Mkwe ulishawahi kushangaa kitu mpaka ukaona aibu!
Natoka home nimevaa zangu tight na blouse , mdada wangu ananiambia mama si uvae kama dera flan hivi msibani utaendaje na tight, namuuliza msiba upi dada? anajibu si huu wanatangaza kwenye TV!
Niko zangu saluni nakata panki langu, naambiwa naona unajipiga sop sop uende msibani,
Nakuta foleni barabarani naambiwa oh wametoka kumpokea mwili unafika leo
Nafika kazini mtu ana nguo nyeusi oh msibani!
Naenda canteen nakuta watu wanaonyeshana video za mwili ulipowasili!
HAPO NIKASHTUKA
nikajiuliza hivi mimi niko sawa kweli, mbona kama NIKO DUNIA AMBAYO WENZANGU HAWAPO!
nikajitafakari kwanini nimepokea tu kuwa ni msiba na nikamuombea na kuendelea na ratiba zingine?
nikajikuta pengine sina tatizo!
PENGINE IT WAS MEANT TO BE THAT WAY!
basi nikajikubalia tu kuwa sijaelewa na sio lazima nielewe kila kitu.