Rubani na msaidizi wa Precision Air iliyopata ajali wamekufa kwa uzembe wa mamlaka zinazohusika na uokoaji

Ni bahati mbaya Sana hatujawahi kujifunza na hakuna dalili yoyote kama tutajifunza hivi karibuni, ni kwa neema tu hizi ndege, meli na magari yanatufukisha tuendako lakini tuna mifumo ya usalama na uokozi duni kabisa.
 
Viongozi wetu wanapenda kutumia magari ya gharama,wakistaafu wanajengeana majumba ya kifahari wakati hata vifaa vya kisasa vya uokoaji hakuna.

Nadhani watu wakishakuwa viongozi huwa wanapata mafunzo ya jinsi ya kutokujali.
Aibu kama hizi zinaendelea kutokea, nakumbuka kuna ajali moja watu wa uokoaji walisema giza limeingia tutakuja kuokoa tena asubuhi, muda huo watu wapo chini ya maji.
 
Huyu aliyezuia rubani na msaidizi wasitolewe ni nani na kwa nini? Alikuwa na motives gani behind?

Your browser is not able to display this video.
 
Inaumiza Sana kwa kweli....taifa la wasiojali.
 
Ajali nyingi za huu ulimwengu wa tatu huwa zinasababishwa na kuzimu. Watu wako connected na shetani kuliko walivyo connected na Mungu Muumba wa mbingu na nchi. Matukio haya ya kimaafa huwa yanaratibiwa na adui ibilisi huko kuzimu. Tujikamate na Mungu, Mwokozi wetu tutakuwa salama.l hakika.

YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Huu ni uzembe kabisa kama walikua wanawasiliana naye kipi kiliwashinda maji yalipowazidia kuvunja dirisha au kioo cha rubani kuwatoa..? Dogo majaliwa asinge pigwa na ile kamba akazima angevunja na rubani angechomoka
 
Hawajafa kwa uzembe, kwa jinsi ndege ilivyoumia mbele, wale kuna uwezekano mmoja wao alikuwa keshakufa, mmoja ndo alikua kavunjika miguu.
Tofauti na hapo wangetoka tu
 
Last minutea before landing on the water
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…