Mkuu wa mkoa amefika eneo la tukio na kuwafariji wafiwa, na pili kukutana na wazee wa kamati ya msiba na mazishi inayoongozwa na Profesa Kazimoto,
Kawahakikishia ulinzi wa kutosha maeneo hayo,
Pamoja na kwamba Ni kijijini lakin mwamko umekuwa mkubwa mno,
Mpaka sasa wameshafika watu wa kulala eneo la tukio zaid ya 200 suala ambalo linaleta mkanganyiko kwamba kama wa kulala ni hawa je hapo kesho mpaka jumatatu itakuwaje,
Aidha mzee Masabala na Jamal Kalumuna wamesimama shughuli yote kwa umakini,
Kuhakikisha hakuna jambo linaloenda vibaya,
Kwa taarifa zisizo rasmi ni kwamba kila atakaye udhuria atapewa huduma kama malazi na kula,
Majirani wameomba kwamba shule ya sekondari na ya msingi kabale zilizo karibu na Kwa mzee mutahaba zitumike kwa ajili ya watu watakaotoka mbali,
Maana vijiji vinavyozunguka eneo husika vinatarajiwa kuwa na wawakilishi,
Kuanzia
Kabale yenyewe, Kitwe, Rwakagongo, Kasheya, Itahwa ,magoti, Maruku, Bwara, Kagondo, Kagege
Hao wote wanategemewa kuwa na wawakilishi,
Pia vijana wamemuomba mwakilishi kwa Clouds FM kwamba wafunge mitambo ya kuonesha matukio moja kwa moja kutoka Bukoba, alafu wananchi wa Bukoba mjini wapunguze msongamano eneo la tukio badala yake waende viwanja vya Gymkhana-Bukoba, na Kaitaba,
Hii itapunguza msongamano wa magari na watu,
Aidha wasanii mbali mbali wanatarajiwa kufika eneo husika, na watu maarufu wakiwemo viongozi wa kitaifa
Ulale salama kaka Ruge
Chanzo nipo eneo la tukio,
Nipo na mwakilishi wa Clouds FM, wa Ayo tv na global TV