika kwa teknolojia, ni kama magari, mengine hivi sasa yanafanana na sura za wanyama

1621906247583.png
vs
1621906314658.png
vs
1621906988830.png

1621906409174.png
1621906431986.png
1621906536617.png
1621906579548.png
1621906715435.png
 
Mbona kama nakumbuka Captain Mapunda alishafariki miaka minne hivi na tukamzika pale makaburi ya kinondoni?Una hakika Mapunda huyu ndiyo yule?

Huyu nadhani ni yule aliyepewa zawadi ya Milioni kadhaa na Magufuli pale Airport miaka kama miwili hivi iliyopita
 
Mbona kama nakumbuka Captain Mapunda alishafariki miaka minne hivi na tukamzika pale makaburi ya kinondoni?Una hakika Mapunda huyu ndiyo yule?
Unashangaa au? Ni Tanzania tu project moja ina sainiwa mara 10 ni Tanzania mradi mmoja unazinduliwa mara kumi ni Tanzania tu mtu mmoja anaweza kufa mara 10 na ni Tanzania tu mtu anaweza kutorosha ndege kama kutorosha gari. Maelezo mengine unasoma tu ndege inaruka sehemu bila kupewa clear sijui kwa kweli kama ni hivyo tuchunguni zile Boeng zetu pale zimepack tusije kusikia mtu kanyanyuka nayo tu huyooooo
 
Kwa kuwa waKenya walikuwa na njama ya kujimilikisha mali zote za iliyokuwa jumuiya ya afrika ya mashariki. Wao ndio waliopanga kuivunja na wakaweka huo mkakati kuwa ndege zote zitakuwa Kenya wakati wa uvunjaji wa jumuiya. Ni bahati hiyo moja ililetwa kwa kuwa nyingine ziliishia Kenya.
Inaweza kuwa na ukweli lakini ndege kuruka airport bila kupewa clear na control tower sijawahi kusikia ndege inaruka airport tu kama bus ubungo kundoka hata bus nadhani wanapewa ruhusa hii story iko kisiasa hivi kwa uelewa wangu traffic control bila kutoa clear na refuel ndege haiwezi kuondoka airport, maoni yangu.
 
Du so ile ofa yake aliyopewa ya kupanda ndege bure maisha yake yote popote anapoenda ndo imetamatishwa hvyo.
 
Inaweza kuwa na ukweli lakini ndege kuruka airport bila kupewa clear na control tower sijawahi kusikia ndege inaruka airport tu kama bus ubungo kundoka hata bus nadhani wanapewa ruhusa hii story iko kisiasa hivi kwa uelewa wangu traffic control bila kutoa clear na refuel ndege haiwezi kuondoka airport, maoni yangu.
Inawezekana kabisa na imeshafanywa mara nyingi. Commander ndio ana amua kuruka ama kutokuruka, na anaamua kufuata ama kutokufuata maelekezo ya tower ingawa, matokeo ya uamuzi wake yanaweza kuwa kufungiwa leseni n.k. Hicho ndio kinawafanya kuogopa.
 
Ok nimekuelewa ila kuna swali la nyongeza, ndege labda inatakiwa fuel na pilot atapita security area maana ziko ground service lazima ndege ipitie ipate clear sasa swali mtu anaweza kupita process zote hizo bila kuulizwa unaenda wapi labda kama alikuwa angani taarifa hizo zikaja akachukuwa maneuver juu kwa juu hapo ina make sense.
 
Back
Top Bottom