Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Naomba kuulizia kuhusu iringa mjini, sijasikia maeneo yenye hizo mali ila pale iringa mjini kuna wajeruman wengi sana na pia mji wa iringa una mawe na umezungukwa na milima hamna sehemu kwenye hizo mali? Mwenye information plz!!!
 
shimwe iko hivi; utatuletea tunainunua kwa laki tano ( mfano) hiyo moja. Halafu tunakwambia ukipata kama kumi hivi tunanunua kila moja kwa laki nane tuseme. Hizo kumi utazikuta tena kwa washikaji zetu zinauzwa laki tanotano au sita tuseme. Ukishazinunua soko hulioni tena zinakufia mikononi. Rupia moja inajulikana thamani yake kwa shilingi yetu. Tafakari unapigwa soon
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni elimu ya hizo rupia wtz wengi hawana. Kutokana na kukosa elimu wtz wengi wanadharau na kutotafuta taarifa kamili juu ya hizo rupia.

Leo ngoja niwape kwa ufupi kuhusu rupia. Kwanza sarafu hizo ni za mjerumani ambazo zilitumika kipindi cha utawala wao hapa Tanganyika. Hela hizo zimetengenezwa kwa majini na sarafu moja inakadiriwa kuwa na majini 200 hadi 500. Kutokana na sarafu hizo kuwa na majini mengi, zina mashart mengi juu ya utunzaji wake na pia uuzaji wake.

Wtz wengi tunapenda kwenda kutibiwa kwa waganga na wengine hupeleka sarafu hizo kwa ajili ya kusafishwa nyota na mengineyo. Kwa kufanya hivyo kama sarafu hiyo ya rupia ulishaifanyia/ilishafanyiwa mambo hayo tayari kitaalam unakuwa umekwisha iharibu. So ili rupia hiyo iwe safi na iuzike kirahisi ni lazima iwe haijapitia kwa waganga na pie iwe imetunzwa mahali pasafi na hasa kwenye kitambaa cheupe. Pia unapoibeba kwa ajili ya kwenda kuiuza usiweke nia ya kuiuza bali weka nia ya kwenda kupewa zawadi.

Kwa ufupi ni hayo nitaendelea.....

Kwanini kitambaa cheupe?,Nikiiweka kwenye pochi kwani nini kitatokea?.
 
Nimechelewa kuisoma hii mada ila sio mbaya kutokana na mda na siku yenyewe ilivyokaa leo ntaomba niwambie kifupi tu na mim nayojua kuhusu hii topic. Baada ya vita ya kwanza kuisha mjeruman alinyang'anywa makolon yake yote na baada ya kunyang'anywa wakat anaondoka kurud kwao muingereza aliwaambia hamna kuondoka na kitu zaid ya beg lako tu na alikuwa anawasachi wakat wakipanda mel au ndege kurud kwao, hii ndio ilopelekea wajeruman kuficha vitu vyao. Bas nije kwenye mada binafsi rupia nimeiona na maajabu yake ingawa sijaishika kakaangu alitumia miaka 3 kuchimba hiyo rupia ukerewe mwanza na baada ya kurud nyumban akil yake ilikuwa sio sawa na hii ilitufanya tujue ni kwel anayosema? Nilienda had ukerewe kwa rafik zake aliposema kuna hivyo vitu na wanatafta mteja. Walipata rupia nying ila wanazo nane ambazo zina nguvu ya ajabu. Hizo rupia mojawapo nimeiona kwenye picha hapo ya huyo mjeruman mwenye kofia yenye ndege. Hiyo rupia ni nyekundu kama shaba na pia ina sumaku na ina vuta coin nyingne na vitu chuma vidogo dogo na pia hiyo coin ukichukua blastic uweke maji na yenyewe ikae chin bas ukiweka coin yoyote juu yake haizam inaelea na bdae inatupwa nje ya kibakul. Na sio kila mtu anaweza kushika hiyo rupia huwa inapotea na kuna makabidhiano wakat inavyotoka kwa mtu kwenda kwa mwingne kuna kafara lazima zifanyike ndo uimilki. Ukiachana na rupia kuna pas kama ya mkaa ambayo ni nzito na hii inafanya kaz inaweekwa juan tu unanyooshea, taa ya chemry hii ipo kama iyo pas nayo, saa ya ukutan na pia walipata bunduki (rifle) na risas zake nying. Kwaiyo sio kitu ambacho ni imagination ila kweli kipo. Inasemekana kwel rupia imechanganywa na damu na mifupa ya watu ila sio zote ni hizo chache ambazo nimesema hapo juu. Watu wamekuwa wakitapelewa kwel sababu rupia ni hela ya kawaida ukiachana na hiyo maajabu. Kaka angu ameniambia walienda had kigoma kupewa dawa kwa waganga ili waweze kuingia kwenye ilo shimo. Na kwel baada ya kupata hivo vitu walisumbuka sana ni kama waliiba ile mizimu iliyoachwa pale iliendelea kuwasumbua had walipoenda tena kufanyiwa matambako kibao. Hivyo vitu wanavyo kabisa ila hadi sasa nakwambia hamna mteja ambaye wamepata na vitu wanavyo tu. Sasa ukija kiundan hivyo sio vitu vya kufuatilia hata kidogo vimezungukwa na nguvu ya giza ambayo sio nzur. Tutafute ela kwa njia halal na sio had kwa waganga au vitu vyenye nguvu ys giza sababu tunapita tu hapa dunian. Bro tulimkalisha chin tukamwelekeza ila hakuelewa na yupo bdo anaangaika na wenzake kutafuta wateja wengi mashart na bei wanayouza vimewashinda.

Mkuu, bado jamaa zako wanavyo hivyo vifaa ??
 
Miaka ya 90 hiyo ndio ilikuwa deal. Rupia zipo maeneo ya singida.arusha.tanga nk. Kama walivyosema wadau kinachotafutwa pale ni yale majini yaliyoko ndani. Story ni kuwa hayo majini yamekuwa traped pale. Kuyafree inaitwa kubangua. Yanapotolewa yakupa zawadi. Inaweza kuwa pesa nyiingi. Au unaweza usitake kuyatoa yakakutumikia. Ila unaishia kuyatumikia. Walio na hizo rupia wanazitumia kukutapeli. Unanunua unalipa na unaondoka. Ukifika njiani inakuwa imepotea. Ukirudi unaikuta kwa mwenyewe. Thubutu kudai pesa yako uone. Jamaa kufumba na kufumbua walitolewa Singida hadi Arusha. Hizi huku mjini za kuganga njaa. Rupia yenyewe ukianza safari mwenyewe anajua kuwa unakuja. Sio biashara ya kufanya kabisaaa. Itakufilisi na sio rahisi kukutana na mnunuzi mwenyewe. Kila mtu ni dalali wa kusikia tu. Pili kipimo chake cha kujua feki na origino kiko na mnunuzi. Unafika na mzigo unaambiwa hii sio. Watu wameingia misikitini na makanisani lakini yote sio.
Huko upareni ziko ila haziendi mjini. Chunga saana.


Bado huna elimu ya unakichosema. Kwanza tafuta elimu yake then fuatilia kwa umakini mbona hata kwenye kuuza korosho kuna utapeli ?
 
Back
Top Bottom