Rudeboy ashauri wanaume pia kukataa uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke fukara!

Kwanza watawakataa wanawake mafukara.

Halafu, kama kigezo ni pesa, itaangaliwa pesa tu, bila kujali mwanamke au mwanamme.

Kwa hiyo hata mwanamke mwenye pesa ataweza kupinduliwa na mwanamme mwenye pesa zaidi.

Si kigezo pesa?
Daa kazi kweli kweli
 
Mwanamke fukara unamuonea huruma unamuo, mbeleni anakusaliti kwa lijamaa lenye hela. Unashindwa uue yupi kati ya wawili hao walioharibu ndoa, unaamua isiwe taabu unamuacha mwanamke akaolewe na mwenye hela kiu yake itulie
Hatari sana aisee
 
Ukiwa nazo ndio inavyotakiwa ila kama huna lazima uende Kwa fukara mwenzio
 
Hamna kitu kibaya hasa kwa mapenzi ya siku hizi, kulithaminisha tendo la ngono kwa fedha, ndio maana linapoteza maana na kusababisha hata ndoa zionekane hazina maana kwani kuna wengine wanauziwa ngono kwenye ndoa zao.

Sometimes unashindwa kutofautisha malaya na mke,sababu mwisho wa siku wote wanataka pesa,bila pesa ngono/mapenzi hamna.

swala la mwanaume kupata faraja wakati anapitia hali ngumu ya kiuchumi siku hizi wanaoweza ni wanawake wachache mno, ila wengi hawawezi wengine wanawakimbia mpaka waume zao,ambao mwanzoni unakuta alikuwa na hali nzuri ya kiuchumi ila kuteteleka kidogo mke anakimbia.

Sometimes ukifikiria sana unaona hata hawa wapenzi tulio nao wanatuuzia.Hata hizi kelele za kutusema wanaume ni wabahili, ukichunguza sana utakuja kugundua kwamba wanwake wengi wanapenda luxury, ila wanaume wengi wana uwezo wa kutimiza mahitaji ya msingi ya mwanamke na si luxury hizi wazitakazo.

Hali itakuwa mbaya zaidi endapo mwanaume nae akianza kuthaminisha tendo la ngono kwa fedha,sababu atakuwa anaenda kinyume na majukumu yake ya kiasili.
 
Naunga mkono hoja mfano mm huwa si date kabisa na Manzi asiye na nauli
 
Uko sahihi kbsa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…