RUGE tuamuangalie upande wa pili

RUGE tuamuangalie upande wa pili

Wee bwege kuoa sio lazima ndorobo weee watoto zake 5 wanatosha
Gulwa hoja yako ni ya msingi sana. Ni ukweli usiopingika yapo mambo mazito ambayo hatupendi kuwa wakweli kuhusu upande wa pili wa huyu ndugu... Ukiangalia kwa undani upande wa pili 'leaves a lot to be desired' Mtu ambaye ana umri huo hana hata familia unajiuliza anawezaje kuwa role model? Watu wengi wanashabikia mambo bila kutafakari kwa undani. Hatuwezi kumhukumu maana hiyo ni kazi ya Mungu lakini ukiangalia hao vijana aliowasaidia wengi hawana msingi imara kama kiongozi wao alivyokua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marehemu hasemwi, kama una mabaya yake kaa kimya na kama una mazuri yake sema.. hatufanyi vyema kwa kutangaza mabaya ya watu
Sio kwel mzee.Marrhemu hasemw mabaya yake binafsi amabayo hayana athari katika jamii.ila kama yameacha athari mbaya katika jamii,lazima yabainishwe.Ili watu wasiyafanye.Usitufunge kama mzeeeeeee.
 
Kwani maadili ni nini ? Maana kuna watu wana ndoa lakini ndio wezi wakubwa WA Mali ya umma , je mnasemaje kuhusu Hilo ?
 
Hizo ni standards ambazo zimewekwa na binadamu tu sijui ukifika umri fulani lazima uoe, Ruge kasoma Marekani na kama ujuavyo tatizo la divorcee lilivyo kubwa US esp ukiwa kwenye entertainment industry nadhani hiyo pia ilimuathiri.
Ukitaja rapper mmoja aliyeoa mimi nataja marapa watano ambao wako single
La kwanza hadi form six kasoma bongo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ni standards ambazo zimewekwa na binadamu tu sijui ukifika umri fulani lazima uoe, Ruge kasoma Marekani na kama ujuavyo tatizo la divorcee lilivyo kubwa US esp ukiwa kwenye entertainment industry nadhani hiyo pia ilimuathiri.
Ukitaja rapper mmoja aliyeoa mimi nataja marapa watano ambao wako single
Ina maana Ruge alikuwa Rapper wa Kimarekani, au?! We ongea mengine bhana lakini hiyo hoja yako ni ya kitoto sana! Hakuna cha kusoma Marekani wala kuzaliwa Brooklyn!
 
Hakuwabaka but most likely, alitumia nafasi yake!! Enzi na Smooth Vibes yake, akatumia nafasi yake kumlala Jide walipoenda South Africa kwenye tuzo! Kale ka-Nandy huenda kauchi kake angekabana endapo Ruge asingekuwa pale alipokuwa!
Yes that's true
 
Tangu kutokea msiba wake sifa lukuki zimekuwa zikitolewa kuhusu maisha na kazi zake ambazo nyingi ni za kweli. Lakini kama tujuavyo hakuna binadamu aliye mkamilifu hivyo ukitaka kumuelezea mtu halisi lazima na upande wa mapungufu yake uyagusie.

Kwangu mimi Ruge licha sifa zote , hakuwa mfano wa kuigwa kwa maisha ya kijana na nitaeleza sababu zaangu.

Ruge amefariki akiwa na umri wa miaka 49 lakini hakuwa na maisha ya familia, kwa maana ya mke na watoto.

Ameishi maisha ya kihuni yasiyofaa kuigwa kwa vijana wanaotafuta kuishi vizuri. Ruge angekuwa ni mtu aliyefanikiwa kimaisha, msiba wake ungekuwa nyumbani kwake na sio kwa wazazi wake.

Vijana wengi alioibua vipaji vyao japo wengi wamefanikiwa kupata pesa lakini wengi wao wanaishi maisha ya kihuni.

Ndoa zao zimeshindikana na wamekuwa watu wa kuonyesha vitendo vya aibu katika jamii. Hili nalo naweza kulihusisha na Ruge kwani mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake.

Zipo pia tetesi kuwa hata pale Clouds wafanyakazi wengi wanajihusisha na vitendo vya kishoga na kwa msemo wa kiswahili kuwa lisemwalo lipo, huenda likawa na ukweli ndani yake na Ruge akawa ni sehemu ya jamii hiyo.

Nimalize tu kwa kusema Ruge amejitahidi katika sehemu moja ya maisha na kufanikiwa, kiuchumi, ila upande wa pili wa maisha , kimaadili, hakufanikiwa hata kidogo.

