RUGE tuamuangalie upande wa pili

RUGE tuamuangalie upande wa pili

Gulwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2008
Posts
10,597
Reaction score
16,394
Tangu kutokea msiba wake sifa lukuki zimekuwa zikitolewa kuhusu maisha na kazi zake ambazo nyingi ni za kweli. Lakini kama tujuavyo hakuna binadamu aliye mkamilifu hivyo ukitaka kumuelezea mtu halisi lazima na upande wa mapungufu yake uyagusie.

Kwangu mimi Ruge licha sifa zote , hakuwa mfano wa kuigwa kwa maisha ya kijana na nitaeleza sababu zaangu.

Ruge amefariki akiwa na umri wa miaka 49 lakini hakuwa na maisha ya familia, kwa maana ya mke na watoto.

Ameishi maisha ya kihuni yasiyofaa kuigwa kwa vijana wanaotafuta kuishi vizuri. Ruge angekuwa ni mtu aliyefanikiwa kimaisha, msiba wake ungekuwa nyumbani kwake na sio kwa wazazi wake.

Vijana wengi alioibua vipaji vyao japo wengi wamefanikiwa kupata pesa lakini wengi wao wanaishi maisha ya kihuni.

Ndoa zao zimeshindikana na wamekuwa watu wa kuonyesha vitendo vya aibu katika jamii. Hili nalo naweza kulihusisha na Ruge kwani mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake.

Zipo pia tetesi kuwa hata pale Clouds wafanyakazi wengi wanajihusisha na vitendo vya kishoga na kwa msemo wa kiswahili kuwa lisemwalo lipo, huenda likawa na ukweli ndani yake na Ruge akawa ni sehemu ya jamii hiyo.

Nimalize tu kwa kusema Ruge amejitahidi katika sehemu moja ya maisha na kufanikiwa, kiuchumi, ila upande wa pili wa maisha , kimaadili, hakufanikiwa hata kidogo.

Kama binadamu mwenye imani kiasi, namwombea kwa muumba wake aipumzishe roho yake mahali zinakopumzishwa roho zote , Amen
 
Hizo ni standards ambazo zimewekwa na binadamu tu sijui ukifika umri fulani lazima uoe, Ruge kasoma Marekani na kama ujuavyo tatizo la divorcee lilivyo kubwa US esp ukiwa kwenye entertainment industry nadhani hiyo pia ilimuathiri.
Ukitaja rapper mmoja aliyeoa mimi nataja marapa watano ambao wako single
 
Gulwa hoja yako ni ya msingi sana. Ni ukweli usiopingika yapo mambo mazito ambayo hatupendi kuwa wakweli kuhusu upande wa pili wa huyu ndugu... Ukiangalia kwa undani upande wa pili 'leaves a lot to be desired' Mtu ambaye ana umri huo hana hata familia unajiuliza anawezaje kuwa role model? Watu wengi wanashabikia mambo bila kutafakari kwa undani. Hatuwezi kumhukumu maana hiyo ni kazi ya Mungu lakini ukiangalia hao vijana aliowasaidia wengi hawana msingi imara kama kiongozi wao alivyokua
 
Hizo ni standards ambazo zimewekwa na binadamu tu sijui ukifika umri fulani lazima uoe, Ruge kasoma Marekani na kama ujuavyo tatizo la divorcee lilivyo kubwa US esp ukiwa kwenye entertainment industry nadhani hiyo pia ilimuathiri.
Ukitaja rapper mmoja aliyeoa mimi nataja marapa watano ambao wako single

Guccimane,Ice Cube,Snoop Doggy,Jay Z,Dr Dre.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom