TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Kama wewe huoni mchango Wa Ruge ni wewe usilazimishe sisi tulioona mchango wake tuseme hatujaona. Neno unafiki siku hizi naona linatumika ndivyo sivyo, yaani kwamba Mimi kama nimeona mchango wake nikisema alikuwa Na mchango mkubwa hiyo inakuwa ni unafiki, Ila wewe ukisema hukuona mchango wake hiyo inakuwa sio unafiki. Pathetic!!!

I rest my Case....
 
Good opinion but one thing it's lacking sense[emoji4]
Watanzania kwa ujumla wetu tumejumuika katika tukio la kuomboleza kifo cha mkurugenzi wa Clouds media, Ruge Mutahaba. Nawapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

Tukiweka unafiki pembeni, tukio la kifo cha Ruge limekuzwa mnoo. Ruge hakuwa mtu maarufu sana Tanzania (japokuwa amefanya mambo mengi makubwa), hakuwa mwema sana na wala hakuwa mtu muhimu sana kwa watanzania walio wengi.

Kila kitu kuhusu maombolezo ya msiba wake kinaonekana kupangwa, kuratibiwa na hata kugharamiwa kwa karibu mnoo na serikali. Tunaambiwa hata tangazo la kifo chake ilibidi itifaki ya ikulu itumike ili rais atangaze kifo chake. Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu naye waliopata taarifa za kifo chake waliambiwa wakae kimya kwanza (walifichwa taarifa?) mpaka rais alipotangaza.

Sote tunajua Ruge alikuwa ni mfanyabiashara na kila alichokuwa akikifanya kwenye jamii kilikuwa kimelenga biashara zake kwa 100% hata kama alikuwa akikifunika kwa koti la kijamii. Waliowahi kufanya kazi naye wanajua hilo, na hakuwa na mchezo mchezo katika kufanya biashara zake. Huo ndio ukweli.

Watanzania wote wanalazimishwa kusema mema ya Ruge, kushiriki kuomboleza kifo cha Ruge na kulipia gharama za mazishi yake kama msiba wa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Sidhani kama jambo hili lina afya sana kwa taifa letu huko tuendako, maana nadhani kila mtanzania angetamani naye siku moja ndugu, jamaa au rafiki yake atakayefariki njia hii hii itumike kwake ili kufuta majonzi na kumpa faraja.

Bado sijajua kwanini hili la kufa na kuzikwa kwa Ruge limelazimishwa kuwa tukio kubwa la kitaifa, lazima kuna sababu, nadhani huenda ipo siku tutaambiwa kinagaubaga.

Ruge hayupo tena, tuliompenda na waliomchukia tumeendea kuwepo, tukishamaliza kumzika turudi na kuendelea na maisha yetu.
One of the richest guy in South Africa sends his condolences and you will still say its overrated.
Screenshot_20190304-084035.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAZO ZURI SANA, ILA TAMBUA KILA MTU ATAZIKWA NA UMATI WAKE, IKIWA YEYE KAZIKWA AU KAKUZWA HIVI ISIKUUMIZE SANA KICHWA MAANA HUJUI ALIKUWA NA MSAADA GANI KWA HAO WANAOMLILIA, NA ISITOSHE TUSIPENDE KUTEMBEA NA RATIBA BINAFSI ZA MISIBA YA WATU WENGINE KICHWANI, USIJENGE TASWIRA YAKUTAKA MSIBA HUU UWE HIVI UWE VILE, AMA MTU HUYU AZIKWE HIVI AU VILE, KIKUBWA TUNAPENDA KUWA MAJAJI WAZUURI SANA WA MAKOSA YA WENZETU LAKINI PIA TUNAPENDA KUWA MAWAKILI HODARI SAN WA MAPUNGUFU YETU, UNAFIKI NI PALE UNAPOTAKA MTU ATENDEWE KWA MABAYA YAKE ANGALI MAZURI YAKE UNAJIFANYA HUYAONI, NA ISITOSHE YY HAKUWA MALAIKA ANA MACHAFU YAKE PIAH, SWALI NI KUWA KWANINI UMJAJI KTK ENGO HIYO TU AS IF TOKA AMEZALIWA HADI UMAUTI HAKUNA ZURI ALILOFANYA????? UKIULIZWA AMEKUUMIZA NA NN??? HUNA JIBU, AMEKUDHULUMU NN?? HUNA JIBU, NA UKIULIZWA KWAKO WEWE AMEKU IMPACT AU KUKUZUIA USIPATE UGALI WAKO?? HUNA JIBU ILA KWA KUWA NI MOYO MTUMBA USIOPENDA KUHOJI HUYU MTU AMESHWAHI NIUDHI? HAPANA, KUNITUKANA?? HAPANA, ILA KWA KUWA TUNAPENDA KUANDIKA KWA KUSIKIA SIKIA NDIVYO MAISHA YA MTANZANIA WA KIZAZI HIKI. TUNAPENDA KUTEMBEA NA MTIZIMO YETU MIFUKONI NA KUJAJI HATA WALE USIOWAJUA KIUNDANI, RUGE SIO MSAAFI SANA ILA MWACHENI APATE HESHIMA YAKE HATA KAMA MACHONI KWAKO HUONI KAMA ANASTAHILI UNLESS OTHERWISE WEWE UTAKUWA NDIO MNAFIKI UNAYETAKA UNACHOWAZA KIWE HIVYO, AND NOT KILA FAMOUS PERSON WEWE UMJUE SIO LAZIMAA SANAAAA MAANA DUNIANI TUKO WENGI ASA WATAFAHAMIKA WANGAPI, PUNGUZA HARD FEELINGS MZEE, KAMA UNAPENDA KUWA FAMOUS NA WEWE PIAH TUTAKUZIKA TU MAANA NJIA YETU NI MOJA PIAH.

bravo
 
Kama wewe huoni mchango Wa Ruge ni wewe usilazimishe sisi tulioona mchango wake tuseme hatujaona. Neno unafiki siku hizi naona linatumika ndivyo sivyo, yaani kwamba Mimi kama nimeona mchango wake nikisema alikuwa Na mchango mkubwa hiyo inakuwa ni unafiki, Ila wewe ukisema hukuona mchango wake hiyo inakuwa sio unafiki. Pathetic!!!
Unataka kuniambia mchango wake kwa vijana alikua anufaiki nao(maslai)?????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wana nature ya ujinga na uvivu wa kujifunza au kujielimisha na kupata taarifa sahihi juu ya jambo lolote kwa kutumia akili binafsi katika haya maisha.

Wanapoona jambo au kusikia kitu, hatua yao ya kwanza ni kutazama wengi wamereact vipi ili nao wafanye the same reaction. Kwa kifupi ni mabendera fuata upepo. Ni wavivu kushirikisha vichwa vyao katika kutafakari maisha na namna zake.

Ndio maana usishangae inshu kama kilimo cha matikiti, wanafunzi wa chuo kuchagua ualimu, magraduate wa chuo kukimbilia jeshini ili watoke kimaisha, inshu ya kikombe cha babu wa loliondo na mengineyo mengi ni matokeo ya watanzania ya kutokufikiri kwanza ila kukurupuka kwa kufuata mkumbo.

Tabia ya kufuata mkumbo huwa ni tabia ya watu wanafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom