RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

Yale yale ya basata.... Hivi kwanin wasitoze faini tu mambo yakaendelea... unakuja tia watu hasara kisa utupu ambao watu wanacheza nao kila siku kweny simu zao na tv zao.

Sent from my SM-G920P using JamiiForums mobile app
Kuna tatiZo mahali. Na lisipo shuhulikiwa tutajuta na hizi Sheria za kipumbavu[emoji849][emoji848]
 
Unaifungia wasafi miezi 6

1. Unakosa mapato kutokana na matangazo yanayotakiwa kurushwa ndani ya miezi 6 ya adhabu

2. Unakosa mapato kutokana na waajiriwa wa Wasafi kupoteza kipato( marupurupu n.k)

3. Unapunguza Wigo wa Ajira

4. Unawatisha na kuwakatisha tamaa wawekezaji waliotaka kuwekeza na waliowekeza kwenye media


Gharama yote hii unaingia kisa nguo za Giggy Money!!

Waafrika tujipime akili zetu
Acha uchizi wewe, usiseme waafrika tujipime akili zetu, wewe ndo uende ukajipime akili zako kama zipo sawa.

Yaani YOU ARE TRADING ETHICS FOR MONEY. SHAME ON YOU.

Watoto wa kike wanakaa wanaona kuvaa hivyo ni sawa, hivi ukiwa na mtoto wa kike ukamkuta sebuleni kavaa hivyo af anakwambia ni fashion utamjibu nini. Hujui kwamba wasafi TV inawaangaliaji wengi kwa sasa hasa hasa watoto na vijana? Sawa adhabu inaweza kuwa kubwa lakini usilete visingizio vya kodi na mapato hapa huku mnatuachia kizazi chenye maadili ya kipumbavu.
 
Habari ni kwa mujibu wa tweet ya Swahili Times:

HIVI PUNDE: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha televisheni, Wasafi TV, kwa muda wa miezi sita. TCRA imesema kituo hicho kimekiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui yaliyomuonesha mwanamuziki Gigy Money akionesha utupu wake akiwa jukwaani.
Hawa wasanii wa bongo kwa kuiga mambo ya ajabu hawajambo.
 
Wacha wabwie vidonge tu.

Naamini kila kituo kinapaswa kufuata miongozo ya urushaji maudhui na pia naamini hii miongozo wanapewa na wanaifahamu.

Utetezi wa watu kukosa ajira ni wa kijinga kabisa.
 
Back
Top Bottom