Distant Relatives
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 414
- 732
Hahaha. Najua deep in ur heart unakubaliana nami kuwa kuna harufu ya dola kutumika. 1. They got the motive. Wanahitaji opposition Bungeni to win donors; and 2nd, Behaviours ya vyombo vya dola kwenye hili ni wa kutia mashaka.Speculations sio ushahidi wa kuweza kutumika ktk kukoleza hoja zilizowasilishwa hapa
Haahaa! Mdee kapotezea tu,yaani Bashiru akatae kumtambua mbunge wa Chama chao CCM halafu huyo mbunge aendelee, weeeh!Kuna madume wengi wanazaa mtoto na kuruka meta mia.
Mshangao wa Mnyika unaweza kuwekwa ktk kundi hili pia.
Kisha uamuzi unafanyika kwa kura ya siri
Ni sawa
Hii ni tofauti,unaepigana nae yeye ndio jaji.....
Unafeli
So what COVID19? Nyie MRIE TU! Cha kufanya ni kutubu dhambi zenu za mliyofanya kukana rushwa ya maccm mliyopewa ya viti maalum ili mrudishwe kwenye timu. Mkifanya hayo mimi pia I’ll fight for you in public and behind the scenes, otherwise BYE BYE!
Haahaa...mdee kapotezea tu.yaani bashiru akatae kumtambua mbunge wa chama Chao ccm halafu huyo mbunge aendelee.weee....
By any means hizi nafasi ilikuwa ni lazima mpewe lakini ni baada ya KK kukaa na kutafakari kwa kina juu ya suala hili faida hasara na hekima ni ipi juu ya hili lakini kimbelembele kikatawala wachache wakajisukuma kuelekea huko kwa barua feki infact maamuzi ya kitaasisi huwa ni muhumu mno.Ushauri wako ukitekelezwa hata wewe utakuwa dumped.
Hiyo ni kwenye vyama vyote ndugu, Sio CCM Wala upinzani.kwa mfano ndani ya CCM ukikata rufaa halmashauri kuu bado mwenyekiti ni JPM, ndo anaongoza vikao vyote.Nadhani una point. Kwa hiyo basi, inabidi kina Mdee wakate Mwenyekiti w Kamati kufanya kazi kama Mwenyekiti wa Baraza Kuu. Sio vizuri mleta mashtaka awe hakimu...
Haahaa we unachanganya mambo ya mahakamani na Mambo ya vyama.Sheria ni msumeno ndugu
Napendekeza kwenye katiba hasa za vyama vya upinzani kuwe na kipengele kinachosema mteule wa nafasi yoyote kwa ngazi yoyote ile ya uongozi au uteuzi atapewa cheti cha uteuzi na kiongozi au viongozi husika mbele ya waandishi wa habari.View attachment 1662261
Mhe Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.
Sasa ni wazi kwamba, Mheshimiwa Halima Mdee na wenzake 18, ambao ni wabunge wa viti maalum kupitia Chadema, watarudishiwa uanachama wao asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la Chadema litakapokutana kusikiliza rufaa yao waliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, juzi tarahe 27 Desemba 2020.
Akiongea na mtandao wa Mama Amon, Mbunge mmoja wa viti maalum, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na mashitaka sita. Anayataja hatua kwa hatua kama ifuatavyo:
“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushiriki katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi.”
“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama.”
“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”
View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema
Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”
Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu. Anasema kuwa, barua za tuhuma zilikuwa na ukurasa mmoja usio na ufafanuzi wowote unaowawezesha kufanya utetezi wenye mashiko.
Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.
“Mosi, katika suala la maudhui ya tuhuma, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.
“Na unajua baadhi yetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma. Ni kwa vipi tumepewa tuhuma eti za kula njama na kujiteua?” anauliza Mbunge huyo.
“Pili, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Na tatu, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.
"Pia, tulishangazwa na uandishi wa tuhuma. Kawaida lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo ya kosa yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge
Sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kuitisha Baraza Kuuu ili kusikiliza na kuamua rufaa hizi kumi na tisa.
Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi huo wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mujibu wa ibara ya 5.4.4 ya Katiba ya Chama baada ya kuridhika kwamba walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama.
Aidha, Kamati Kuu iliwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.
Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.
Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.
Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema," kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama.
View attachment 1662268
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema
Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.
Waandike barua za kujiuzulu ubunge Kama kweli wanakipenda chama chao.Baraza kuu, liwasemehe na kuwa rudushia uanachama, lakini iwavue ubunge.
NGOMA IKO HAPA: Tunaweza kuwekwa mtegoni, Kitu ambacho hatufahamu kwa sasa, ni kuwa isije kurudishiwa uanachama ukahalalisha ubunge wao kwa muomo wa Mh Spika.
Napendekeza kwenye katiba hasa za vyama vya upinzani kuwe na kipengele kinachosema mteule wa nafasi yoyote kwa ngazi yoyote ile ya uongozi au uteuzi atapewa cheti cha uteuzi na kiongozi au viongozi husika mbele ya waandishi wa habari
Kwahiyo wadhani huyu atakuwa nani?Bulaya hana uwezo wa kujenga hoja kisomi hivyo.
Mbona unaandika kama vile unakimbizwa. MRIE TU ndo nini. Tuliza akili. Soma hoja. Jibu hoja.
Waandike barua za kujiuzulu ubunge Kama kweli wanakipenda chama chao
Haahaa we unachanganya Mambo ya mahakamani na Mambo ya vyama.
CHADEMA haitambui ushindi wa CCM uchaguzi 2020, utasemaje wateue wengine?Napendekeza wakati chama kinakamilisha kuwafutilia mbali hawa waliojiteua,kipendekeze na kupeleka majina mengine rasmi kwa idadi hiyo ili kutendea haki nafasi hiyo ya viti maalum
Wewe kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa hasa za upinzani nchini, unalichukuliaje hili suala mama Amon?Kwenye rufaa yao wanasema hawajafanya kosa. Kwa nini wajiuzulu?
Hyo ni kwenye vyama vyote ndugu, Sio ccm Wala upinzani.kwa mfano ndani ya ccm ukikata rufaa halmashauri kuu bado mwenyekiti ni jpm, ndo anaongoza vikao vyote