TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Kesho asubuhi saa 12 wahi pale utamkuta baba Paroko na Sakramenti zoote akiisoma misa kuu na ubani na kumuombea atoke jehanam aingie Toharani. Mark ma words. Paroko asingelithubutu kwenda pale leo bali kuanzia kesho kila siku atasoma misa 4 pale kwenye kaburi.
Hakuna dini nzuri ka Katoliki ya mitume weye
Weka mstari wa biblia unaosema mtu akiombewa /akifanyiwa ibada au misa baada ya kufa atatoka jehanam kwenda toharani mkuu
Halafu pia usisahau kutuambia toharani imetajwa wapi kwenye biblia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo mmaandiko uliyoyaweka hayakumaanisha kanisa physically, ni tafsiri ya kujenga imani, kanisa la roman catholic lilitoka huko urumi halikuanzishwa Israel alipokuwepo Yesu...
Hiyo ni tafsiri yako na sangoma wenzio. idiot.
 
Kwa heshima zote za kiserikali na kibinadamu na mapokezi aliyopata Marehemu Ruge, Je, alisitahili kuzikwa kwa ibada kuendeshwa na KATEKISTA?

Ukitilia maanani ukaribu wa familia ya marehemu na Askofu M. Kilaini

Ujirani uliopo kijijini kati ya Askofu na Prof. Mutahaba

Mazingira ya mwamko wa kidini ya RC uliopo hapo kijijini

Ujirani na Parokia yake ya Itahwa

Ushiriki wa viongozi hao wa dini katika kuaga mwili wa Marehemu hapo Bukoba Club/Gymkhana

Mwisho wa Mwisho ibada ya mazishi ikaishia kuendeshwa na KATEKISTA ikishuhudiwa viongozi hao wa kanisa kushindwa kushiriki ibada hiyo.

Kwanza Sio utamaduni wa eneo hilo kwa mtu kama wa aina ya Mutahaba.

Mwisho wa RUGE imekuwa simanzi kubwa kwani mbwembwe za mitaani zimezimwa na KANISA lake.

The very last RESPECT imeua yote.
Hakuna kilichozimwa na kanisa lake! ila hakuwa na vigezo vya kupata aina hiyo ya mazishi kutokana na kushindwa kuishi misingi yake akiwa hai. Boss hakuchagua kuishi kama Mkatoliki so amepata heshima kwa kadri ya stahili zake na pia ni kwa ukaribu huo unaousema ndio maana Katekista aliruhusiwa kuendesha hiyo ibada!!HAKUNA UTATA HAPO
 
Hili kanisa limegubikwa na kashfa dunia nzima ya maaskofu wake kubaka watoto miaka na miaka, mpaka juzi askof mkuu wa marekani kavuliwa uaskofu. Ni barani Afrika tuu vijana waliolelewa ndani y kanisa na seminari zao hawajajitokeza kulishitaki kwa kulawitiwa wakiwa mashuleni, etc Nadhani ni sababu ya mila za kiafrika, hatusikilizi wanyonge. Lakini mtu mwenye kujielewa hatajihusisha na hili kanisa. Hatujui matakwa ya Ruge yalikuwaje. Hatujui uhusiano wao na huyo aliyeendesha misa. Watazania tujifunze kumind our own business..
You are surely a poor and bad teacher.
 
Kama hujauona umuhim wa Ruge mpka dakika hii mm na ww nan mwenye akil mgando!?

Mtu aliegusa na kunyanyua vijana wengi....alieinsipire vijana kufanya kaz kwa bidii na kujipatia kipato

Mtu alietambua, kuvumbua vipaji vya wasan almost wote hapa tz na kuwasimamia ad wakawa na majina makubwa bado unamfananisha na bab yako!?

Kupitia yy ndo leo tunaiona THT inayozalisha vijpaji vya uimbaji bado unalalamika huon thaman yake

Kuna meng kafanya huyu jamaaa bahat nzur sio ktu wa shobo kutaka ajulikane kila kitu

Ww umegusa maisha ya vijana wangap apo mtaan kwako!?
Achen roho mbaya mwachen Ruge apewe heshima anayostahili

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani ww inaonekana Afisa wa Serikali akikuomba Boga lazima utampa maana inaonekana serikali ikisema kitu ni sahihi....

Goodlucky
 
Tena kuna wafia dini wa ajabu sana, Biblia zipo, maandiko yapo, mafundisho yapo, mfano mzuri ni kuhusu ibada za masanamu, watu wanawaaminia sana binaadamu, wanamtumikia shetani wakiaminishwa ni Mungu, bila wenyewe kujijua, sisi Wakatoliki tuliojitambua, tunamwelewa sana mtu kama Ruge kukataa ujinga ujinga fulani in the name of Catholic Church, zimewekwa sheria kibao ati usipofanya hivi, siku ukifa hatukuziki!.
Tena kitu cha ajabu ni wanafanya Cherry picking, kwa kuangalia status.
Angalieni msiba huu wa kigogo huyu walifanya nini na sikilizeni rais Magufuli alisema nini juu ya mtu huyu na bado alizikwa kwa heshima zote za kanisa, tena kwenye Hilo mimi meshauri
"Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?" - JamiiForums
P
Hujalazimishwa kuwa mkatoliki. Kenge wewe! Ruge aliishi kihuni huni tu, halafu unataka apate heshima ya misa ya mazishi?
Inawezekana we jamaa ni wa dhehebu la aic au la ng'wanamalundi. Usilinganishe kanisa katoliki na vitu vya kijinga.
This is Catholic Church; the universal church.
 
Kumbe Waroman wanalilia kuzikwa na Mapadre kwa kuwa wanaamini Padre anaweza kumuombea mtu aliekufa akasamehewa dhambi
Zingatia: Misa za Wafu
Martin Luther kuondoka katika kanisa hakukosea
Mtu akiishakufa kinachotakiwa ni kuusitiri mwili kaburini. Kuna watu wanaamini uongo kuwa kwa maombi ya viongozi wa dini yanaweza kumuepusha marehemu na adhabu au mustakabali wa ama aende mbinguni au aende motoni. Mustakabali ni wapi mtu ataenda unajengwa mtu anapokuwa hai. Ukishakufa hizi nyingine ni mbwembwe tu.

Juu ya wafu huenda wapi baada ya kufa, jibu lake linatolewa na Yesu mwenyewe katika Yohana 5:28; “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.” Yesu hapa anasema watu waliokufa wanabakia hapo hapo walipofia (kama haikuwezekana kuwazika) ama wanabakia makaburini (kama iliwezekana kuwazika) hadi yeye mwenyewe atakaporudi, bila kujali kama wanastahili hukumu ama wanastahili uzima wa milele.

Hakuna kinachofanyika sasa kwa watu waliokufa. Wanapumzika wakisubiri kufufuliwa siku ya mwisho. Siku hiyo Mungu atakaposhuka maiti zote zitainuka na kutoka makaburini na watakaotangulia kutoka watakuwa wale wenye haki. “Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.” (Isaya 26:19) “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.” (1 Wathesalonike 4:16)

Baada ya wenye haki kufufuliwa ndipo watafuatia waovu (au wale ambao hawakumwamini Yesu). Hawa watafufuliwa kwa ajili ya kupokea hukumu yao ambayo Yesu aliwalipia pale msalabani lakini hawakutaka kuipokea kwa imani. “. . . Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.” (2 Wathesalonike 1:7-9). Sababu ya waovu kuangamizwa inatajwa hapa kuwa ni kutomjua Mungu, na kutotii injili ya Bwana Yesu.

Hakuna atakayeangamizwa kwa sababu ya uwingi wa dhambi zake maana Yesu alizilipia dhambi hizo pale msalabani.Kristo alikuja duniani kulipa adhabu ya kifo kile kitakachowapata watakaokataa kumwamini. Na kwa kuwa Mungu hana sera ya kulazimisha viumbe wake kukubali anachowafanyia atakubaliana na uchaguzi wao wa kutengwa naye milele kwa maangamizo yale makuu ingawa alilipa kila kitu kwa ajili yao.

Juu ya hoja kuwa wenye waliokufa wanaendelea kuishi katika mfumo fulani unaowawezesha kuwasiliana na walio hai au kujua kinachoendelea katika maisha ya wanadamu, Maandiko Matakatifu yanapinga dhana hiyo. “Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.” (Mhubiri 9:5). Na kwa kuwa Yesu alisema waliokufa wanaendelea kukaa makaburini hiyo inaondoa uwezekano wa wao kuendelea kuishi. Ili binadamu aweze kuishi kunatakiwa muunganiko wa vitu viwili; kiwiliwili na pumzi ya Mungu. “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” (Mwanzo 2:7). Kifo kinapotokea pumzi hutoka na kiwiliwili kukosa uhalali wa kuendelea kuishi. “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.” (Zaburi 146:4)

