TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Hii imenishangaza sana kwa kweli wahaya wameanza ujenzi wa kaburi leo mazishi siku tatu zijazo mbona mapema sana au litakuwa la ghorofa? au litakuwa lina underground
Kwani kuna ajabu gani kujenga mapema?

Ughaibuni kuna makaburi yanachimbwa kabla hata atakae zikwa hajulikani. Yanauzwa.

Mafarao walijenga makaburi kwenye pyramid miaka kibao kabla.

Njombe kuna mganga wa tiba za asili kajenga kaburi lake la gharama tena ghorofa na underground kabla hajafa wala kuugua anasema anataka liwe la makumbusho.

Usikariri mazoea au mila ya sehemu flani ukadhani kwa wengine kuna ubaya kutofuata hayo mazoea au mila.

Kupanga ni kuchagua. Hakuna madhara yeyote zaidi ya faida kwa kujenga mapema kupunguza vurugu siku ya mazishi kama kuna mabadiliko ya vipimo n.k.
 
Nyumba yake au nyumba ya kupanga, wenye nyumba wengine hawaruhusu wapangaji kuhani msiba kwenye nyumba zao.
Kimsingi jamaa angekuwa anaishi kwenye nyumba yake mwenyewe ya kujenga au kununua, au hata kupewa na wazazi, msiba ungetakiwa uwe hapo. Tatizo sio hivyo
 
Tuseme.kweli hakuna kijana alokuwa anawasaidia wenzake kama Ruge,

Akina diamond muda huu wanajifanya hawakupata mchango wowote kwake lakin Mungu ndo anajua
Naona Diamond na wasafi wake wametoa nyimbo ili watu watoe concentration Kwa msiba wa Ruge Ila cha ajabu msiba unatrendi kila kukicha na mkono wa serikali unazidi kuhisaport

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachoendelea ni sahihi, maana msiba upo kwa wazazi wake. Hata kama angekuwa na familia kwa kuwa wazazi wake wapo msiba unakuwa kwa wazazi.

Ila wazazi kama wangekuwa wamefariki sawa msiba kuwa kwake.
 
Hapo kweli kuna cha ajabu,mimi nilivyoona tweeter ya Rais nikaweka cloud plus waliweka tangazo lao la changia matibabu.nikajiuliza hii clouds plus ni yao au kuna nini.
Kuna watu walitaka waendelee kuchangisha dinari hata baada ya mtu kufariki
 
Hajawahi kuwaona wakenya na wanigeria huyo.

Mi sioni kama kujisifia ni dhambi useme Tu wahaya wakijisifia wanajiona inferior mbele ya wahaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachoendelea ni sahihi, maana msiba upo kwa wazazi wake. Hata kama angekuwa na familia kwa kuwa wazazi wake wapo msiba unakuwa kwa wazazi.

Ila wazazi kama wangekuwa wamefariki sawa msiba kuwa kwake.
Sio kweli, tatizo jamaa hakujenga hapa mjini na alipokuwa anaishi ni nyumba ya kupanga,wenye nyumba za kupanga wengi hawataki wapangaji kuweka misiba kwenye nyumba zao
 
Na hili nalo kwako lemekua nongwa,,!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…