Mtoa mada... Ulishawahi uguza ndugu yako wa karibu,jamaa au rafiki???
Kwenye matibabu iko hivi,hasa tatizo alilokua nalo marehemu Ruge,huwezi fanya surgery ya kidney plant kama mgonjwa pressure yake ipo juu sana..
Na hii labda ndiyo tatizo lililokua linamsumbua marehemu Ruge hadi wakashindwa kumufanyia,walikua wana control pressure ishuke then wafanye mambo....
Mwaka juzi nilipoteza kaka yangu pale Bugando hospital,alipata stroke, pressure ikapasua mishipa ya damu kichwani,akazima for seven days,siku ya nane akafariki....
Kila wakitaka mpeleka kwenye chumba cha upasuaji,pressure iko juu,wanashindwa mpasua,wanaanza control pressure...
Ogopa sana, mtu kama Ruge alipatwa na majanga haswa kutoka serikalini na kwa mpenzi wake Zamaradi
1. Kuvamiwa Clouds Fm na rafiki yao mkubwa,halafu mamlaka za juu zikamwacha mvamizi wake,bila yakumpa adhabu yoyote... Hapa alipata maumivu makubwa sana,hakuamini macho yake,kama serikali ya ccm inayotumia kituo chake kwenye propaganda zao leo hii wamekua watesaji wake...
2. Kuachwa na mzazi mwenzake Zamaradi na kwenda kuolewa sehemu nyingine,Ruge alijaribu kuomba samahani kwa mwenzake hadi akawa analia,yule mwanamke alikua ana mrekodi,akaitoa audio na kuisambaza,hapa napo aliumia...
Serikali kuzuia matamasha yake,mara vile anaandaa tamasha,dakika za mwisho ananyimwa kibali,walikua wapi kumunyima tangu mwanzo,kaingia gharama kiasi gani kuandaa hilo tamasha? Je wa zamini wataendelea fanya kazi na Ruge tena???
Pumuzika kwa Aman kaka Ruge...
Sent using
Jamii Forums mobile app