Dhana kuwaa mtu anapokufa anaendelea kuishi zinalenga kuwafariji wafiwa kwa kuwapunguzia uchungu, ama zinalenga kuwahadaa wanadamu. Maana wengine kwa kutumia dhana hizo wamewatoza wafiwa wakiwaahidi kuwaombea marehemu wao na kuwatoa sehemu ya mateso. Njia sahihi ya kukabili uchungu wa kuondokewa na marehemu ni kukubali kuwa amekufa na hajui lolote na Mungu ndiye atakayeamua pa kumweka siku hiyo ya mwisho anapokuja kuhukumu wanadamu.
 
Kwa heshima zote za kiserikali na kibinadamu na mapokezi aliyopata Marehemu Ruge, Je, alisitahili kuzikwa kwa ibada kuendeshwa na KATEKISTA?

Ukitilia maanani ukaribu wa familia ya marehemu na Askofu M. Kilaini

Ujirani uliopo kijijini kati ya Askofu na Prof. Mutahaba

Mazingira ya mwamko wa kidini ya RC uliopo hapo kijijini

Ujirani na Parokia yake ya Itahwa

Ushiriki wa viongozi hao wa dini katika kuaga mwili wa Marehemu hapo Bukoba Club/Gymkhana

Mwisho wa Mwisho ibada ya mazishi ikaishia kuendeshwa na KATEKISTA ikishuhudiwa viongozi hao wa kanisa kushindwa kushiriki ibada hiyo.

Kwanza Sio utamaduni wa eneo hilo kwa mtu kama wa aina ya Mutahaba.

Mwisho wa RUGE imekuwa simanzi kubwa kwani mbwembwe za mitaani zimezimwa na KANISA lake.

The very last RESPECT imeua yote.

Mbinguni ni makao mema ya heri na furaha (2Kor 5:1, Ufu, 2:17). Waendao mbinguni ni wale wanaokufa katika hali ya neema ya utakaso na urafiki na Mungu na waliotakaswa kikamilifu. Pia Kanisa haliwezi kumpeleka Kanisani kwa Misa ya mazishi maana alikuwa haendi Kanisani na haliwezi kumtupa kama mpagani kabisa. Kanisa linamtumia Katekista afanye ibada kwenye maziko.
 
1. Sala ya Toba anaongozwa mtu???
2. Huyo anaeongoza Una uhakika yeye hana Dhambi??
3. Yule mnyang'anyi aliesulubiwa na Yesu msalabani lakini akatubu na kusamehewa dhambi alitubu moyoni au alisubiri mtu aje amuongoze kwa sala??
4. Wewe mwenyewe unapaswa kufanya Toba na Mola wako. Askofu, Mchungaji,Sheikh hana Mamlaka ya Kumuombea mtu msamaha
5.mtu akishakufa Kumbukumbu yake imesahaulika hata aje Paroko kumuombea hakuna kitu.
6. Hizo misa za kuwaombea Marehemu mnajisumbua tu. Nipe fungu la Biblia linalotaja Marehemu waombewe
 
Hujalazimishwa kuwa mkatoliki. Kenge wewe! Ruge aliishi kihuni huni tu, halafu unataka apate heshima ya misa ya mazishi?
Inawezekana we jamaa ni wa dhehebu la aic au la ng'wanamalundi. Usilinganishe kanisa katoliki na vitu vya kijinga.
This is Catholic Church; the universal church.
Ndugu yangu Mkuu The Invincible, hakuna haja ya kutukanana "kenge wewe" na kuwahukumu marehemu wa watu, waachwe wapumzike, anayetoa huku ni Mungu mwenyewe, na hivi vitu ninavyowaambia hapa nyinyi wafia dini, usiviite vya kijinga, kwa sababu haya ninayoyazungumza humu ni mafundisho yake YEYE mwenyewe, ametufunza, "Tutaokolewa kwa neema na sio kwa matendo", hivyo hata mtu awe aliishi kihuni vipi na kanisa kugoma kumzika kwa heshima zote, wakovu haitokani na matendo yake bali ni neema tuu. Na wote wanaozikwa kwa sala na misa Takatifu, sio kigezo kuwa wao ndio wataenda mbinguni.
Mwacheni Ruge apumzike, tusinyooshe vidole na kumhukumu kwa maisha yake, yale ni maisha yake, ajuaye ya mbele ni Mungu pekee.
P
 
Kwa utaratibu Dhehebu la katoliki kama huna ndoa ya Kanisa na hushiriki Sakramenti Takatifu na Jumuiya ndogo ndogo ukifa huwezi kusomewa misa na Baba Padri. Huo ndiyo utaratibu wa dhehebu la Katoliki na hauwezi kuvunjwa na mtu yeyote na hapa hakuna urafiki hata Baba Askofu awe rafiki yako atafuata tu sheria.
 
