Ruby Aamua Kuacha Muziki wa Bongo Fleva na Kumrudia Yesu

Ruby Aamua Kuacha Muziki wa Bongo Fleva na Kumrudia Yesu

Yohana 1:12-13
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
 
RUBY was such a natural born talent
Nahisi alikuwa too neurotic na wakubwa walimshinda tabia.. Kuna muda ili ufanikiwe inahitaji uwe na roho ngumu.

Angekuwa msanii bora wa kike kama angepata the right people wa kumsimamia
 
Mwanamuziki mashuhuri nchini Tanzania, Ruby, ametangaza kuanza sura mpya ya maisha yake kwa kuamua kuacha muziki wa Bongo Fleva na kuwekeza maisha yake katika kumtumikia Mungu.

Akiwa mmoja wa waimbaji wa kike walioacha alama kubwa nchini kupitia sauti yake ya pekee na uwezo wa kutumbuiza jukwaani (LIVE show), Ruby amekuwa akionyesha mabadiliko ya kiroho kwa muda sasa. Kupitia kauli na maisha yake ya hivi karibuni, msanii huyo ameweka wazi uamuzi wake wa kuingia kwenye huduma na kumfuata Yesu Kristo.

Uamuzi huo unagonga fikra za mashabiki wengi waliomfuatilia kwa miaka mingi, huku wengi wakimtakia kheri katika safari yake mpya ya kiroho licha ya kwamba sauti yake na nyimbo zake zitaendelea kukumbukwa kwenye tasnia ya burudani.

View attachment 3655933
Welcome aboard,Jesus is Lord...
 
Back
Top Bottom