Kama binadamu mwenye imani kiasi, namwombea kwa muumba wake aipumzishe roho yake mahali zinakopumzishwa roho zote , Amen

Ruge is a Human being. Na amesema mwenyewe Ikitokea amekufa washeherekew Mazuri yake.

Mengi mabaya, umeweka Tetesi tu. Sijui ushoga nk.. Na pia Usidhani kila mtu atatimiza kila kitu katika Umri wake. Kama Ndoa, watoto.nk

"A 4 year degree attained after 7 years is still a degree.
A graduation at the age of 50 is still a graduation.
A Mercedes bought at the age of 65 is still a Mercedes dont let people bully you with their timelines of success."- Chris Brown.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila binadam anamapungufu yake na udhaifu wake.. wote mnaomdiss hapa mnamapungufu yenu pia yasiyofaa kuigwa na jamii.. Fateni yale mazuri aliyoyafanya hizo bullshit zingine achaneni nazo

kikubwa alichokua akikifanya ni kuwasaidia vijana kuinuka kiuchumi na kuwapa fikra za kimaendeleo na ndo kilichompa umaarufu. wala maisha yake binafsi hayajawahi mpa umaarufu kwanza hajawahi kuweka hadharani maisha yake binafsi wala mahusiano yake au familia yake au watoto wake alikua hataki kabisa kuvizungumzia kwenye media ni sisi ndo tunataka kuyachimba sana

Mambo ya vijana wa clouds kua sijui mashoga hayo ni maisha yao binafsi na ni uamzi wa mtu au mlitaka aanze kucontrol na maisha yao binafsi na tabia zao? Mbona clouds wapo vijana wengi tu waliooa na wadada walioolewa wanafamilia zao, na wanajiheshimu na boss wao hajaoaa?

Swala la yeye kuoa au kutooa halituusu chochote kwanza haya mambo ya mahusiano ni kitendawili huwezi jua alipitia nini mpaka hajaoa
Maana humu mitandaoni watu wanavyosema kwa uhakika ni muhuni ni muhuni Utafikiri walikua wanamsaidia kushika miguu ya hao madem wanaowataja wakati yeye anapiga pumbu.. vitu ambavyomuhusika hajawai kuviweka wazi lakini kuna watu wanajikuta wajuaaaajiiii! Acheni hizo bana hakuna mwenye uhakika kuhusu mambo yake ya mahusiano!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzaniaaaa. Kumsema mtu kwa mabaya ama mazuri yake baada kufariki sioni ubaya wowote, utasikia ana mapungu yake ana mapungufu yake lakini hivi lakini vile, sasa hayo mapungufu yasiposemwa jamii na hasa vijana watajifunzia wapi? Nyerere alieipa nchi hii uhuru anasemwa vibaya, mi sioni tatizo.
 
Nahisi hakuna jambo baya kama kuoa..tena kuoa mke mmja...ni gereza litakalokumaliza kabla ya muda wako duniani..
Tumezaliwa na mitazamo huru hasa sisi tulio huru kuchagua tunataka nn na sio makumbafu wengi/jamii inataka nifanye nn...
Kilamtu atakufa peke yake na majutio yake pekee
 
Marehemu hasemwi, kama una mabaya yake kaa kimya na kama una mazuri yake sema.. hatufanyi vyema kwa kutangaza mabaya ya watu
Umeongea vizuri sana ndio utamaduni wetu sote narudia ndio utamaduni baadhi ya watu wanajitahidi kuupoteza wengine huenda mbali na kuwa na roho mbaya kusema Mungu amuweke mahali anapojua sio sawa tumuombee kheri ndivyo ilivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliye mkamilifu ni MUNGU PEKEE, siye binadamu ni dhaifu hakuna mkamilifu. Hivyo unapomnyoshea mwenzio kidole waza pindi na wew utapoondoka utakumbukwa kwa yapi?!
 
Naunga mkono hoja. Thread hii inabalansi zile sifa za utukufu anazopewa ndugu yetu Ruge. Sio chuki wala!

Ni dhahiri jamaa kuna sehemu aliteleza. Hasa huko kwenye maadili. Watakaopinga watapinga tu kiholela lakini moyoni wanakiri maana ushahidi upo wazi wazi.

However, genius fellows ndivyo walivyo lakini. Wengi wanafeli kwenye mahusiano. Labda ni dhaifu sana eneo hilo au hawana utaalamu nalo hivyo wanababatizwa bila ya kujua.

Tuliobaki tujifunze!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom