Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,513
- Thread starter
-
- #41
Wenye akili wanasubiri kikao kikae maamuzi ya rufaa yatolewe.mengine yote ni umbea na ujinga. Kupoteza muda.
Sijui kwanini unahangaika hivi.
Hizo hoja umeziandika kiushabiki sana, hayo majibu unayoyaita ya "uhakika" kwangu sijaona uhakika wowote, hao wanawake walikosea usije kuwatetea hapa kwa kigezo cha "haki za wanawake"
Lazima sheria na taratibu zifuatwe siku zote regardless ya jinsia ya mtu.
Sasa kilio kwa Mbowe kinatoka wapi kwani wakishinda ina maana wanaendelea kuwa wabunge na ruzuku inaingia CHADEMA hapendwi mtu.View attachment 1662261
Mhe Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.
Sasa ni wazi kwamba, Mheshimiwa Halima Mdee na wenzake 19, ambao ni wabunge wa viti maalum kupitia Chadema, watarudishiwa uanachama wao asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la Chadema litakapokutana kusikiliza rufaa yao waliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, juzi tarahe 27 Desemba 2020.
Akiongea na mtandao wa Mama Amon, Mbunge mmoja wa viti maalum, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na mashitaka sita. Anayataja hatua kwa hatua kama ifuatavyo:
โMosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushiriki katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi.โ
โPili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.โ
โTatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.โ
โNne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.โ
โTano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama.โ
โNa sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.โ
View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema
Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, โtayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.โ
Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu. Anasema kuwa, barua za tuhuma zilikuwa na ukurasa mmoja usio na ufafanuzi wowote unaowawezesha kufanya utetezi wenye mashiko.
Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.
โMosi, katika suala la maudhui ya tuhuma, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,โ anasema Mbunge huyo.
โNa unajua baadhi yetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma. Ni kwa vipi tumepewa tuhuma eti za kula njama na kujiteua?โ anauliza Mbunge huyo.
โPili, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,โ anasisitiza Mbunge huyo.
โNa tatu, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,โ alifafanua Mbunge huyo.
"Pia, tulishangazwa na uandishi wa tuhuma. Kawaida lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo ya kosa yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Ni kama Kamati Kuu inabahatisha. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakamilika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge
Sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kuitisha Baraza Kuuu ili kusikiliza na kuamua rufaa hizi kumi na tisa.
Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi huo wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mujibu wa ibara ya 5.4.4 ya Katiba ya Chama baada ya kuridhika kwamba walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama.
Aidha, Kamati Kuu iliwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.
Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.
Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.
Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema," kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama.
View attachment 1662268
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema
Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. โKwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,โ alionyesha mshangao.
CHADEMA ikae kimya tu kwa sasa isubiri hii miaka minne. Hawa ni wakaidi itengeneze tena akina mama wengine mashujaa watakaochukua nafaai zao 2024. Its time now to dump all that disobeys Party integrity.
UPUUZI MTUPU
Wasitegemee nafuu yoyote. Kwa muundo wa vyama vyetu vya siasa, maamuzi ya KK huwa hayapinduliwi.
Bulaya hana uwezo wa kujenga hoja kisomi hivyo.
Upuuzi ni jambo la kipumbavu lisilo na maana.
After you have read many books this year, Is this what you mean realy?
Unajua makala za kipumbavu hivi ndio zitapelekea hata msamaha wasipate
Endeleeni kushika simba sharubu
Halafu mpo humu kudharau Chadema,haya Chadema itakapo waonesha kua si ya kuchezea msilie
Halima Mdee and her group inawatuma muendelee kutukana Chadema,mtalia
๐๐๐๐ where did you learned that I read many books this year? ๐ณ๐ณ๐ณ
Narudia tena ulichoandika ni UPUUZI MTUPU!
Inasikitisha sana watu smart kama nyie kuingizwa mkenge na Dk Mahera na Ndugai tu.Nimekula kiapo sitaji mtu ng'o
Naona boss unauliza jibu badala ya kupigia mstari๐๐๐๐๐Hisia zangu zinaniambia mmojawapo wa wale 19 ni Mama Amon mwenyewe.
Ni hisia tu
Inasikitisha sana watu smart kama nyie kuingizwa mkenge na Dk Mahera na Ndugai tu.
I disagree.
I see good arguments which will exercise the minds of sensible members of Baraza Kuu
Mara zote nampuuza Sana mtu anayewadanganya wenzio kwamba individuals zinaweza shindana na taasisi.Ni kujidanganya
Yaani mpaka kesho sijaelewa Mdee aliendaje kuapa bila kuongea na Katibu Mkuu hata kwenye simu kwamba wanaelekea kuapa?Hizo hoja umeziandika kiushabiki sana, hayo majibu unayoyaita ya "uhakika" kwangu sijaona uhakika wowote, hao wanawake walikosea usije kuwatetea hapa kwa kigezo cha "haki za wanawake"
Lazima sheria na taratibu zifuatwe siku zote regardless ya jinsia ya mtu.
Kwani hamjaingizwa mkenge na Dkt. Mahera na Ndugai ?Unapiga ramli. Turudi kwenye hoja
Answer my question please about your statement that I read many books this year. Acha kuruka ruka,