TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Juzi KKKT waligoma kumzika kaka yangu kapuku kisa tu hana ndoa sasa nasubiria kuona wakimzika hadi na askofu kisa tu Ruge ni tajiri...lets stay eye opened

mmmh wakimzika utafanyaje ? kama amebatizwa na ameishi kwa kufuata sheria zote za dini ana haki zote
 
Ndugu wananchi, tuna msiba mkubwa leo umetokea hapo kusini mwa Africa,........Poleni sana wa-Tanzania wote. ndugu, jamaa na marafiki, hasahasa kwa dada yangu Zamaradi Mtetema, wewe bado mdogo ki-umri, kiumbo nk, naamini Mungu atakusaidia kuyashinda haya magumu unayopitia kwa sasa....tuko pamoja na mimi ndo mfariji wako mkuu, sitakuacha kamwe amini ivo nakupenda sana na pia ni mtu wangu wa karibu, pengo ntaliziba kwa gharama yeyote ile. wote tulipitia kipindi hiki kigumu na wengine wengi wanapitia sasa,na wewe leo wapitia hapa.usishangae au kuumia sana. haya yameumbwa na mpaka leo tunaishi Mungu akupe wepesi...KOSA LA RAIS ALITAKIWA KUREKEBISHA HARAKA SANA. ''HAJATOA POLE KWA WATANZANIA WAKE, WAPIGA KURA WAKE, AMEWASAHAU AU HAJAWAJALI KATIKA MSIBA HUU MKUBWA WA KITAIFA.
 
Furaha kwa zama
Mateso yanakuja
Roho itaumia sana
Watoto wakija kuwa wakubwa watamuuliza maswali mengi ambayo atakosa majibu
Kama aliwapa watoto nafasi ya kwenda kumuona baba yao basi itakuwa salama kwake
What goes around comes around!
Tamaa inatuponza sana wanawake.
 
DAR ITAMUAGA JUMAMOSI: ATAZIKWA BUKOBA. Ndugu Kashasha ambaye ni msemaji wa Familia ya Mutahaba amesema kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa #RugeMutahaba utawasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya IJUMAA (March 1/2019). Ikiwa hivyo wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga mpendwa wetu siku ya JUMAMOSI (March 2/2019). . . Baada ya hapo: Familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya JUMATATU (March 4/2019) (Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba)
 
Too sad,pumzika kwa amani kaka,mwenyezi Mungu akupe pumziko la Amani.Binafsi nilikuwa naona mchango wako mkubwa katika tasnia ya habari hapa Tanzania.Nawapa pole wanafamilia wote na clouds group kwa ujumla.Hiyo ni safari yetu sote,mbele yetu nyuma yako.RIP RUGE
 
Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa ya Machi 1,2019 na utazikwa Bukoba, mkoani Kagera wiki ijayo.

Akizungumza leo Jumatano Februari 27, 2019 nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam, msemaji wa familia Annik Kashasha amesema taratibu za kuuleta mwili zimeanza kufanyika kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa.

“Mwili wa marehemu utarejeshwa hapa nchini siku ya Ijumaa (Machi 1) na siku ya Jumapili (Machi 3) utasafirishwa kwenda Bukoba kwaajili ya mazishi.

Kashasha amesema shughuli za kumuaga Ruge ambaye ni mwanzilishi wa semina za fursa zitafanyika siku ya Jumamosi.
 
Back
Top Bottom