Moto Mkubwa uliosababishwa na baadhi ya wananchi umeteketeza eneo la Mwekezaji Suba Agro katika Kata ya Kipande, Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali amesema moto huo umesababishwa na wananchi walioukuwa wakitafuta kitoweo cha Panya jirani na eneo hilo la mwekezaji analotumia kama Kitalu cha kupanda mbegu zake.