Ndugu yangu Mkuu The Invincible, hakuna haja ya kutukanana "kenge wewe" na kuwahukumu marehemu wa watu, waachwe wapumzike, anayetoa huku ni Mungu mwenyewe, na hivi vitu ninavyowaambia hapa nyinyi wafia dini, usiviite vya kijinga, kwa sababu haya ninayoyazungumza humu ni mafundisho yake YEYE mwenyewe, ametufunza, "Tutaokolewa kwa neema na sio kwa matendo", hivyo hata mtu awe aliishi kihuni vipi na kanisa kugoma kumzika kwa heshima zote, wakovu haitokani na matendo yake bali ni neema tuu. Na wote wanaozikwa kwa sala na misa Takatifu, sio kigezo kuwa wao ndio wataenda mbinguni.
Mwacheni Ruge apumzike, tusinyooshe vidole na kumhukumu kwa maisha yake, yale ni maisha yake, ajuaye ya mbele ni Mungu pekee.
P
Haya baba nimekusikia.
 
Kwa heshima zote za kiserikali na kibinadamu na mapokezi aliyopata Marehemu Ruge, Je, alisitahili kuzikwa kwa ibada kuendeshwa na KATEKISTA?

Ukitilia maanani ukaribu wa familia ya marehemu na Askofu M. Kilaini

Ujirani uliopo kijijini kati ya Askofu na Prof. Mutahaba

Mazingira ya mwamko wa kidini ya RC uliopo hapo kijijini

Ujirani na Parokia yake ya Itahwa

Ushiriki wa viongozi hao wa dini katika kuaga mwili wa Marehemu hapo Bukoba Club/Gymkhana

Mwisho wa Mwisho ibada ya mazishi ikaishia kuendeshwa na KATEKISTA ikishuhudiwa viongozi hao wa kanisa kushindwa kushiriki ibada hiyo.

Kwanza Sio utamaduni wa eneo hilo kwa mtu kama wa aina ya Mutahaba.

Mwisho wa RUGE imekuwa simanzi kubwa kwani mbwembwe za mitaani zimezimwa na KANISA lake.

The very last RESPECT imeua yote.
Matendo ya Mungu si ya mwanadamu amestahili alichopata kulingana na ushiriki wake katika mambo ya kiroho... Alichopata kinaitwa minimum service

Jr[emoji769]
 
Pole nyingi sana kwa Zama na watoto wake, mapito anayopitia kwakweli ni Mungu tu ndio anajua.
Iliwahi kunitokea aisee nikaachiwa mtoto wa miaka miwili yaan sijawahi kusahau mpk leo. Nilikuwa naona kila kitu kibaya, nilitamani ht niache kazi ili niwe najifungia tu ndani.
Nikiona picha ya Zama na watoto wake nakumbuka kbs jinsi ilivyokuwa kwangu na mtoto wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Oooh pole mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msianze...
Kinachomuingiza binaadamu mbinguni au motoni, sio misa yako ya wafu imeendeshwa na nani, au watu wamekulilia vipi, bali tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo.

Kwa mujibu wa the law of the karma, Ruge as of now, ameingia peponi straight kwa mengi mengi aliowatendea watu hapa duniani.

Siku ukifika mbinguni, unaweza kushangaa kuwaona hao maaskofu motoni, halafu yule Katekista ndio ukamkuta peponi.

Hata kimataifa, unaweza kumkuta Bush, Blair na Obama, upande wa chini wakiogelea kwenye lile ziwa la jehanum ya moto was milele, halafu ukashangaa kuwakuta Osama, Saadam na Ghadafi wakiwa peponi wakienjoy.
P
-1.Usiingize karma wakati issue ni christianity
-2.Afadhali yaliyomkuta Ruge amepata katekista kuliko yalimkuta tajiri wa ngurudoto(waligoma kumzika kisa ushiriki wake kanisani)
 
Back
Top Bottom