Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Wakiitwa watu wenye akili na wewe utajitokeza?

Kura alizopewa Lisu ndio zimezaa hao Covid 19 na ndizo zinahalalisha Chadema kupewa ruzuku.

Usitumie kichwa kufugia nywele.
Wabunge wasipokwenda ile milion kwa mwezi kila mbunge wa Chadema analipa kwa chama itatoka wapi ?Kwani umesahau wabunge wa Chadema kila mwezi huchangia chama kwa sababu ya kujenga chama ????????
 

1609266361537.png



Haya! Nina yangu moyoni!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Halafu sijaona mtu mlafi na mbinafsi kama huyu Halima Mdee.

Hili sakata lisingekuwepo jina lake ningejuwa angalau anapigana kuwainuwa Bawacha, lakini Halima amekaa bungeni miaka 15 na bado kwa ulafi nafasi hizi kajipachika yeye na fiancee wake na Uenyekiti wa Bawacha bado akabaki yeye.

Huu ni ulafi uliopitiliza.
 
Halafu sijaona mtu mlafi na mbinafsi kama huyu Halima Mdee.

Hili sakata lisingekuwepo jina lake ningejuwa angalau anapigana kuwainuwa Bawacha, lakini Halima amekaa bungeni miaka 15 na bado kwa ulafi nafasi hizi kajipachika yeye na fiancee wake na Uenyekiti wa Bawacha bado akabaki yeye.

Huu ni ulafi uliopitiliza.
Off target.
Kuhusu topiki hizo anzisha bandiko tofauti.
 
Kwa majibu hayo ni wazi kuwa hao Covid hawana hoja na wanapoteza muda wao kung'ang'ana kuwa sehemu ya Chadema!
Tunalitaka baraza kuu lipigie mstari maamuzi ya kamati kuu!Hili suala liishe na hao Covid wabaki wabunge wa mfukoni wa Ndugai!
Ibada njema ya utawala bora lazima ianzie nyumbani kwenye chama kabla ya kusogezwa serikalini.
Haki juu ya utaratibu ni muhimu na lazima
Haki juu ya maudhui nayo ni muhimu na lazima
 
Mama Amon ni mmoja wa COVID19 tena ni kinara aliye na tamaa kubwa ya kurudi mjengoni hata kama ni kwa njia haramu.
Mama Amon. Tuseme tu ukweli. Hawa wabunge (Covid 19) . Je ingelikuwa ni Ccm wangekata hata hiyo rufaa huko Baraza kuu ?!. Tunakosa nidhamu kwenye vyama hivi visivyo na madaraka . Walichokifanya kina Mdee ukiondoa Nusrat Hanje ni utovu wa nidhamu.
 
Mama Amon ni mmoja wa COVID19 tena ni kinara aliye na tamaa kubwa ya kurudi mjengoni hata kama ni kwa njia haramu.

1609264569338.png


BAK na Odhiambo nawajibu kwa pamoja, maana naona mnapigana tafu kunishugulikia.

NI hivi:

1. Fomu zilizoko NEC zina sahihi ya Mnyika ambayo ni halisi.

2. Dispatch book ya Katibu Mkuu, John Mnyika, ina mhuru wa NEC kuonyesha kwamba wamepokea barua na fomu zake.

3. Kwa hiyo, Mnyika aliandaa kila kitu halafu

(a) Ama mjanja mmoja akabeba mzigo na kukabidhi NEC
(b) Au Mnyika mwenyewe alipeleka na sasa anajishebedua kwa kukana.

4. Kwa hiyo, kuna watu wawili maximum wanaopaswa kuadhibiwa na Chadema.
(a) Mnyika kwa uzembe wa kushindwa kutunza Ofisi yake.
(b) Mtu mmoja X aliyeiba nyaraka kutoka kwenye ofisi ya Mnyika, endapo 3(b) sio kweli.

5. Kama huyo mtu X ni miongoni mwa wabunge 19, basi wabunge 18 hawana hatia, kwani, kwa mujibu wa hoja hii, ni vigumu kuthibitisha conspiracy.

6. Kwa hiyo, kelele za fukuza covid19 wote, nye nye nye, sijui nini, ni dalili za watu walioziba akili zao na kuzizuia kufikiria juu ya extra possibilities.
 
View attachment 1662261
Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.

Sasa ni wazi kwamba, Mheshimiwa Halima Mdee na wenzake 18, ambao ni wabunge wa viti maalum kupitia CHADEMA, watarudishiwa uanachama wao asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yao waliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020.

Akiongea na mtandao wa Mama Amon, Mbunge mmoja wa viti maalum, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na mashitaka hafifu sita na ambayo hayana mashiko.

Anayataja hatua kwa hatua kama ifuatavyo:

“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushiriki katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. Barua haina maelezo yanayojibu maswali haya: tulitenda kosa lini, kivipi, wapi, na tukiwa na nani? ”

“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama. Barua haina maelezo yanayojibu maswali haya: tulitenda kosa lini, kivipi, wapi, na tukiwa na nani? ”

“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama. Barua haina maelezo yanayojibu maswali haya: tulitenda kosa lini, kivipi, wapi, na tukiwa na nani? ”

“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama. Barua haina maelezo yanayojibu maswali haya: tulitenda kosa lini, kivipi, wapi, na tukiwa na nani?"

“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama. Barua haina maelezo yanayojibu maswali haya: tulitenda kosa lini, kivipi, wapi, na tukiwa na nani?"

“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama. Barua haina maelezo yanayojibu maswali haya: tulitenda kosa lini, kivipi, wapi, na tukiwa na nani? ”


View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema

Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”

Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu.

Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.

“Mosi, katika suala la maudhui ya tuhuma, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.

“Na unajua baadhi yetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma. Ni kwa vipi tumepewa tuhuma eti za kula njama na kujiteua?” anauliza Mbunge huyo.

“Pili, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.

“Tatu, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.

"Na nne, ni kuhusu utaratibu vile vile. Tunapinga mtindi wa uandishi wa tuhuma dhidi yetu. Kawaida ya kuandika tuhuma ni kwamba lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo ya kosa yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge

Kwa kuzingatia haya yote, sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kuitisha Baraza Kuuu ili kusikiliza na kuamua rufaa hizi kumi na tisa.

Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi huo wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mujibu wa ibara ya 5.4.4 ya Katiba ya Chama baada ya kuridhika kwamba walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama.

Aidha, Kamati Kuu iliwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.

Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.

Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.

Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa
mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema," kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama.

View attachment 1662268

Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema

Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.
Mama Amina...

K.....m...ko!
 
Umechekarika lakini bado ni upuuzi mtupu. Waambie COVID19 wenzio kurudi Chadema inawezekana tu ikiwa mtaomba samahani na kutema hiyo rushwa ya JIWE na ndugai ya viti maalum ila kama mnataka kuendelea kujifanya wajuaji MTAULA wa CHUYA.
View attachment 1662438

BAK na Odhiambo nawajibu kwa pamoja, maana naona mnapigana tafu kunishugulikia.

NI hivi:

1. Fomu zilizoko NEC zina sahihi ya Mnyika ambayo ni halisi.

2. Dispatch book ya Katibu Mkuu, John Mnyika, ina mhuru wa NEC kuonyesha kwamba wamepokea barua na fomu zake.

3. Kwa hiyo, Mnyika aliandaa kila kitu halafu

(a) Ama mjanja mmoja akabeba mzigo na kukabidhi NEC
(b) Au Mnyika mwenyewe alipeleka na sasa anajishebedua kwa kukana.

4. Kwa hiyo, kuna watu wawili maximum wanaopaswa kuadhibiwa na Chadema.
(a) Mnyika kwa uzembe wa kushindwa kutunza Ofisi yake.
(b) Mtu mmoja X aliyeiba nyaraka kutoka kwenye ofisi ya Mnyika, endapo 3(b) sio kweli.

5. Kama huyo mtu X ni miongoni mwa wabunge 19, basi wabunge 18 hawana hatia, kwani, kwa mujibu wa hoja hii, ni vigumu kuthibitisha conspiracy.

6. Kwa hiyo, kelele za fukuza covid19 wote, nye nye nye, sijui nini, ni dalili za watu walioziba akili zao na kuzizuia kufikiria juu ya extra possibilities.
 
Umechekarika lakini bado ni upuuzi mtupu. Waambie COVID19 wenzio kurudi Chadema inawezekana tu ikiwa mtaomba samahani na kutema hiyo rushwa ya JIWE na ndugai ya viti maalum ila kama mnataka kuendelea kujifanya wajuaji MTAULA wa CHUYA.
Naona siku hizi umeanza utopolo.
Dawa yako inachemshwa jikoni.
Tutakusubiri kwenye kaburi la yule mmama role model wa mtoto wako...
Ngoja...
 
😂😂😂😂😂😂😂 mbona unapanick sasa lol! Acha kujibaraguza mimi role models wangu ni wazazi wangu huyu unayemjua wewe ni FAKE. Kwi kwi kwi B banaaa kule Twitter unarudi lini? Mbona umekimbia kimoja?
Naona siku hizi umeanza utopolo.
Dawa yako inachemshwa jikoni.
Tutakusubiri kwenye kaburi la yule mmama role model wa mtoto wako...
Ngoja...
 
Back
Top Bottom