Pre GE2025 Rufiji: Akina mama wagalagala chini kumpokea Mbunge Mchengerwa Ikwiriri

Pre GE2025 Rufiji: Akina mama wagalagala chini kumpokea Mbunge Mchengerwa Ikwiriri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi ndivyo Mbunge Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI alivyopokelewa jimboni Rufiji, Ikwiriri na akina Mama kwa kugalagala.

Soma Pia:

Maendeleo hayana Chama nimeona t-shirt ya CHADEMA inagalagala pia.
 
Kugalagala tena mimi nilifikiri ilikuwa ni enzi za Jiwe tu.
 
Kama Waziri kagalagala unashangaa nini kuhusu hao wakinamama?!
 
Huu ni ujinga sana,ni kujidhalilisha.
Ndo maana tunaonekana ni toleo la mwisho na la chini sana kwa kila kitu.

Kiongozi unafanyiwa hivyo na upo kimya tu kwa kudhani hiyo ni sifa.

Huu ni utumwa wa kifikra. KWANINI WAZUNGU,WAHINDI,WACHINA NA WAARABU wasitudharau na kutuchapa viboko? Wanaona matendo yetu na kutafsiri kwamba hazitutoshi hata kidogo.

Uafrica ni kielelezo cha Ujinga​
 
Hivi ndivyo Mbunge Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI alivyopokelewa jimboni Rufiji, Ikwiriri na akina Mama kwa kugalagala.

Soma Pia:

Ukute wamepewa buku 5 tu....wacha wafe kwa umaskini...
 
Hivi ndivyo Mbunge Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI alivyopokelewa jimboni Rufiji, Ikwiriri na akina Mama kwa kugalagala.

Soma Pia:

Huu ni udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za kibinadamu mtu mzima kugalalagazwa chini chini ya vumbi kisa kiongozi wa kisiasa kawatembelea.

Kosa hili ni sawa na ukeketaji na ni utamaduni ambao sio kuoneshwa kwa kila mtu ili waige maana hauna tija yoyote.

Kwanini hawa hawajachukuliwa hatua kama ambavyo tunaona watu wenye itikadi tofauti na CCM wakifanya?

Baraza la utamaduni, mila na desturi pamoja na TCRA hawalioni tatizo hili la kuwadhalilisha akina mama kwa kutweza utu wao?
 
Kwa akili hizi Bado tuna safari ndefu
 
Chama dola kongwe hakiishiwi na vituko, kwa kisingizio cha jadi na mapendo ruhani ya wananchi kwa CCM.
 
Hawa wa mama hawana watoto smart waume smart Wala ndugu ambao ni smart kichwani wanaongozwa na laana ya umasikini, km ni mkewangu katika uzee wake talaka inamfuata hapo hapo ya wazi kabisa
 
Back
Top Bottom