Watanzania wengi tu Wanafiki sana, ni Watu tunaishi kwa sura mbili, mbele ya Mtu na nyuma ya mgongo wake.
Mtu akiwa na matatizo tunashabikia mitandaoni ili hali najua kabisa ni nyie nyie mkiwa macho kwa macho mtatoa na machozi kujifanya mnamuhurumia.
Juzi mlikuwa mnamkebehi Ally Choki, siku kadhaa baadae nikakuta Watu wanashangilia kilichokuwa kinasemekana kuwa ni kijana mdogo amemtukana Baba yake Mzazi mtandaoni.
Hivi ukiwakusanya hao woote waliokuwa wanashangilia matusi ya Mtoto yule na uwaulize kama wanaweza kupita njiani wakamkuta Mtoto anamtukana Mtu mzima achilia mbali kama huyo Mtu mzima ni Mzazi wake ama la, je watasimama pembemi na kushangilia au wangemuadhibu Mtoto yule?
Nina uhakika Watu 9 kati ya 10, kama sio wote watakwambia tutamfunza adabu Mtoto yule...sasa mbona mitandaoni/nyuma ya mgongo tupo tofauti?
Na ndio maana hata wakati ule mlimchuuza yule Dada yenu kuhusu maandamano lakini ilipokuja kwenye siku ya vitendo mikia ikaingizwa makalioni kama Mbwa koko.
......WANAFIKI.....